Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Dodoma muanze kuweka na showrooms sijui kama zipo
 
Dodoma sio rahisi kuipiku dar es salaam hata kidogo . Dar es salaam ndio business hub ya Tanzania na Africa mashariki . Mji wenye bandari, airport , viwanda na ni gateway ya eat and central Africa.
Dodoma itakuwa second largest city by 2030, huko mbeleni watakuwa wanafukuzana na Dar.
 
Unashid wewe Hadi udom unahesabu
Kwani UDOM ipo Chamwino,Kondoa au Mpwapwa si ni Dodoma Jiji ndiomana nina wasiwasi hujawahi kufika Dom au kama ulifika ulikatisha na basi tu wakati unaelekea mkoani kwako 😆 .Punguza chuki kwa Dom huku ni Jamiiforums sio Facebook watu tunabishana kwa facts+points sio mihemko
 
Itakuwa hujafika Dodoma toka huu mwaka uanze mkuu .
Huyo kasimuliwa tu hajawahi fika...eti anakwambia maghorofa ya mfano Tambukareli kama BOT,HAZINA,TAKWIMU,PSSF KAMBARAGE,NHIF,PPRA,OSHA,SEKRETARIATI YA AJIRA,JKIC,NAOT,ERB,UHAMIAJI nk.ni nje ya mji😂😂😂😂 wakati kutoka Nyerere Square mpaka BOT kwa gari ni mwendo wa dakika 5 tu.

Tanzania hii hakuna mji wowote unaofikia Dom hata robo kwenye ubora wa mipangomiji na ubora wa miundombinu huo ndio ukweli mchungu.
 
Dodoma kweli kwenye mipango mingi wamejitahidi, kuna maeneo machache kama Mipango ndo nyumba zimejengewa bila mpangilio. Hata Area A ambapo sasahivi kuna nyumba zimechakaa na penyewe nyumba ziko kwenye mpangilio, sio kama Dar nyumba zimejengwa bila mpangilio hata Goba tu hapo nyumba hazina mpangilio. Dodoma ukienda sehemu mfano Kisasa hadi moyo unaburudika, unaona kweli hili ni eneo la makazi ya watu.
 
Mwenye 8mil aje nimuuzie nusu heka ipo 8km toka ukuta wa ikulu, 14km toka mji wa kiserikali mtumba 0656399870
 
Hapo palipo Makao Makuu ya Mahakama - Judiciary Square, kumejengwa haswa
Kwa kuongezea wajitahidi Miti na garden kuongeza mvuto wa mazingira na pavement ziwe za kueleweka kuwe hakuna vichaka na vumbi.
 
Dodoma slums ni za kutafuta na torch.

Pia, sewage system ipo vizuri kutokana na mpangilo wa makazi, hakuna harufu chafu kama Dar.
 
Dodoma slums ni za kutafuta na torch.

Pia, sewage system ipo vizuri kutokana na mpangilo wa makazi, hakuna harufu chafu kama Dar.
Hapo kwenye sewage system na harufu toa Area A, pale kila siku maji machafu yanatiririka,miaka nenda miaka rudi. Ila huko pengine kama Ilazo,Kisasa, burudani hakuna harufu wala maji machafu.
Kuhusu kutokuwepo kwa slums kweli Dodoma ni ya mfano, mahali pekee panapofanania na slums labda ni baadhi ya sehemu za Chang'ombe, na slums zake hazifikii za Dar eg kule Tandale. Sehemu nyingi kuna makazi bora.
 
Unauliza maswali kama mtoto, uliza swali lieleweke ili nikujibu kwa ufasaha unaoutaka.
Bei za Huijui vizuri Dodoma kiuhalisia wala kijiolojia. Dodoma ni kukame lakini siyo jangwa. Inapata mvua japo si sawa na mikoa kama Tanga, Mbeya, Dar etc. Dodoma ina mabwawa (e.g. Mtera, Hombolo). Why? Kwasababu ina supply ya maji kupitia hizohizo mvua za msimu. Kule Bahi Dodoma wanalima mpaka mpunga kwasababu tope/maji yakutosha. Ukienda Kondoa Dodoma kuna mto pale Kondoa mjini kabisaa. Northern Kondoa wana maji everywhere kama mkoa wa Manyara wanaopakana nao. Water table ya Dodoma is very shallow. Hata zile sehemu very dry unachimba kidogo maji hayooo. Hayaishi leo wala kesho kwasababu Dodoma inapata Mvua kila mwaka japo ni kidogo ukilinganisha na mikoa mingine. Mimea na mazao yanayolimwa Dodoma ni ya kustahimili ukame - haitumii maji sana. Kuna maji mengi chini ya ardhi ya Dodoma ambayo hayatumiki. Kuhusu garama za maji Dodoma hazitofautiani sana na za mikoa yenye mvua nyingi.
 
Umesema vema. Makazi mangi ya Dodoma ni mapya na yapo katika mipango miji
 
Na ujanja wangu wote Area A sipajui, napajua Area C kule Lissu alipopigwa risasi ndio kunaitwa Site 1?
 
Hata Arusha kuna Oysterbay
Na Wakurugenzi nao wanakuwa kama hawakusoma! Wanaruhusuje majina yasiyoendana na mahali penyewe? Nilishangaa kusikia eti Kahama nako kuna Masaki na Oysetrbay! Hii kwa Wasukuma unaweza kuthibitisha kabisa ni ushamba wetu! Mawaziri wanaipita humu hebu wasikie huu ujumbe walifanyie kazi. Ni upumbavu!
 
Ni kweli, sehemu nyingi dodoma ukichimba maji yapo juu kabisa, ni siasa tu zinaleta shida hizi palipaswa kutokuwa na shida ya maji kabisa au ndio point yao ya kuombea kura kwenye kampeni?
 
Si kama Uzunguni? Tunaabudu vizuri pasipokujua tunapoteza identity yetu

Hata kuita hiyo sehemu ya Dar kama Oyster bay ni kuabudu lugha ya kikoloni kwanini wasingeita tu Bongoyo au jina lingine asilia?
 
Si kama Uzunguni? Tunaabudu vizuri pasipokujua tunapoteza identity yetu

Hata kuita hiyo sehemu ya Dar kama Oyster bay ni kuabudu lugha ya kikoloni kwanini wasingeita tu Bongoyo au jina lingine asilia?
Kwa Dar mkuu wako sahihi, imeitwa hivyo tangu enzi za ukoloni! Baada ya kuona kwenye hiyo Ghuba kuna makombe mengi!
 
Daah inanipa hasira hii kupishana na fursa, natamani sana kuwekeza kwenye real estate ila pesa bhana ndio kipengele.
Dodoma kweli ukiona juu kwa drone pamepangika vizuri sana, hasa hiyo mitaa ya washua yaani imechorwa na kupangwa kwa umahiri mkubwa.
Ukiwa Itega mji unauona kwa chini. Hakuna mpangilio wowote sijui ni kitongoji gani kile.
 
Haiwezi kuipiku Mwanza hata kwa dawa! Miaka 10nijayo Mwanza inaenda kuungana na Misungwi pamoja na Magu! Sasa hivi inaelekea kuungana na Kayenze! Magorofa sasa yanavyoporomoshwa usiombe!
Umefika Dodoma hivi karibuni? Wapi umefika?
Sasa ukiongelea miradi inayokua, Dodoma ina

1. Njedengwa Investment Centre - hapa Bunge la Afrika linajenga Hotel ya Nyota tano, International conference centre and high end shopping malls ipo under construction. Pia, NSSSF wanajenga Hotel ya Nyota tano, zitakuwa mbili eneo moja for diplomats, UN high profile visitors and delegates. Mbali na haya kuna Ghorofa za ofisi za Umma kama TBS, BIMA house, Chuo cha IFM, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, UCSAF bado watu binafsi wana project za kutosha etc by 20230 Njedengwa itakuwa smart city in East Africa.


2. Magufuli City- hapa ndio usiseme hii ndio posta mpya ya dodoma, majengo yote ya wizara ya kisasa yapo hapa, kunajengwa balozi, UN office, High end hotels , international conference centre, shopping malls and apartments.

3. NICC link- hapa ndio Makao Makuu ya Mahakama Tanzania- Judiciary Square, Mahakama kubwa kwa jengo Afrika baada ya Misri. Huu mji una maofsi ya Umma kama BOT, Treasury, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Utumishi wa Umma, NHIF, Jakaya Kikwete Convention Centre, Mhandisi House, Usalama wa Taifa, Kambarage Tower, Osha HQ na nyingine nyingi. Well organised township.

4. Msalato International airport - hiki ndio kichocheo kikubwa cha kuipa dodoma hadhi ya kimataifa, Septemberi inakadiriwa kukamilika( Mwanza haina International airport)

5. SGR - hii ndio imeleta flexibility ya Dar. Moro Dodoma, imekuza muingiliano mkubwa na kuboost biashara

6. Inland Dry Port - pale Nala kupitia SGR mizigo ya bandarini ina park hapo kusafirisha kwenda nchi jirani na sehemu za ndani ya nchi. Ni mradi mkubwa huu.

7. Mihimili mitatu ipo fully functioning in Dodoma, hili halihitaji maelezo unajua effect yako.

8. Viwanda vinavyojengwa- kuna kiwanda cha Steel kinajengwa ni kikubwa East Africa kitakuwa game changer kwa dodoma, Don mwingine anajenga kiwanda cha ku assemble auto parts kikubwa East Africa.

9. Uwanja wa Mpira- pale nzuguni ukikamilika utakuwa uwanja mkubwa na wakisasa baada ya Dar.

Mwanza hatoboi, just a matter of time mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…