Dodoma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ashiriki ibada Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska

Dodoma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango ashiriki ibada Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska

Asante Mungu!, maana!. Kwa vile tulielezwa kuwa yupo nje ya nchi kikazi, na VP akiwa popote kufanya lolote ni kumwakilisha rais, hivyo tulitegemea siku akirudi, apokelewe, aonekane akitoa mrejesho wa safari kwa aliyemtuma!, kama jana alikuwa Dodoma, alitarajiwa kuonekana pale uwanjani kwenye maadhimisho ya uhuru!.

Hata hivyo asante kwa hii picha roho zetu zimetulia, ngoja nipitie meta data za hii picha kuithibisha ni ya leo!.

Asante tena.

P
Mkuu karejea nchini leo na moja kwa moja akaenda kanisani pale pale airport ya Dodoma. Unajua kwanini katua Dodoma moja kwa moja? Pia ni kweli kuwa alikuwa nje ya nchi ila ni kwa matibabu. Mimi ninachojiuliza kwani kuugua ni dhambi mpaka wafiche?
 
Mlokua mnamzushia kifo mna hali gani?Mlokua mnatangaza na kujiapiza kwamba akionekana mtafuta page zenu mshafuta?Mlokua mnapiga ngoma ya nchimbi na kuanza kumpost mpo wapi?Huwezi kushindana na Mungu hata kidogo!! Kwa mara nyingine wahuni na genge lenu mmefail again!!

Kama mnadhani mtafanikiwa kama mlivyofanikiwa kipindi kile basi safari hii mmechemka Mungu wetu hawezi kuruhusu hilo liwe labda atake yeye

Hii tabia ya kuzushia watu vifo siyo nzuri hata kidogo!! Na ingekua ni busara hawa wahuni washughulikiwe humo humo ndani ya chama na mtandao wao!!Lakini inakua ni vigumu maana wana mizizi kila mahali.

=======

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Mapadre mara baada ya kushiriki Ibada ya Jumapili ktk Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo Desemba 10, 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo, Dk Mpango amewaasa Watanzania kutumia vema mitandao ya kijamii.

Amesema matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii yamekuwa yakiumiza watu wengi hivyo yampasa kila mmoja kutumia vema pamoja na kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais amewashukuru waumini hao kwa kuendelea kumuombea ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.
View attachment 2838329

Ahaaa!amesema alikuwa wapi?
 
Baba ....So happy to see him!Mungu akutunze,akulinde na akuepushe na kila baya.Uishi sana Dr.Mpango.
 
Asante Mungu!, maana!. Kwa vile tulielezwa kuwa yupo nje ya nchi kikazi, na VP akiwa popote kufanya lolote ni kumwakilisha rais, hivyo tulitegemea siku akirudi, apokelewe, aonekane akitoa mrejesho wa safari kwa aliyemtuma!, kama jana alikuwa Dodoma, alitarajiwa kuonekana pale uwanjani kwenye maadhimisho ya uhuru!.

Hata hivyo asante kwa hii picha roho zetu zimetulia, ngoja nipitie meta data za hii picha kuithibisha ni ya leo!.

Asante tena.

P
Tuthibitishie kama ni ya leo....Mungu ni mwema
 
Katika siku za hivi karibuni kumetokea habari nyingi saaana mtandaoni baada ya kutokuoneka kwa Makamu wa Raisi Dk. Philip Mpango.
Kwa upande wangu kuna wajibu wa kufanya ,kwa serikali, na kwa wananchi
Kwa serikali inapaswa kutoa taarifa kwa wananchi wake juu ya viongozi wake ,hasa yuko wapi, anafanya nini kwani wananchi wana haki ya kufaham alike kiongozi wao
Kwa wananchi nako kuna shida, tumekuaje yaani mtu asipooneka kwa muda ni tayari amefariki, hizi roho tumezotoa wapi ? Kwani tunafikiria juu kifo tu?? Ni kweli kifo kipo lakini ndiyo tuwawazie watu?
Nasawasilisha
 
Attachments

  • Screenshot_20231210-104505_Instagram.jpg
    Screenshot_20231210-104505_Instagram.jpg
    151.2 KB · Views: 2
Mzee alikuwa nje kutekeleza majukumu yake ya kazi, mbona karudi kimya kimya hata jana hakuonekana Dodoma kwenye tukio muhimu?
Ama tuseme karudi usiku akadamkia Kanisani?

Mnatupanga kama kwa Jiwe ila tumeshajua ninyi ni washenzi
 
Asante Mungu!, maana!. Kwa vile tulielezwa kuwa yupo nje ya nchi kikazi, na VP akiwa popote kufanya lolote ni kumwakilisha rais, hivyo tulitegemea siku akirudi, apokelewe, aonekane akitoa mrejesho wa safari kwa aliyemtuma!, kama jana alikuwa Dodoma, alitarajiwa kuonekana pale uwanjani kwenye maadhimisho ya uhuru!.

Hata hivyo asante kwa hii picha roho zetu zimetulia, ngoja nipitie meta data za hii picha kuithibisha ni ya leo!.

Asante tena.

P
Ujue itakuwa La Mitume vs Luther King 😂😂

Bakuata wanazoom tu!
 
Back
Top Bottom