Dodoma: Rais Samia awaapishwa viongozi wateule leo Oktoba 11, 2021

Dodoma: Rais Samia awaapishwa viongozi wateule leo Oktoba 11, 2021

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwaapisha Viongozi Wateule watatu walioteuliwa Oktoba 08, 2021.

Jaji Mustapha Siyani ameteuliwa kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Omar Othman Makungu ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Pia, Sophia Edward Mjema ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.



UPDATES:

PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS

Ushirikiano baina ya Mihimili
Nimekuja kukumbana na kesi kama mbili hivi. Mahakama inaamua lakini hukumu haitekelezwi… Nataka niwaombe sana Mh. Mkuu wa Mkoa, na kupitia mhadhara huu, wakuu wa mikoa wote, mlaiangalie hili. Ninyi ndiyo mnasimamia vyombo vya dola ka niaba ya rais katika mikoa mliyopangiwa. Lakini pia waheshimiwa Mahakimu waliangalie hili.

Mh. Jaji Mkuu nadhani nadhani ni vizuri mkawa na namna ya kufuatilia jinsi ambavyo hukumu ambazo zimetolewa na mahaka kama kweli zimetekelezwa ama hapana.

Nawapongeza sana. Nendeni mkachape kazi. Rais Samia amewaamini na ndiyo matarajio ya Watanzania.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Tunatarajia uongozi uliotukuka
Kwa majaji, langu mimi ni kutegemea kwamba mtakwenda kutenda haki kama mnavyotakiwa.

Kwa Jaji Mkuu Kiongozi, juzi hapa wakati tulipokuwa na shughuli ya kufungua vituo jumuishi vya kutoa haki, kulikuwa na mambo mengi ambayo niliyaagiza, ikiwemo yale ya kuimarisha shughuli za mahakama kwenda kwa mtandao. Naomba ukalisimamie vizuri, najua kuna budget deficit na nikaomba sekta ya sheria na Waziri wa Fedha, probably na wewe mwenyewe, muone mnachoweza kufanya, na mkishindwa basi mje tuone tunaweza kusukuma vipi. Lakini kwa ukubwa wa nchi yetu na mambo yanavyokwenda, lazima twende na mitandao.

Tunatarajia utendaji uliotukuka.

Wakuu wa Mikoa msiwe miungu watu
Kwa ujumla niseme kuwa uongozi ni dhamana… Sitegemei kumuona Mkuu wa Mkoa anaingia kwenye vitendo vya Rushwa. Sitegemei wala sitostahimili. Sitegemei Mkuu wa Mkoa mnakuwa miungu watu kule mlipo. Mpo kule kuwatumikia watu, si watu wawatumikie nyie.

Msifanye kazi kwa misingi ya ukabila
Lingine, Samia Suluhu ninapotoka hatuna makabila. Kwetu kule Zanzibar tunajuana kwa maeneo.

Kwenye system ya makuzi – shule na siasa – tunamshukuru sana Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kwahiyo, tunapofanya kazi hapa, na mimi binafsi, ninafanya kazi bila kuangalia kabila fulani. Sasa watu wakifanya makosa, “nimewajibishwa kwakuwa ni kabila Fulani”. Sina kabila. Mimi hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakwambia ni Mzanzibari.

Tamisemi Wazri Mtanga, Katibu Mkuu ni Mtanga, nikaambiwa umetuletea Watanga watupu nikawaambia waacheni wafanye kazi. Wakikoroga nawatumbua, kama ni wa Tanga kama ni wa wapi.

Sipangi kwa makabila. Napanga kwa uwezo na ninayeona anaweza kufanya kazi na mimi.

Msiache kukusanya mapato
Kuletwa fedha TAMISEMI kusifanye halmashauri zika-relax kukusanya mapato. Huo ndiyo mtihani wa Wakurugenzi. Fedha zile zimeletwa kuleta msukumo. Najua mna uwezo mkubwa wa kukusanya mapato. Changamoto bado ni nyingi.

FBan_gwWQAUZqdJ.jpg


FBauk-iWUAAA3XE.jpg


FBaxhp9XoAMyZIa.jpg
 
Hierarchy of courts in Tanzania Mainland

Muundo wa Mahakama Tanzania Bara

The Magistrates Courts Act of 1963 strengthened the court system established in the colonial era. This system remained undisturbed until 1984 when the present court system was introduced through the Magistrates Court Act 1984. In 1977 when the Constitution of the URT came into force and in 1979 when the Court of Appeal of Tanzania was established there were significant developments in the legal system. These particular developments created the High Courts of Tanzania mainland, that of Zanzibar and the Court of Appeal, a union matter.

The Principal Judge (Jaji Kiongozi) is the Head of the High Court of Tanzania Mainland. The High Court was first established by Article 17 (1) of the Tanganyika Order-in-Council, 1920. The High Court now derives its establishment from Article 108 (1) of the 1977 Union Constitution as the High Court of the United Republic. Administratively, the High Court is headed by the Principal Judge (Jaji Kiongozi), a special assistant to the Chief Justice. The Judicature and Application of the Law Ordinance, No. 7 of 1920, established The High Court of Tanzania mainland. It was then adopted by the Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 under Article 107 of Chapter 5, Part I of the Constitution and it has unlimited original jurisdiction to entertain all types of cases and appeals, there from go to the Court of Appeal.

It is the court of first instance in cases of murder, treason and armed robbery and an appellate court in all cases from Districts and Magistrates’ courts. The High Court exercise original jurisdiction on matters of a constitutional nature and have powers to entertain election petitions. The High Court has specialized divisions like The Commercial, Land and Labour. The High Court also has Admiralty jurisdiction, to make orders and to hear and determine claims, proceedings and other matters as conferred by the Merchant Shipping Act, No.43 of 1967.

Source: Tovuti Kuu ya Serikali: Muundo wa Mahakama Tanzania Bara
 

MAHAKAMA YA RUFANI​

Courts \ Court of Appeal​


1.0 UTANGULIZI​

  • Mahakama ya Rufani ilianzishwa tarehe 15 Agosti, 1979 baada ya kufa kwa iliyokuwa Mahakama ya Afrika Mashariki. Mahakama hii imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 117(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
  • Mahakama ya Rufani ina mamlaka Tanzania bara na Zanzibar.
  • Kimsingi ndiyo Mahakama ya mwisho katika utoaji wa haki nchini.
  • Mahakama hii haina mamlaka ya awali (Original jurisdiction) isipokuwa ina mamlaka ya kusikiliza na kutoa maamuzi ya rufaa, maombi ya mapitio , marejeo na masahihisho.
  • Rufaa na maombi yanayowasilishwa Mahakama ya Rufani ni kutoka katika Mahakama Kuu Tanzania bara, Mahakama Kuu Zanzibar na kutoka kwenye mabaraza maalumu kama vile Baraza la Rufaa za Kodi.

2.0 DIRA​

Dira ya Mahakama ya Rufani ni ile ya Mahakama ya Tanzania: Haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mahakama ya Rufani inalenga kutoa huduma bora kwa ustadi na weledi wa hali ya juu.

3.0 UONGOZI KATIKA MAHAKAMA YA RUFANI​

 
JAJI KIONGOZI

4.0 UONGOZI KATIKA MAHAKAMA KUU


Shughuli za utendaji wa kila siku wa Mahakama Kuu na Mahakama za chini zinasimamiwa na Jaji Kiongozi. Katika kutekeleza majukumu yake anafanya kazi za kusimamia uendeshaji wa mashauri na za utawala. Madaraka ya Jaji Kiongozi ya usimamizi wa mashauri katika ngazi ya Mahakama Kuu Kanda na Divisheni yamekasimiwa kwa Majaji Wafawidhi . Na katika ngazi ya Mahakama za Hakimu Mkazi, Wilaya na Mwanzo madaraka hayo yamekasimiwa kwa Mahakimu Wafawidhi . Shughuli za utawala zinafanywa na Wasajili na Watendaji wa Mahakama.... Source : Court Mapping | App Management Portal
 
Kutoka maktaba :

MIAKA 100 YA MAHAKAMA KUU

Kwa mujibu wa Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt alisema kuwa sherehe za maadhimisho hayo zitaanza mwishoni mwa mwaka huu (2020) na kufikia kileleni mapema mwaka 2021.

“Mahakama Kuu ya Tanzania, ilianzishwa kisheria 1920 Tovuti Kuu ya Serikali: Muundo wa Mahakama Tanzania Bara na kuanza kufanya kazi rasmi Januari 03, 1921 ikiwa na masjala chache,” alieleza Mhe. Sarwatt.

Msajili huo alisema kuwa kupitia maadhimisho hayo, Mahakama itafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Aidha, Mhe. Sarwatt alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa ngazi hiyo ya Mahakama nchini kumekuwa na mafanikio kadhaa ikiwemo ongezeko la Masjala 22, Kanda 16 za Mahakama Kuu, Divisheni nne (4) pamoja na Kituo cha Usuluhishi.

Mbali na hilo, Msajili huyo aliongeza kuwa kumekuwa na mafanikio pia katika suala zima la usikilizaji/uondoshaji wa mashauri, ongezeko la majengo ya kisasa, Matumizi ya TEHAMA Mahakamani na kadhalika.

“Lengo la Mahakama Kuu ni kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi, hivyo mpango wa Mahakama ni kuwa na Mahakama Kuu katika kila mkoa,” alisisitiza Mhe. Sarwatt.

Mahakama ya Tanzania imegawanyika katika ngazi kuu tano ambazo ni Mahakama za Mwanzo, Mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi/Mkoa, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani.

Aidha, Mahakama Kuu ina Divisheni zake ambazo ni
  1. Mahakama Kuu- Divisheni ya Ardhi,
  2. Mahakama Kuu-Divisheni ya Biashara,
  3. Mahakama Kuu-Divisheni ya Kazi na
  4. Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi almaarufu kama Mahakama ya Mafisadi.
Source : MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 100 YA KUANZISHWA KWAKE
 
Pongezi nyingi kwa Jaji Kiongozi mpyaa, Jaji Mustafa Siyani.

Hakika anastahili, ni kijana bado ana nguvu.

jambo la msingi anapaswa aondoe uonevu ndani ya Mahakama yenyewe kwa kushirikiana na Prof. Elisante kisha haki itamalaki kwa wananchi wote.
 
Safi Sana Rais Samia, hafanyi Kazi kwa kuangalia kabila la mtu, anateua mtu kulingana na utendaji wake

Sio kipindi kile Cha mtani wangu mwendazake, Kama sio wa kanda hile hupati teuzi ya nafasi nyeti

Kwa hakika Sasa tumepata Rais mnyenyekevu na mwenye hofu ya Mungu ya dhati
 
Inaonekana kuna kundi la watu au aina ya watu fulani wanajiona kuwa wao ndio wana haki ya kuteuliwa ktk nafasi mbali mbali za kulitumikia Taifa hili kuliko watu wengine!

huu ni upuuzi ulio ota mizizi kwa miongo mingi.

Kila mtanzania mwenye sifa anayo haki sawa ya kuteuliwa ktk nafasi yoyote ile.

Hongera sana Rais Samia kwa kuliona hilo na Watanzania wote tuko nyuma yake.....na wale wote wanao dhani wao tu ndio wanayo haki ya kuteuliwa ktk nafasi za uongozi washindwe na wafia mbali kabisa.
 
Inaonekana kuna kundi la watu au aina ya watu fulani wanajiona kuwa wao ndio wana haki ya kuteuliwa ktk nafasi mbali mbali za kulitumikia Taifa hili kuliko watu wengine!

huu ni upuuzi ulio ota mizizi kwa miongo mingi.

Kila mtanzania mwenye sifa anayo haki sawa ya kuteuliwa ktk nafasi yoyote ile.

Hongera sana Rais Samia kwa kuliona hilo na Watanzania wote tuko nyuma yake.....na wale wote wanao dhani wao tu ndio wanayo haki ya kuteuliwa ktk nafasi za uongozi washindwe na wafia mbali kabisa.
Kuna Mambo anajishitukia Baada ya Kujaza Bakwata Watupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Mambo anajishitukia Baada ya Kujaza Bakwata Watupu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu acha kuleta udini, hao unao waita "Bakwata" ni wachache sana ukiangalia ktk kila idara za Serikali ukilinganisha na hao ambao sio "
"bakwata".
Mfano mzuri tu fanya utafiti ktk Muhimili wa Mahakama;
~Angalia Idadi ya Majaji wa Mahakama za Rufaa.
~Angalia Majaji wa Mahakama kuu pamoja na viongozi wake.
~Angalia wasajili wa Mahaka kote nchini.
n.k, hao unao waita "bakwata" ni wachache sana.
~Hata hivyo uwiano ni Jambo la msingi sana ktk kuimarisha umoja, uzalendo na mshikamano wa Taifa letu, kwa kuzingatia sifa.

Mama yuko vizuri sana kamwe asitetereke wala kuyumba.
Takwimu zipo na zipo wazi kabisa.

Nchi hii itajengwa na watanzania wote.
~Viongozi wengine wenye mamlaka za kuteua wanapaswa sana kuzingatia UWIANO katika kuteua waache tabia ya kujaza aina moja ya watu ktk utumishi wa umma.
Mungu Mbariki Rais wetu.
 
Mkuu acha kuleta udini,
hao unao waita "Bakwata" ni wachache sana ukiangalia ktk kila idara za Serikali ukilinganisha na hao ambao sio "
"bakwata".
Mfano mzuri tu fanya utafiti ktk Muhimili wa Mahakama;
~Angalia Idadi ya Majaji wa Mahakama za Rufaa.
~Angalia Majaji wa Mahakama kuu pamoja na viongozi wake.
~Angalia wasajili wa Mahaka kote nchini.
n.k, hao unao waita "bakwata" ni wachache sana.
~Hata hivyo uwiano ni Jambo la msingi sana ktk kuimarisha umoja, uzalendo na mshikamano wa Taifa letu, kwa kuzingatia sifa.

Mama yuko vizuri sana kamwe asitetereke wala kuyumba.
Takwimu zipo na zipo wazi kabisa.

Nchi hii itajengwa na watanzania wote.
~Viongozi wengine wenye mamlaka za kuteua wanapaswa sana kuzingatia UWIANO katika kuteua waache tabia ya kujaza aina moja ya watu ktk utumishi wa umma.
Mungu Mbariki Rais wetu.
Tena ningeomba sehemu inayojazwa kabila Serekalini ifiutwe kabisa hata tukienda Police au Mahakamani hakuna haja ya kuulizana kabila na Dini, tujuwe moja sisi ni Watanzania tu,hiyo inatosha sana!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hii kauli ya mama imeongea mengi sana

Kumbe wale vichaa wakitumbuliwa wanaona ni kwasababu ya kabila lao

Nawaambia hakuna watu wakabila kama hilo genge wanatakiwa watolewe wote tu

Haiwezekani nchi ya makabila 120 marehemu mmoja alijaza kikundi cha kijijini kwake serikalini na hawa ndo wanatupa shida sasa hivi

Bahati tu sikua kiongozi mkuu wa JMT hadi hicho kijiji ningekifutia hadhi kabisa kwa jinsi navyochukia ukabila

Kwahiyo kutumbuliwa kwasababu ya kuleta ujinga, wizi, ufisadi, makosa na ulegacy na ukabila wanaona wanaonewa?

#Masembo

#Matondo

FB_IMG_16339528928072076.jpg
 
Back
Top Bottom