Dodoma City vs Arusha City (The Battle of Tanzania Capital City vs EAC Capital City)

Usiwe mbishi ,mipaka ya jiji la dodoma imechukua mpaka vijiji vya mbali kama vile hombolo zaidi ya km 30 kutoka mjini lakini kiuhalisia ni porini ,arusha ni tofauti kuna maeneo ya wilaya ya arumeru na arusha dc mfano tengeru ,usa river ,maji ya chai,ngara mtoni kitakwimu za sensa hayapo arusha jiji yangeingizwa jíji arusha population ingekua kubwa sana
 
Ila hombolo ipo jiji na niporini zaidi ya km 30
 
Mzee ukiwa unaongea uwe na fact na usiwe muongo, tangia lini Abuja ikawa mji wa 2 kwa ukubwa Nigeria[emoji1484], Dodoma ukiacha Makao makuu akuna mfanyakaz wa Serikali atakae Kaa pale mji haujakaa kistarehe kabisa
 
Toa upuuzi wako hapa,Dodoma Kama Mkoa Wakaazi wake wengi wako Kwenye Wilaya zipi?

Ukiacha hivyo Vijiji ikachukua Chamwino unajua watu watakuwa wangapi? Maana Mji wa Serikali uko Wilaya ya Chamwino sio Jiji la Dodoma.

Mwisho Dom kama jiji metropolitan yake ni sehemu kubwa sana ndio maana Kuna Mpango wa Manispaa ya Chamwino so hata Arusha ichukue Kata za Usariver sijui Kisongo Bado population yake haiwezi kufikia Dodoma.
 
Haya miaka ya badae yatakuwa magofu..hivi unadhani ukiacha na shughuli za kiserikali nani anataka Aishi Dodoma?
Hicho ni Chuo Magofu gani? Magofu how?

Watu wanaishi Egypt jangwani sembuse Dom? Watu wanafuata fursa na pesa na sio hizo blaa blaa.

So Wacha ndoto za mchana kijana kisa wivu kubali tuu Arusha ni Kijiji Cha Utalii tuu Kwa Dom 🤣🤣🤣🤣
 
Abuja sio Mji wa kila nyumbu kwenda Kuishi.

Hata hivyo Abuja iliundwa specifically kama Mji Mkuu wa Serikali purely Sasa tofauti na Dom ambayo upande ni Mji wa Serikali na upande Mji wa biashara na viwanda.

Kwa mantiki hiyo Dodoma haitakuja kuwa kama hizo Miji Zingine na vile uko junction ya Barabara kuu ndio kabisaa utazidi kupaa.
 
Vile Dom itakuwa baada ya Kukamilika Kwa Outer ring road harafu Vijiji vya Arusha na Mwanza vikisalia kama makambi ya wakoma 😁😁
 
Lami ndio natural environment? Mfano angalia tu mazingira yalivoView attachment 2686314
Naona unaruka ruka tu kuhamisha magoli😀😀😀.Mwanzo umesema Dodoma Jiji hakuna barabara za lami nikakuchapa na facts kuwa Dodoma ndio Jiji pekee lenye mtandao mrefu wa barabara za lami ndani ya CBD,sasa umekuja na ishu nyingine ya natural environment😀😀.Majiji ya kisasa yaliyoendelea huwa hayapimwi kutokana na kigezo cha hali ya hewa...angalia Gaborone,Windhoek,Cairo,Tel Aviv uone
 
Arusha na Mwanza wakiona hivi watanuna , watakwambia Dodoma.hakuna uoto 🤣🤣🤣
Hawa jamaa wanachekeshaga sana wanakwambia Dom ni jangwa lakini nikiangalia kule kwa Waziri Mkuu Area D Mlimani naona miti ya kutosha kijani mwaka mzima.Barabara za Dom nyingi pembezoni zimepandwa miti ya kupendezesha mfano Arusha Road,Nkuhungu four ways,Iringa Road,Veta Road,Udom Road,Kisasa Road n.k
 
Kwanza sahihisho, jiji la Dodoma ni la pili kwa idadi ya watu ikifuatiwa na Arusha. Mwanza ni jiji na nne kwa idadi ya watu, karejee sensa ya 2022. Usichanganye jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela hayo ni maeneo mawili tofauti ya maeneo ya kiutawala. Hata Mkoa wa Dar kuna jiji na kuna manispaa kama nne. Mislazimishe kajiji lenu hilo la Mwanza ukweli ni kuwa ni dogo kuliko jiji la Arusha.
 
Usilinganishe vitu ambavyo havilingani, Dodoma imejengwa na serikali, majengo yote hayo makubwa ni ya serikali. Arusha imejijenga yenyewe. Havina na ulinganisho. Bila serikali Dodoma ingezidiwa na manispaa nyingi na wala isingekuwa jiji
 
nchi hii sijui ujinga utaisha lini. Watu kwa ujinga au kwasababu zao hasa ujinga wanachanganya maeneo ya kiutawala. Kwa mujibu wa sensa ya 2022, Mkoa wa Dar Es Salaam una idadi ya watu 5,383,928, hii idadi siyo ya jiji. Idadi ya watu ktkt majiji na rank zao hapa nchini ni km ifuatavyo:
1. Dar Es Salaam - 1,649,912
2. Dodoma - 765,179
3. Arusha - 617,631
4. Mwanza - 594,834
5. Mbeya - 541,603
6. Tanga - 393,429.
Msichanganye population ya Ilemela na ya jiji la Mwanza, jiji la Mwanza ni eneo la Nyamagana km jiji la Dar ni eneo la Ilala, ndiyo maana ktkt sensa huwezi kuona idadi ya watu wa Ilala wala wa Nyamagana. Jiji la Mwanza ni dogo tu imekaribiwa hata na jiji la Mbeya. Rejea kitabu cha ripoti ya sensa ya mwaka 2022.
 
Hiyo ni mojawapo wewe na ndio inayovutia watu kwenda kuishi na kutafuta Fursa kwa Tanzania ukimuliza mtu yoyote awezi kukwambia ana ndoto ya kwenda kuishi Dom ,Bali ni utaskia kama sio Mwanza ,Arusha ,mbeya au dar kutokana hali ya hewa ya kuvutia
 
Dodoma tuma Picha ya CBD tuone au unadhan hatupajui huko..huko ni jangwani
 
Ukweli mchungu Arusha kashapigwa parefu..

Nimeona baadhu ya nyumba zimepigwa landscaping nzuri na kuoteshwa maua ya kijana na huko Dodoma kwa kweli pesa unaongea.

Miaka 10 ijayo tukija kwa facts na logics kabisa Dodoma litakuwa jiji la pili.
 
Kwamba unataka kusema Abuja hamna viwanda?! Tuna Rudi pale kwenye fact kwamba Dodoma sio mji wa kuishi na huwezi kumvutia mwekezaji kuishi na kujenga dodoma kutokana na nature yake ilivo
 
Mwanza nitofauti na majiji mengine, ina kilimo, uvuvu, madini lkn uwepo wa viwanda pia unaleta ahueni

Arusha kidogo msimu wa utalii huwa inafunguka ila Dodoma ina nini ukitoa bunge na vyuo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…