Wewe ndio umesoma na kuona shule na jeshi tuu kwenye bandiko langu, kama Mimi nilivyoona Aya yako ya Mwisho.
Kwa hiyo ulitaka nicopy/paste yote ulioandika[emoji1][emoji1]. Aya yangu ya mwisho nimeandika " Wajibu wa raia ni kutii sheria pekee na si vinginevyo" Siwezi kumtii raisi anaeniambia niue bali nitatii sheria inayoniambia nisiue.
 
Si angesema hivyo SASA?.. yaani wewe jamaa inabidi UWE mshauri wake kwenye Mambo ya public affairs...umeiweka vizuri Sana kuliko maelezo
Mtaka ana taka maamuzi ya chini yafanyike na kuamukiwa huko chini, Kama Ni katanibau wilayani maana mdio wanaojijua mazingira yao na sio maamuzi yafanywe na Serikali kuu. Loud and Clear. Yuko sawa. Ndio maana tunataka katiba mp
 
Mama anaweza kumwita Tony akamchapa kwanini amemfedhehesha dada yake
 
Zamani tukisoma kujifunza haikua Darasani tuu .nakumbuka ata kurudi nyumbani saa nane unapumzika for an hour.. baadae unafanya shughuli za home(kujijenga for future independent life ) kama kufua na kupika au kusafisha nyumba na mazingira, and then saa 11 unaenda kucheza for an hour na by 18:00hrs unakua home kubond na ndugu au wazazi kama wapo... asubuhi ukienda shule unakua fresh na brain inakuwa tayari kupokea mafundisho mapya...Na zamani wazazi hawakuwa wanakupressurize ili UWE a As Student..kama uko average wanakuelewa na wanaanza kukusukia mipango na mbinu zitakazokutoa maishani...siku hizi wazazi wanadhani watoto wao wote ni geniuses...as a result tuna wasomi wengi ambao hawana KAZI na hawakujengwa kimbinu kupambana..SASA isije watu wanadhani kusoma Sana au Kwa muda mrefu ndio solution...la hasha...we use to say SOMA SANA CHEZA SANA.
Ye Mtaka anataka watoto wasome hadi saa ngapi?
 
Mchawi mkubwa we...
Kwa hiyo watu waache kuwa creative?
Hii ndiyo akili mbovu ya watanzania wengi iliyotufikisha hapa
 
Dingi mazingira yanabadilika
 
Mmmmm mkuu H uyu naye kachemka
 
Sijui kama atabaki salama. Nahisi kitaota nyasi soon akaungane Chalamila
Hata Mtaka anajua madhara ya kauli zake lakini jamaa huyo yuko vizuri upstairs sina shaka nae hata akitolewa leo iko siku ataibukia Bungeni.

Mtaka ni mtu flani anayependa kutumia akili zake sio za chama, aliweza kuishi zama za Magufuli bila shida bila kukomoa watu kama ilivyokuwa kwa wakuu wa mikoa wengine.

Jamaa ni smart i believe, hata akitolewa sawa ila ukweli ameusema nasisi tutajua ukweli wake ndo umemgharim
 
Mtaka yuko sahihi mazingira ya vijijini ni magumu lazima watengenezewe special program. Mimi mtoto wangu yuko la kwanza hizi English medium shuleni kwao wanatoka saa 11. Sembuse hawa wa madarasa ya mitihani kila mzazi ana wajibu wa kupambania ustawi wa mtoto wake. Kwa mazingira hayo unaona kabisa wazazi walimfuata hapo kutaka ufafanuzi baada ya kupokea maelekezo ndiyo maana kawambia wamskilize yeye.
 
Dingi mazingira yanabadilika
Exactly...siku hizi waweza ata kuchukua ujuzi na elimu Kwa Msaada wa Google...sio lazima kurundikana kwenye majengo hafifu mnayoyaita madarasa the all day...ukikaa kwenye box muda murefu akili inakua inactive... inabidi utoke nje ya box..
 
In Africa it's dangerous to be right when your master is wrong RC Mtaka kasimama na wananchi na katupa jiwe gizani huu ndo ukweli ambao wananchi wengi wanapiga kelele viongozi pelekeni watoto wenu shule za kata
Yeye wa kwake yupo shule za kata?
 
Nakataa, Mtaka huo usmart hana na hajawahi kuwa nao.
 
Exactly...siku hizi waweza ata kuchukua ujuzi na elimu Kwa Msaada wa Google...sio lazima kurundikana kwenye majengo hafifu mnayoyaita madarasa the all day...ukikaa kwenye box muda murefu akili inakua inactive... inabidi utoke nje ya box..
Okey
 
You are very wrong.
It should be the other way round, namely, Anthony Mtaka awe Waziri wa Elimu, na Prof. Joyce Ndalichako awe Mkuu wa Mkoa.
Watoto wote wa Viongozi Waandamizi Serikalini wanasoma private Schools mpaka saa 4 usiku.
Wanapata Division 1 kwenye matokeo yao.
Kwa nini watoto wa Walalahoi wasome mwisho saa 9 jioni?
Au kuna njama za kuwabagua watoto wa Kitanzania kutokana na uwezo wa pesa wa Wazazi?
Ndalichako apeleke Mswada Bungeni, wa kuwataka Watendaji Waandamizi wa Serikali kusomesha watoto wao Shule za Serikali.
Hili likitokea, Shule za Serikali zitapata huduma na heshima stahiki.
Hali ya Elimu Nchini, na Utendaji wa Wizara ya Elimu inakera sana.
Ninamuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka kwa asilimia mia moja.
 
Mr. Mtaka kachemka...

Si kwa sababu ya alichoongea kuwa hakina maana. Inawezekana ana nia njema lakini si katika namna alivyoi - present hiyo hoja yake na mahali na wakati...

1. Lazima akumbuke kuwa serikali ni moja na lazima ajue pia kuwa ktk serikali kuna kitu kinaitwa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility). Kama tamko la waziri mwenye dhamana ya elimu lilikuwa na kasoro, kwanini serikali kwa ujumla wasingelipitia, wakafanya marekebisho na kwa kupitia kwa waziri huyo huyo tena serikali ikaja kutoa tamko likawa ndiyo mwongozo kote nchini...?

Haileti picha nzuri kwa viongozi wa serikali moja kuanza kulumbana hadharani tena kwa kutumia lugha ngumu dhidi yao wenyewe kwenye mambo yanayowahusu wananchi na watendaji wengine wa chini ambao ndiyo tunatakiwa kutekeleza hayo...

Huku ni kuwachanganya hao wananchi na watendaji (wasimamizi wa elimu nk) wasijue wafuate la nani na kuacha la nani....

2. Hata hivyo, it's all understood that, the overall incharge wa sekta ya elimu Tanzania ktk mambo ya kisera ni Waziri wa Elimu ambaye kwa sasa ni Bi. Joyce Ndalichako na siyo Mr. Anthony Mtaka...

Waziri akitoa tamko la kisera ktk mambo ya elimu na wakati huohuo RC fulani akatoa kajitamko kuhusu jambo hilohilo la kielimu kwenye kijimkoa chake likipingana na la waziri, basi automatic la RC linakuwa batili...!!

3. Sijapenda huu mnyukano. Hii ni ishara kuwa kuna tatizo ndani ya serikali. Katibu mkuu kiongozi na waziri mkuu haraka sana warekebishe. Haiingii akilini RC wa kijimkoa fulani anaamka kivyake huko na kuja na utaratibu wake wa namna ya kupeleka jambo fulani la kisera kinyume na sheria na utaratibu tena kwa kutumia kauli na lugha zenye kila aina ya insubordination dhidi ya Waziri...!
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Nimeogopa huu ujasiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…