Tungeambiwa kwanza kama ile IGA inayozunguka mitandaoni ni ya ukweli au uongo? Hilo la TPA kuachiwa gati chache kuziendesha hata Mbowe alilizungumzia.
Amandla...
Serikali inajichanganya sana katika hili.
Katika Clubhouse ya Msigwa, Msemaji wa serikali (Msigwa) ameikana. Hapo hapo alikuwa na CEO wa TPA, kila kifungu anachokisema na kukinukuu CEO kipo katika ile ya mtandaoni. Kifungu kwa kifungu.This was a contradiction.
Hata kama huu mkataba ni mzuri na una manufaa kwa umma na raia wengi sana wanaweza kuutetea, serikali inavyofanya usiri, usiri huo unatoa ishara kwamba kuna jambo baya.
Kwa nini mikataba hii haiwekwi wazi?
Nature abhors a vacuum, katika Information Theory tunafundishwa kwamba, usipoweka habari sahihi wazi, unaalika habari zisizo sahihi zisambae. This is PR 101, somo la awali kabisa katika PR. Kwa nini serikali inaendekeza usiri? Ni kwa sababu sisi ni washamba sana tunaendekeza usiri wa kizamani?
Au ni kweli usiri unatokana na ukweli kwamba serikali inajua kuwa mikataba ikiwekwa wazi na kukubaliwa na serikali kuwa hii ndiyo mikataba yenyewe, wananchi wataikosoa na kuonesha mapungufu?
So, huu ni ushamba, hadaa ya wezi au yote mawili pamoja?
Kama mkataba una manufaa sana kwa wananchi, kwa nini usiwekwe wazi?
Kwa nini uliwekwa kwenye tovuti ya bunge halafu ukatolewa? Bunge halijui kwamba wananchi wanaweza kuwasaidia sana wabunge kujadili mkataba?
Kwa nini Msigwa aliukataa Clubhouse? Kama huo alioukataa Msigwa si wenyewe, wenyewe uko wapi?
Wananchi wana haki ya kikatiba (ibara ya 18 (1) na (2) ) ya kujua jinsi nchi yao inavyoendeshwa. Serikali haioni kwamba inavunja katiba kwa kupitisha hii mikataba bila kuwaonesha wananchi mikataba inasemaje?