Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Ukiomuona nguchilo anatamba Na kubwata ujue yuko karibu Na shimo lake. Kunguru hana kibiongo kama ukiona kibiongo ameinama anaokota kitu.

Mtaka amejiamini nini kumbwekea waziri?
 
 
Ukiomuona nguchilo anatamba Na kubwata ujue yuko karibu Na shimo lake. Kunguru hana kibiongo kama ukiona kibiongo ameinama anaokota kitu.

Mtaka amejiamini nini kumbwekea waziri?
Ameshaomba samahani tayari. Itamkosti huko mbeleni aombe Mungu aendelee kupanda juu.
 
Mkuu, inaelekea una tatizo binafsi na waziri wa elimu. Kuna msemo wa kiingereza usemao - "All work and no play makes Jack a dull boy". Ulizia maana yake.
 
Ndalichako mara ngapi anatoa pesa ili aandikwe vizuri
 
Mkuu wa mkoa hana facts ni siasa tu watoto wanahitaji kupumzika bhana.Mbona Tabora girls na tabora boys zimeshika namba 3&4 kitaifa bila makambi.Aaacha kuja mikakati isiyo na takwimu za ukweli
Ila tabora girls na boys aina ya wanafunzi wanaoenda pale ni wazur shule ina walimu wazoefu, mazngira mazur na pia hata hao wanafunz wengi wanao uwezo makwao
 
Yeye wa kwake yupo shule za kata?
Haka kama, lakini japo kausema ukweli kule punda kihongwe yule anayejifanya haelewi maisha ya watanzania walio wengi.
Ndalichako ni jini binadamu.
 
Nakataa, Mtaka huo usmart hana na hajawahi kuwa nao.
Uko sahihi. Hayo ni mawazo yako. Tuliowengi tunaamini yuko smart.
Kwa serikali za Afrika, kiongozi wa ngazi yake ni vigumu sana kupinga kauli ya waziri hadharani. Ameonesha tofauti kubwa sana.
 
Wewe umesoma shule za kina Junior ndio maana tuulize sisi tuliosoma Kayumba tukusimulie ugumu wa hii elimu ya huku kwetu.
Mkuu mimi sipo huko.

Kwenye sheria za utumishi wa umma watumishi wanatakiwa kutoka ofisini saa ngapi?

Ulitaka waziri akiuke sheria hiyo?
 
Mr. Mtaka kachemka...

Si kwa sababu ya alichoongea kuwa hakina maana. Inawezekana ana nia njema lakini si katika namna alivyoi - present hiyo hoja yake na mahali na wakati...
Ndalichako naye ana makosa. Alipaswa kujifunza na kuifahamu vema jamii anayoiongoza pamoja na changamoto zake kabla ya kubwatuka kwa kuwa ni waziri.

Masomo ya muda wa ziada nchini hayajaanza leo, angejifunza ni kwanini hali hiyo ipo na inazidi kushika kasi kutoka masaa hadi kuwa makambi ya mwezi. Baada ya hapo angekuja na mwongozo badala ya kuja na tamko ambalo linatetea sera mbovu za elimu.

Mtaka kaongea ukweli mchungu unaofichwa na viongozi wengi wa wizara hii.

Walimu wametwishwa mzigo wa kufikia viwango vya ufaulu bila huruma. Mzigo ni mkubwa kuliko uwezo lakini lazima ubebwe. Ataubebaje huyu mwalimu? Katafuta mbinu ya kuubeba bado anawekewa vikwazo.

Profesa anashindwa kutafuta suluhisbo la tatizo anabaki kubweka bila uelekeo. Ndo maana Msukuma alisema uprofesa wao hauna tija kwa ustawi wa taifa letu.
 
Hilo agizo la Waziri wa Elimu lenye lengo la kufelisha kwa kuzuia watoto wasisome baada ya saa 9 lilitolewa kimya kimya au hadharani?
Tena amewadhalilisha wakuu wa mikoa na wilaya ambao wanapambana kupata matokeo mazuri kwenye maeneo yao kwani walishawashawishi wananchi kukubali kugharamia masomo ya ziada, alijua hilo na bado akathubutu kusema wamepoka mamlaka.

Acha tu ajibiwe kihuni kwa kuwa alitumia ubabe wa mamlaka badala ya hekima.
 
Yeye mkubwa aliwaheshimu wadogo?
Tusichokijua hapa ni kuwa kila RC /DC kwenye eneo lake amewekewa malengo ya kutimiza kwenye kila idara, nj pamoja na elimu.

Sasa mkuu wa mkoa kaweka mikakati yake, waziri anakuja kuwaambia wananchi kuwa hiyo mikakati si sahihi. Huyu mkuu wa mkoa au wilaya atafanikiwaje?

Vitabu kapewa vichache, walimu pungufu, majengo mabovu, madawati hakuna na hata walimu wachache waliopo wamekata tamaa ya kazi.

Waziri aje na suluhusho halisi badala ya kushikilia sheria na kanuni ambazo hazileti tija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…