Dodoma: Adaiwa Kumuua Mkewe kwa kumchoma kitu chenye ncha kali shingoni

Inakuwa ni sababu muhimu kwa wale wenye akili kisoda. Kwa akili ya kawaida ingefaa wenye ndoa wajisemee nafsini mwao kwamba Niliingia humu Ndoani mm mwenyewe kwa hiari yangu na sio kwa shinikizo la Jamii. Kwa hiyo Jamii inione kama itakavyoniona potelea mbali. Msimamo wangu utabaki palepale
Akili visoda wako wa kutosha! Huwezi kuwatenga katika mijadala inayowahusu.
 
Kuna mambo kadhaa yanayopelekea uvumilivu kwenye ndoa hata kama wanandoa hawaelewani;

Mosi, kutunza viapo; pili, mtazamo wa kijamii - tukiachana jamii itatuonaje; tatu, watoto - tukiachana watoto watateseka; nne, hofu ya maisha - nitaanzaje maisha mapya? Nitaolewa/oa tena? Tano, kweli hamuelewani lakini moyoni bado unampenda hasa kwa wanawake, nk.

cocastic, Lamomy, ShesRise_1 ni wazamivu wa hizi mambo.
Kama wangekuwa wanatunza viapo, wasingefikia sehemu ya kutendeana mabaya. Kutunza viapo kunaanza kwanza kwa kutendeana mema sio kung'ang'aniana mkishatendeana mabaya. Kama hamna upendo,maana yake hamheshimu viapo vyenu.
Hapo kwenye mtazamo wa kijamii, hata ufanyeje jamii haitaacha kuongea. Ukishakufa kwa ajili ya ndoa, jamii hiyohiyo itasema kwa nini hukutoka kwenye hiyo ndoa wakati upo hai.
Hapo kwenye watoto watateseka, kama wanandoa hamna maelewano watoto watateseka tu haijalishi mnaishi pamoja au mbalimbali. Kuna watu wanapigana hadi watoto wanasikia, hayo sio mateso?. Na mbaya zaidi mmoja akishaenda jela na mwingine kaburini ndo watoto watateseka zaidi. Sasa si bora mtengane tu kuliko kuacha watoto yatima?.
Hapo kwenye kuanza upya, ukiwa kwenye hatari cha muhimu ni kujiokoa na kuwa salama, haya mambo ya sijui nani atanioa tena ni mambo ambayo hayapaswi kupewa kipaumbele kwa wakati huo. Uhai kwanza, mengine yatajijua baadae.
Mwisho, upendo sio sababu ya mauti au jela, kama unampenda mtu halafu hakupendi, usimlazimishe.
 
Nimekuelewa! Kwenda jela au kaburini ni extreme results. Kwa kawaida hakuna anayekuwa ametegemea "tutafika huku".
 
Akili visoda wako wa kutosha! Huwezi kuwatenga katika mijadala inayowahusu.
Sasa wanashindwa wapi kutofautisha Jambo la Kijamii na Jambo la Kibinafsi??
Ndoa ni jambo la kibinafsi na sio la kijamii.
 
Kuna tatizo la Afya ya akili kwa watanzania wengi kwa Sasa. Serikali ifanye jambo, kuua imekua jambo rahisi sana. Sasa huyu kaua na kalala na maiti mpaka asubuhi.
Serikali ipi ifanye jambo mkuu, wao wenyewe wamekuwa vinara wa kuuwa na kupoteza waty, wana nguvu gani ya kusimamia mauaji yanayotokea kwa wanandoa.

Afya ya akili ni changamoto from top to bottom.
 
Sasa wanashindwa wapi kutofautisha Jambo la Kijamii na Jambo la Kibinafsi??
Ndoa ni jambo la kibinafsi na sio la kijamii.
Acha tu brother! Jamii is so complex kiasi kwamba hakuna na hazitatokea tafiti kuhusu social behavior zikaweza kuitolea majibu kamilifu. Wajinga na kila aina ya "takataka" zitaendelea kuwemo hadi ukamilifu wa dahari.
 
Nimekuelewa! Kwenda jela au kaburini ni extreme results. Kwa kawaida hakuna anayekuwa ametegemea "tutafika huku".
Inafikirisha. Hivi unapanda mchicha halafu unategemea mwisho wa siku uvune tembele? Migogoro ndani ya nyumba(Ndoa)isiyoisha ndo chimbuko la kuwepo kwa matukio maovu kama haya. Wahenga walisema: "ukiona moshi; ujue chini kuna moto". Migogoro ndani ya Familia hata baina ya Nchi/Mataifa mwisho wake huweza kuzaa Vita.
 
Mkuu likikukuta tukio kama hilo; hiyo ni Fursa kwako ujiulize sana ni kitu gani hicho Mke wako anakisotea sana kukipata kutoka kwako ilhali waote mpo ndani, halafu kumbe anaweza kukipata kwa msela tena vichakani nyuma ya nyumba yako???
Demu akikuelewa haijarishi anakipata au hakipati kikubwa yeye ni kutekeleza unyambilisi wake
 
Inafikirisha. Hivi unapanda mchicha halafu unategemea mwisho wa siku uvune tembele? Migogoro ndani ya nyumba(Ndoa)isiyoisha ndo chimbuko la kuwepo kwa matukio maovu kama haya. Wahenga walisema: "ukiona moshi; ujue chini kuna moto". Migogoro ndani ya Familia hata baina ya Nchi/Mataifa mwisho wake huweza kuzaa Vita.
Kwanza, kuna thinking ya " let's hope for the best"; atabadilika hali ambayo huzaa kuvumiliana. Pili, process ya kuachana isn't an overnight issue - it takes time including social intervention - tuachane vizuri.

Na hata kama ungeamua kukatisha mahusiano ghafla wewe ndiwe utaonekana chanzo cha migogoro hali ambayo wengi hawaipendi.

Matrimonial issues are a bit complex than they might be taken at a glance!
 
We bhana.. kusema kuna pepo la taifa linaandama labda tupo pamoja.. Maana damu imemwagika shekhe.!

Mimi nimesikiliza na kuamini kabisa Wife akitongozwa na Mume wa mtu kwa phone ..!? Bora hata angekuwa boda au mla skanka ningesema uchu umemponza wife labda sifanyi vizuri na ningemsamehe.🤔

Eti skrepa mume ba mutu kweli.! Itoshe kusema wife ni mnafiki na malaya aliyetengenezwa kwao kwa wivu mkubwa kuwanyanyua vigagula vya kwao kwa utapeli wa familia na ndoa
Wanawake ni kawaida kutongozwa, tena ukiwa na mke mrembo anaweza kutongozwa hata mara 3 kwa siku

Ni uamuzi wake kuwakubalia ama kuheshimu ndoa yake

Pamoja na hayo, hutakiwi kumuua unapogundua ametongozwa ama kuchepuka

Adhabu inayomfaa ni kumuomba muachane tu ili Kila mmoja akaishi maisha yake

Unapoamua kumuua, ni kujipotezea maisha maana lazima utafungwa
 
Nimekuelewa! Kwenda jela au kaburini ni extreme results. Kwa kawaida hakuna anayekuwa ametegemea "tutafika huku".
Lakini mkuu,dalili siku zote huwa zinaonekana, shida ni watu wanapuuzia hizo dalili. Mfano yule Jeni, aliona kabisa hapa naenda kuuwawa na hata aliwaambia ndugu zake. Na hata huyu wa Dodoma, mume wake aliwahi kutamka hayo maneno na alikuwa akimpiga mara kwa mara. Ukishatishiwa maisha cha kwanza ni kukaa mbali ili kuokoa usalama wako.Huyu dada wa Dodoma alibembelezwa na ndugu atoke hapo ila akaendelea kubaki.
 
Kwanza, kuna thinking ya " let's hope for the best"; atabadilika hali ambayo huzaa kuvumiliana. Pili, process ya kuachana isn't an overnight issue - it takes time including social intervention - tuachane vizuri.

Na hata kama ungeamua kukatisha mahusiano ghafla wewe ndiwe utaonekana chanzo cha migogoro hali ambayo wengi hawaipendi.

Matrimonial issues are a bit complex than they might be taken at a glance!
Kuachana ni process ndefu mkuu nakubali, ila unaweza kuamua kukaa mbali na mtu huku ukikamilisha taratibu nyingine. Na hapo pa wewe kuonekana chanzo cha migogoro, ni kufanya maamuzi ya kujijali mwenyewe. Hata hao watu watakaokusema vibaya sijui umevunja mahusiano, yakikukuta majanga watasema kwanini ulibaki kwenye ndoa ya mateso. Huwezi kuridhisha watu hata ufanyeje,jitazame mwenyewe.
 
Lakini mkuu,dalili siku zote huwa zinaonekana, shida ni watu wanapuuzia hizo dalili. Mfano yule Jeni, aliona kabisa hapa naenda kuuwawa na hata aliwaambia ndugu zake. Na hata huyu wa Dodoma, mume wake aliwahi kutamka hayo maneno na alikuwa akimpiga mara kwa mara. Ukishatishiwa maisha cha kwanza ni kukaa mbali ili kuokoa usalama wako.Huyu dada wa Dodoma alibembelezwa na ndugu atoke hapo ila akaendelea kubaki.
Kwenye post #263 nimeeleza sababu kadhaa kwanini inakuwa hivyo. Ndoa pamoja na uchache wa key players, kidogo ni kataasisi flani hivi very complex.
 
Ila yote kwa yote,Haya mambo wala sio ya kujivunia, kufurahia au kuchukulia kawaida

Pombe ni hatari na afya ya akili is really.
 
Kuachana ni process ndefu mkuu nakubali, ila unaweza kuamua kukaa mbali na mtu huku ukikamilisha taratibu nyingine. Na hapo pa wewe kuonekana chanzo cha migogoro, ni kufanya maamuzi ya kujijali mwenyewe. Hata hao watu watakaokusema vibaya sijui umevunja mahusiano, yakikukuta majanga watasema kwanini ulibaki kwenye ndoa ya mateso. Huwezi kuridhisha watu hata ufanyeje,jitazame mwenyewe.
Tukirejea mfano wa yule Jeni wa Urassa unajua alikuwa haishi na Kweka kwa muda? Alikuwa amehama kabisa nyumbani? Mistake ya siku moja kurudi nyumbani ilikatisha uhai wake pamoja na tahadhari alizokuwa anachukua. Siku ikifika utaitwa kwa lugha nzuri na upendo wa ajabu wala huwezi kudhania!
 
Kamuwa alafu akalala naye
Aise,
Soon wanawake nao watakuja na come back yao

Ova
 
Tuanze kulala kimachale saivi

Ukiona umegombana na mkeo, bora ukalale guest house tu, itakuepushia vingi
 
Back
Top Bottom