Ngoja na wewe tukuone hapo kisarawe utafanya Nini!
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Wote ni wateuzi wa rais
 
Naopongeza ujasiri wa mkuu wa Mkoa huu. Mtaka hongera sio Waziri anakurupuka tu bila kuwashirikisha wakumbuke hilo ni la Serikali za mtaa. Na huo ndio ukweli wototo wao wapo Canada sisi wapo shule za kata.
 
Usimdanganye Mama Samia achague kati ya watoto wa masikini, na watoto wa Viongozi kama Waziri Ndalichako.
Unamtaka Rais Samia aamue kuwa watoto wa wakubwa wasome mpaka saa 4 usiku lakini watoto wa wanyonge wasizidishe kusoma zaidi ya saa 9 jioni.
Waziri Ndalichako na miongozo ya Wizara wamekosea.
Wajirekebishe mapema iwezekanavyo.
Hali hii inanikumbusha miaka ya Baba wa Taifa wakati Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Kanali Nsa Kaisi, alipokaidi maagizo wa wakubwa akajichimbia Vijijini na kuhamasisha uchimbaji wa mtaro wa maji ulioleta ukombozi mkubwa kwa Vijiji kadhaa.
Msimsumbue Rais Samia na mawazo yenu ya kupinga Elimu ya watoto wa Shule za Kata
 
Kwani kipi kaongea kubaya hapo tatizo ccm mnataka watoto wa wenzenu waendelee kuwa mbumbu angalia mikoa ya watu walio pita pita shule huwezi kuta Wana ushabiki wa kijinga kwa ccm na hicho hicho ndicho hamkitaki ninyi
Mikoa gani mkuu? Nchi hii kuna shule kweli? Au kukariri makaratasi?
 

Rais makini anapaswa kumtoa huyo Mtaka taka ndani ya masaa tu apishe kabisa, serikali imevuliwa nguo kwa kiasi hiki, no hapana kabisa
 
Utii hata kwa fyongo utii wa woga wewe hufai hata ukatibu kata huwezi kuhuji?
Una upepo mfu na infant wa kutupwa kabisa, think think. Poor Tanzania huna akili kabisa achana na ushabiki na mihemko
 
Miongozo ya Elimu?
Kwa Shule za Kata tu?
Mwambieni Waziri Ndalichako atekeleze hiyo miongozo kwenye Shule wanazosoma watoto wa Mawaziri, Wabunge, Wenyeviti wa Vyama vya Siasa, (Mbowe, Samia, Mbatia, Zitto, et al), uangalie moto utakavyomuwakia!
 

Hongera sana Mkuu barikiwa mno
 
Yule mama ni zero nasemaga mara nyingi,sijui anatumiaga nini kufikiri huyu bibi,mtaka yuko sahihi,Mh rais tuondolee huyu bibi
 
Mkuu wa mkoa wa Songea hoyeee!!
 
mtaka yuko sahihi 100 percent kabsa waziri wa elimu ni hovyo. kama Yule fedha huu ni usawa wa ukweli n.a. uwazi.
 
Mtaka tumemsifia sana sasa kalewa sifa! Anajiona very exceptional

..Nakubaliana na wewe kwamba RC Mtaka hakutakiwa kumshambulia Waziri Ndalichako waziwazi kana kwamba hawatumikii serikali moja.

..Mtaka angeweza kuwaambia waalimu na wanafunzi waendelee na kambi zao za mafunzo ya ziada, na yeye kama RC wao atakwenda kuzungumza na Waziri wa Elimu ili kuweka mambo sawa.

..Mambo ya international school, sijui gari yenye kiyoyozi, etc etc hayakupaswa kuzungumzwa na RC mwenye heshima zake kama Mh.Mtaka.
 
Kisiasa huyo Mkuu wa mkoa kakosea sana. Alichofanya ni utovu wa nidhamu kwa serikali na Chama Cha Mapinduzi. Sema huyo RC ana nguvu kubwa sana ya umma nyuma yake... kumtumbua kizembe inaweza leta mtikisiko. Waziri angetulia zake na kufanya mambo yanayomhusu. Hii kuingilia hadi watoto wasomeje ni upumbavu kwa hadhi ya waziri.... waziri adili na mambo ya madawati, mitaala, maslahi ya walimu na mambo mengine ngazi ya kitaifa. Kambi za wanafunzi ni jambo dogo mno. Tusubiri uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM (Rais wa JMT) katika hili.
 
Ni kweli kuna tatizo kidogo katika suala la elimu yetu, kutokana na kukosekana dira ya moja kwa moja ambayo kila waziri ataifuata kuendeleza pale alipoishia mwingine!
Hata hivyo pamoja na mapungufu ya waziri wetu wa elimu siungi mkono kitendo cha Mtaka kumtolea maneno aliyoyatoa kwani ni mbali ya kumdhalilisha pia amemkosea heshima kama kiongozi mwenye mamlaka zaidi yake! Wote ni wanaCCM kwanini wasiyaongee wawili wakamalizana? Angekuwa ni waziri wa CHADEMA ingekuwa sawa maana tumezoea kusikia wabunge wake wakizodolewa hadharani na hata kuitwa wezi lakini Mungu ni mwema anawavusha!
Hivyo busara itumike na ikibidi viongozi hao wakutanishwe!
 
Una upepo mfu na infant wa kutupwa kabisa, think think. Poor Tanzania huna akili kabisa achana na ushabiki na mihemko
Naona tunashabilikia udicteta type of rule. Wizara ingeconsult watu wa chini through their staffs in Councils and RC s office ili kupata uhalisia ulivyo chini. Sio kutoa tu amri bila kupata mambo yalivyo chini. Rc yeye na team yake walishajipanga kuondoa zero kwenye mkoa wao wewe unaleta amri ya kusitisha masomo saa tisa alasiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…