Dodoma, Mbeya, Mwanza na Tanga sio majiji; zirudishwe kuwa halmashauri au manispaa

Dodoma, Mbeya, Mwanza na Tanga sio majiji; zirudishwe kuwa halmashauri au manispaa

Nimesafiri kwenye maeneo tajwa hapo juu katika siku za hivi karibuni na ninathibitisha kwamba hayo sio majiji.

Hizo ni halmashauri tu na labda juu sana ni manispaa lakini sio zaidi ya hapo. Vigezo viboreshwe ili nchi itoe hadhi ya mahali kulingana na uhalisia.

Nyumba zimesambaa kama takataka na miundombinu ni hatarishi katika maeneo haya. Hali ya maisha sio nzuri.
Majiji yote ni hovyo tu kwanza machafu mno
 
Nimegundua watu hawajui Halmashauri ni nini , Mji, Jiji, Manispaa n.k
 
Vatican city kuna watu hawazidi elfu kumi,kwa nini isiitwe vatican village
Unapozungumzia Vatican city unazungumzia kitu chenye utata, "Ambiquious phenomenon".
Jina "Vatican city" lisikuchanganye, hiyo ni nchi kama zilivyo nchi nyingine, kama vile USA, Urusi, Canada nk, ndio maana Tanzania kuna ubalozi wa Vatican.
Kama hauangalii hali ya maisha, mpangilio na mazingira basi hakuna vigezo hapo.
Mpangilio na mazingira? I see. Yaani kukiwa na mazingira mazuri na mpangilio hata kama ni kaeneo kadogo ka watu ishirini kaitwe jiji? Ulishawahi kufika Moshi? Mpangilio ni mzuri sana na mazingira ni masafi sana, mbona haipewi hadhi ya jiji?

Unaposema kuangalia hali ya maisha ndio kufanya nini? Kwamba kama maisha ni marahisi ndio iitwe jiji au kama ni magumu? Hoja zako zimenisikitisha sana!
 
Nimesafiri kwenye maeneo tajwa hapo juu katika siku za hivi karibuni na ninathibitisha kwamba hayo sio majiji.

Hizo ni halmashauri tu na labda juu sana ni manispaa lakini sio zaidi ya hapo. Vigezo viboreshwe ili nchi itoe hadhi ya mahali kulingana na uhalisia.

Nyumba zimesambaa kama takataka na miundombinu ni hatarishi katika maeneo haya. Hali ya maisha sio nzuri.
Kwa Mwanza umechemka, wewe ni wale mnaokwenda mahala unalala hotel kunakucha baada ya siku tatu mnaondoka kijijini kwenu
 
Mbeya sio jiji aiseeh

Siku nafika nilishangaa Sana Sana inakuaje sehemu ya Hovyo namna Ile inakuwa ya jiji.

Na Tanga eti nalo ni jiji hehehe
 
Mmh usafi wa mazingira ni kigezo pia Mkuu.
Ok, ngoja tuvumiliane tujaribu kuelekezana taratibu.

Wewe unakaa mkoa gani?

Mimi nakaa Dsm lakini nimekaa mikoa mingi sana, namaanisha kukaa, sio kupita.
Usafi wa mazingira ingekuwa ni kigezo, Dsm isingekuwa jiji.
Dar es salaam ndio mkoa mchafu wa mazingira almost kuliko mikoa yote Tanzania.
 
Mbaya zaidi unalikuta kwao ni huko Uyole ndani ndani ila lilikimbilia Dar... Yanasemaga eti watu wa mkoani, majinga kama nini
Ulishawahi kufika Uyole? Unapoitaja Uyole itaje kwa heshima. Ni mojawapo ya maeneo mazuri sana katika jiji la Mbeya.
 
Upandishaji wa majiji uliwekewa vigezo, ila vigezo vya kisiasa pia vilikuwepo ila havikuwekwa wazi ulikuwa under the capet. Usishangae unachokiona kwenye majiji hayo uliyoyataja kwani hii ni TZ. Makazi ya watu zamezidi uwezo wa serikali kupanga and kuwaletea wananchi huduma stahiki kwa wakazi wa majiji hayo. Mikoa ilipigania miji yao kuwa majiji kwani mgao wa keki ya Tiafa ni kubwa kuliko kwa halmashauri na manispaa. But, kiini cha yote haya ni Serikali kuu kukumbatia kila kitu na kutokuwapa nguvu mikoa/miji kujiendeleza bila kuingiliwa na serikali kuu. Serikali kuu imeingilia mapato yote ya miji yote na kuyakusanyia mfuko mmoja ambao kwa sasa huitwa mfuko wa Rais alie madarakani, kuanza kugawa kwa hisani na sio kufuata budget ilivyopangwa na basically on political grounds/personal.
Hahaaa hivi kuna jiji ambalo halina halmashauri
 
Mbeya sio jiji aiseeh

Siku nafika nilishangaa Sana Sana inakuaje sehemu ya Hovyo namna Ile inakuwa ya jiji.

Na Tanga eti nalo ni jiji hehehe
Kama unatafuta maghorofa marefu Mbeya hutayapata, ila Mbeya ni mojawapo ya miji mizuri sana, unless useme uhovyo wake ni nini..
 
Ok, ngoja tuvumiliane tujaribu kuelekezana taratibu.

Wewe unakaa mkoa gani?

Mimi nakaa Dsm lakini nimekaa mikoa mingi sana, namaanisha kukaa, sio kupita.
Usafi wa mazingira ingekuwa ni kigezo, Dsm isingekuwa jiji.
Dar es salaam ndio mkoa mchafu wa mazingira almost kuliko mikoa yote Tanzania.
Wakati inapandishwa hadhi haikuwa hivyo Mkuu ndio maana unaona nguvu kubwa sana inaelekezwa kwenye Hilo eneo
 
Ulishawahi kufika Uyole? Unapoitaja Uyole itaje kwa heshima. Ni mojawapo ya maeneo mazuri sana katika jiji la Mbeya.
Unadhani ukisema Dar es Salaam mahala pote ni pazuri? Mbona mko majinga majinga sana nyie waTanzania
 
Ni kweli kabisa vigezo vilivyotumika ni vya kisiasa zaidi. Mahali panaitwa jiji lakini ardhi katikati ya hilo jiji haijapimwa na makazi ni holela.

Miundombinu ya barabara, maji safi na taka na usafi wa mazingira ni hatarishi kabisa. Yaani hizi ni halmashauri tupu, hakuna jiji hapa.
Hahaaa sio jiji ni halmashauri hivi kuna jiji lisilo na halmashauri unaonekana hujui maana ya halmashauri,
 
Tanga, Dom na Mbeya big no.
Siyo small No?

Ninachokwazika kwenye huu uzi, watu mnaochangia hamuelewi hata vigezo vinavyotakiwa mnapuyanga hovyo tu, kama hujui kitu ni bora kuuliza, siyo kuandika vingereza vya kinanilii eti big no!
 
Safari inakuwa ndefu zaidi pale ambapo maeneo ambayo yako kwenye hatua za ujima yanapoitwa majiji.

Dar kuna maeneo hovyo lakini angalau kuna maeneo ukipita unasema hili linaweza kuwa jiji.
Kwani mkuu dar ilipokua jiji ilikua na muonekano gani ?,vigezo vilivyotumika ndio vilivyotumika kuipa tanga jiji
 
Back
Top Bottom