beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwaapisha Viongozi Wateule watatu walioteuliwa Oktoba 08, 2021.
Jaji Mustapha Siyani ameteuliwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Omar Othman Makungu ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Pia, Sophia Edward Mjema ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
UPDATES:
PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS
Ushirikiano baina ya Mihimili
Nimekuja kukumbana na kesi kama mbili hivi. Mahakama inaamua lakini hukumu haitekelezwi… Nataka niwaombe sana Mh. Mkuu wa Mkoa, na kupitia mhadhara huu, wakuu wa mikoa wote, mlaiangalie hili. Ninyi ndiyo mnasimamia vyombo vya dola ka niaba ya rais katika mikoa mliyopangiwa. Lakini pia waheshimiwa Mahakimu waliangalie hili.
Mh. Jaji Mkuu nadhani nadhani ni vizuri mkawa na namna ya kufuatilia jinsi ambavyo hukumu ambazo zimetolewa na mahaka kama kweli zimetekelezwa ama hapana.
Nawapongeza sana. Nendeni mkachape kazi. Rais Samia amewaamini na ndiyo matarajio ya Watanzania.
SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Tunatarajia uongozi uliotukuka
Kwa majaji, langu mimi ni kutegemea kwamba mtakwenda kutenda haki kama mnavyotakiwa.
Kwa Jaji Mkuu Kiongozi, juzi hapa wakati tulipokuwa na shughuli ya kufungua vituo jumuishi vya kutoa haki, kulikuwa na mambo mengi ambayo niliyaagiza, ikiwemo yale ya kuimarisha shughuli za mahakama kwenda kwa mtandao. Naomba ukalisimamie vizuri, najua kuna budget deficit na nikaomba sekta ya sheria na Waziri wa Fedha, probably na wewe mwenyewe, muone mnachoweza kufanya, na mkishindwa basi mje tuone tunaweza kusukuma vipi. Lakini kwa ukubwa wa nchi yetu na mambo yanavyokwenda, lazima twende na mitandao.
Tunatarajia utendaji uliotukuka.
Wakuu wa Mikoa msiwe miungu watu
Kwa ujumla niseme kuwa uongozi ni dhamana… Sitegemei kumuona Mkuu wa Mkoa anaingia kwenye vitendo vya Rushwa. Sitegemei wala sitostahimili. Sitegemei Mkuu wa Mkoa mnakuwa miungu watu kule mlipo. Mpo kule kuwatumikia watu, si watu wawatumikie nyie.
Msifanye kazi kwa misingi ya ukabila
Lingine, Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo.
Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani. Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.
Tamisemi Wazri Mtanga, Katibu Mkuu ni Mtanga, nikaambiwa umetuletea Watanga watupu nikawaambia waacheni wafanye kazi. Wakikoroga nawatumbua, kama ni wa Tanga kama ni wa wapi.
Sipangi kwa makabila. Napanga kwa uwezo na ninayeona anaweza kufanya kazi na mimi.
Msiache kukusanya mapato
Kuletwa fedha TAMISEMI kusifanye halmashauri zika-relax kukusanya mapato. Huo ndiyo mtihani wa Wakurugenzi. Fedha zile zimeletwa kuleta msukumo. Najua mna uwezo mkubwa wa kukusanya mapato. Changamoto bado ni nyingi.