Dodoma: Pamoja na katazo la Kiongozi wao, Wabunge kadhaa wa CHADEMA wakiwemo Silinde na Lijualikali wahudhuria bungeni

Dodoma: Pamoja na katazo la Kiongozi wao, Wabunge kadhaa wa CHADEMA wakiwemo Silinde na Lijualikali wahudhuria bungeni

Kwa chadema mbunge anamuwakilisha mbowe sio mwanainchi

Ujinga mwingine bana, rais kakimbia ofisi zake 2 yuko nyumbani kwake, kisha anatoka anaongea kwa jazba kuwa wabunge wasioingia bungeni wasilipwe.
 
Kwa hali ya kisiasa sasa hivi nchini, mwanasiasa asiyejua kuwa kuwa ndani ya CCM sio salama kuliko nje ya CCM basi ana akili mgando.
Hivi hawaoni kuwa hata jiwe amekata tamaa kabisa? Hana imani na Ku survive shinikizo LA ndani lakini hata LA nje pia hayuko salama maana dunia ilishachoka watu madikteta.
Wapo wale tuu ambayo wamejizatiti na wana uwezo wa kijeshi kiasi kuwa kumuondoa inaweza kusababisha maisha ya wengi kupotea mfano DPRK na Iran
Sijui hata umeandika vitu gani
 
Kwenye mambo yakuzaliti chama ndipo nawaunga mkono ccm hawatakagi ujinga mfano Membe alikuwa anajifanya mjuaji leo anakimbia Media Chadema wafukuze watu wa namna hii
Mjinga kama Silinde katoka Shule kafikia Chadema imempa maisha halafu analeta ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Kilichompa hayo maisha ni jitihada zake mkuu. Kama humfahamu unakula mee. Harakati hakuanzia chadema.

Ni kwamba tu 2010 chadema ndicho kilikuwa tumaini pekee la wananchi. Sasa ikiwa kimekuwa chama cha kipuuzi afanyaje? Aendelee kuzidumisha fikra za mwenyekiti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya Wabunge wa Upinzani hasa CHADEMA kugomea kuingia Bungeni ili kupitisha bajeti ya wananchi waliowachagua hali imekua tofauti kwa wabunge hao wanaonekana wameiva Kifikra na waliojawa huruma kwa wananchi wao waliowachagua mwaka 2015.
Mie namkubali Magu tu, amefuata ushauri wa WHO to the letter. Amefanya Lockdown ya uhakika nyumbani kwake, kama walivyofanya mabeberu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga mwingine bana, rais kakimbia ofisi zake 2 yuko nyumbani kwake, kisha anatoka anaongea kwa jazba kuwa wabunge wasioingia bungeni wasilipwe.
Huu ndio ujinga na kutokujua raisi ni mkuu wa nchi anafanya shughuli yake popote kikatiba wala hakuna zuio la kikatiba linalomzuia mh raisi na amiri jeshi mkuu, tatizo mnajaribu kumfananisha DJ na mamlaka ya uraisi ni vitu viwili tofauti DJ ndio afanye shughuli zake mtaa wa ufipa au jimboni kwake tu ndio sehemu alizonazo mamlaka chadema huwa hamjielewi kabisa
 
..hiyo ndiyo demokrasia.

..vyama vya siasa vinatakiwa vi-accomodate viongozi na wanachama wenye mitizamo tofauti.
Sasa hicho chama au saccos. Chama makini lazima waongee ndani then wakitoka nje wanakuwa lao moja siyo mnatoka nje kila mtu na lake.
 
1588666025490.png

Wabunge wanane wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walikaidi maagizo ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuwataka kutohudhuria vikao vya bunge na kujitenga kwa siku 14.

Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Joseph Selasini (Rombo), Peter Lijualikali (Kilombero), David Silinde (Momba), Antony Komu (Moshi Vijijini), Susan Masele (Viti Maalum), Jaffary Michael (Moshi Mjini), Latifa Chande na Subrina Sungura (Viti Maalum).

Wabunge hao walihudhuria mkutano wa 18 wa kikao cha 21 cha Bunge la 11, kilichojadili na kupitisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na walikuwa katika ukumbi wa Msekwa na ukumbi mkuu wa Bunge. Mbunge Selasini wiki iliyopita alilalamika bungeni kwa kuondolewa kwenye kundi songezi la wabunge wa Chadema na kushindwa kuchangia mjadala wowote tangu kuanza kwa bunge, hadi alipopitia kwa Spika, Job Ndugai.

Aidha, siku iliyofuata Selasini alitangaza kuendelea kuwa mbunge, lakini hana mpango wa kugombea kupitia Chadema, bali NCCR- Mageuzi, Oktoba mwaka huu. Februari mwaka huu, Komu alitangaza kuwa atagombea ubunge jimbo hilo, na kwamba wakati ukifika atagombea kupitia NCCR- Mageuzi.
 
View attachment 1440292

na bado
 
Kuna mtu mmoja alijisemea Bungeni kuwa, Sisi ndio tulikuwa wapinzani haswa tena kipindi chenyewe kilikuwa ni cha Baba wa Taifa angali akiwa hai, Tulimtingisha Mwalimu mpaka akaingia kwenye kumkampenia Mkapa, sembuse nyinyi wapingaji na wapigania njaa? Hii ni kweli kumbe!
 
Sasa hicho chama au saccos. Chama makini lazima waongee ndani then wakitoka nje wanakuwa lao moja siyo mnatoka nje kila mtu na lake.

..kweli.

..lakini haiwezekani kuwepo na hoja halafu iungwe mkono 100%.

..vijana mkienda na attitude kwamba msimamo wa chama ni lazima uungwe mkono 100% mtakuja kuleta shida nchini.
 
Tatizo sio siasa bali sisi wenyewe kwenye hii nchi.siasa iko dunia nzima ila sidhani kama nauko kwenye nchi zinazojielewa wanaweza kua na ujinga kama wetu.
Dah yani nikikumbuka Lijuakali na sakata lake lote lile,Lijuakali na kumpambania Dogo-Janja wa Arumeru,halafu ghafla picha inageuka,siasa bhana kama vile kivuli cha gizani.
 
Back
Top Bottom