Kwa mtizamo wangu naona hata kama RC Mtaka alikuwa na nia nzuri ya anachokiwakilisha lakini njia aliyoitumia sio sahihi kabisa. Hata kama Mtaka anajiona bora kutokana na sifa anazopata toka akiwa RC Simiyu sidhani kama ndio iwe tiketi ya yeye kubwata kiasi kile halafu eti anamchambua waziri hadharani vile hata kama huyo waziri ana mapungufu kiasi gani. Wote ni wateule wa raisi sasa vipi yeye Mtaka amshushie heshima mwenzake mbele za watu kiasi kile. Tena badala ya kuishia kumpinga waziri kwa hoja tu na hoja yake ilikuwa na mashiko kiasi fulani yeye akahamia kwenye mambo binafsi sijui gari yenye bendera, kiyoyozi, mara International school, sijui kupeleka watoto kusoma Ulaya. Na mbaya zaidi kumchonganisha hadharani waziri na wanafunzi, walimu na wazazi.
Mtaka hakupaswa kutafuta sifa kwa kumdhalilisha mwenzake ambaye wanajenga nyumba moja. Alipaswa kuwasilisha mpango kazi wake ambao unapingana na sera wizarani kwa Ndalichako angepigwa dana dana angeenda nao kwa waziri mkuu moja kwa moja na waziri mkuu akishindwa angeenda nao kwa mamlaka ya uteuzi wake yaani raisi. Kwa mihemuko ile aliyoonyesha Mtaka kwa Ndalichako nadhani kuna jambo baya kati yao linaendelea inabidi mamlaka ya uteuzi wao iingilie kati ikiwezekana mmojawapo apigwe chini kama sio wote wawili. Siku zote ogopa sana mtu anayetaka aonekane yeye ni bora kwa kutumia njia ya kuwadhalilisha/kwashushia hadhi wenzake.
Kwa kifupi alichafonya Mtaka ni udhalilishaji kama udhalilishaji mwingine wowote. Aliposema mpuuzeni huyo waziri nisikilizeni mimi maana yake Mtaka alikuwa anamaanisha nini kwa huyo waziri ambaye anasema asisikilizwe?