Dodoma: Pamoja na katazo la Kiongozi wao, Wabunge kadhaa wa CHADEMA wakiwemo Silinde na Lijualikali wahudhuria bungeni

Dodoma: Pamoja na katazo la Kiongozi wao, Wabunge kadhaa wa CHADEMA wakiwemo Silinde na Lijualikali wahudhuria bungeni

Kwenye mambo yakuzaliti chama ndipo nawaunga mkono ccm hawatakagi ujinga mfano Membe alikuwa anajifanya mjuaji leo anakimbia Media Chadema wafukuze watu wa namna hii
Mjinga kama Silinde katoka Shule kafikia Chadema imempa maisha halafu analeta ujinga
Halafu utasikia wanachadema wanamuita Zitto msaliti, hivi hamjui wasaliti wa kweli miongoni mwenu ni akina nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe anachukuliwa poa sana
2007280_17_Tanzanian_opposition_legislators_face_various_politically_motivated_offenses_.jpg
 
Kwa hali ya kisiasa sasa hivi nchini, mwanasiasa asiyejua kuwa kuwa ndani ya CCM sio salama kuliko nje ya CCM basi ana akili mgando.

Hivi hawaoni kuwa hata jiwe amekata tamaa kabisa? Hana imani na Ku survive shinikizo LA ndani lakini hata LA nje pia hayuko salama maana dunia ilishachoka watu madikteta...
Ungejibu hoja kamanda acha kuweweseka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Elius Ndabila.
0768239284

Wiki iliyopita Mh Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa KUB aliitangazia dunia kuwa chama chake wamekubaliana wabunge wao wasiingie bungeni kwa siku 14 kwa kile kilichoelezwa kujikarantini kutokana na ugonjwa wa corona.

Kitendo cha Mh Mbowe kuitangazai dunia hivyo kiliibua maneno mengi akiwepo Mh Rais aliyesema amemuagiza Spika asiwalipe posho. Wadau wengine walisema kukimbia vita ni uoga na ushamba.

Jana kuonyesha kuwa Demokrasia inakua ndani ya CHADEMA na WABUNGE kuchoshwa kuburuzwa na Mh Mbowe inasemekana wabunge zaidi ya kumi walihudhuria kikao cha bunge. Kitendo hicho kinaonyesha maamuzi ya Mh Mbowe kuitangazia dunia kuwa chama wamekubaliana kukaa siku 14 hayakuwa makubaliano ya wabunge wa chama bali ya kwake mwenyewe.

Tafsiri ya hili ni kuwa wabunge hawa wanaitangazia dunia kwa kumjibu Mh Mbowe kuwa hawakubaliani na maagizo yake ambayo anaamua pekee yake. Kitendo cha hao wabunge kumpuuza mwenyekiti wao ni kitendo cha kishujaa na kinachojenga demokrasia ya kukataa kuendeshwa endeshwa.

Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanasema inawezekana tukashuhudia wabunge wengine kuanzia leo wakiendelea kulipuuza agizo la Mh MBOWE na kuendelea na vikao vya bunge jijini Dodoma. Wachambuzi wanadai wabunge walioenda jana wakiongozwa na wabunge wa jimbo Ernest Silinde wa Momba na Mh Lijualikali wa Kilombero na wabunge wengine wa Viti maalum ni dira tu ya mashujaa walioamua kutangulia lakini wengi watafuata.

Hitimisho lake ni kuwa kitendo hicho kinaonyesha Wabunge wanakubaliana na hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya kupambana na janga la Corona na si vinginevyo. Lakini pia hili ni fundisho kwa Mh Mbowe kuwa sasa wabunge wake wameanza kuwa matured ndiyo maana wameamua kumpuuza. Na asipoongalia anaweza kuiondoa CHADEMA kutoka chama kikuu cha upinzani na kuingia kwenye historia ya vyama vingine vilivyo wahi kuibuka na kufifia kama mshumaa.

*Msingi mkubwa wa demokrasia si tu kuchagua lakini pia ni kukubaliana au kuto kukubaliana*. Wabunge wa CDM walioingia bungeni jana wametimiza nguzo ya Kuto kukubaliana na maagizo ya Mh Mbowe ambayo ni haki yao kikatiba.

#Tanzaniakwanza.
 
Katika kila kinachoonekana mwisho wa ufalme wa enzi umefika, wabunge 11 wa Chadema wamepinga waziwazi agizo la Mbowe la kutoingia bungeni mpaka wapimwe Corona.

Tulipoonya miaka 5 iliyopita kwamba laana ya Dk Slaa ni kali mno na kwamba itaisambaratisha kabisa Chadema tulitukanwa sana na bavicha waliomwagwa mitandaoni kutetea udikteta wa Mbowe.Kabla hata miaka 5 haijaisha, madiwani mamia na wabunge makumi wameikimbia Chadema! Hata hao waliobaki hawasikilizi tena maagizo ya mwenyekiti wao, yani wako tayari kufuata maagizo ya mwenyekiti wa ccm rais Magufuli kuliko kufuata Mbowe anataka nini.
IMG_20200505_081635.jpeg
IMG_20200505_081815.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mbowe anapwaya sana kwenye nafasi ya uenyekiti,kama watu unaowaongoza hawakutii sasa unategemea nini ,awe muungwana ajiuzuru kwenye nafasi hiyo apishe damu changa

Katibu wa chama chake naye kwa sasa hawaelewani,nasikia juzi kampigia simu mara tano lakini katibu hakupoke na wala hajamtafuta kujua simu hiyo ilihusu nini,na kuna taarifa zinadai huenda katibu akabwaga manyanga hivi karibuni,hiki chama kimekosa mwelekeo kabisa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom