Unajua hili suala la kambi nimekuwa nikijiuliza sana kwamba hivi huwa kinafanyika nini huko makambini!! Lakini ninachoona ni kama kile kinachoitwa kunenepesha ng'ombe siku mnada!!!
Lakini cha ajabu, inaelekea huu mtindo unasaidia sana wanafunzi kufaulu mitihani, lakini am sure, uchukue wanafunzi wote waliofaulu mtihani waliofanya november kisha uwape mtihani ule ule mwezi mmoja baadae, usishangae ukakuta nusu ya wale ambao mwanzoni walifaulu, hivi sasa wakafeli kwa sababu kama ulivyosema, inaonesha wazi kwamba wanasomea mitihani!
Miaka ya 90, pale Mgulani Primary School kulikuwa na teacher mmoja maarufu sana kama Mwalimu Imma!!! Pamoja na umaarufu wake kwenye ufundishaji wa tuisheni, lakini pia karibu na mitihani alikuwa na kitu kinachofanana na hizi kambi, na kweli, over 90% ya wanafunzi wake walikuwa "wanafaulu"!!
Cha ajabu, at least wale ninaowafahamu mimi, wengi wao walikuwa wanaishia Form IV kwa kile ninachodhani walienda sekondar sio kutokana na uelewa wao bali kutokana na ujanja ujanja wa kusomea mitihani, na matokeo yake, unaingia sekondari wakati hauna msingi imara wa elimu ya awali.