Dodoma: Serikali yakiri Watu kushangilia Kifo cha Ndugai, ila yasema itawaeleza vijana kwamba hilo si jambo zuri

Dodoma: Serikali yakiri Watu kushangilia Kifo cha Ndugai, ila yasema itawaeleza vijana kwamba hilo si jambo zuri

Wasipoteze muda.

Wakae chini wajiulize maswali mawili tu.

1. Hii kushangilia vifo imeanza lini?
2. Imetokana na nini?
Huwezi razimisha kumpenda mtu, na kudondoka kwa adui ni furaha kwako. Vitani ni ama zake ama zako. Kwa hiyo swala la kufurahia kifo cha adui si geni japo kuna unafiki wa kujenga huzuni huko kuna vicheko moyoni.
 
Hivi ndivyo alivyoeleza Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.

Zaidi huyu hapa

Swali letu ni hili, unadhani kwanini kifo cha Ndugai kimeshangiliwa badala ya kuwa Huzuni kama Marehemu wengine wanapofariki akiwemo Maalim Seif na Ally Kibao?
======================

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Saimon Mayeka, amekemea baadhi ya watu kushangilia kifo cha Spika mstaafu Job Ndugai kilichotokea jana Agosti 06, 2025.

Soma Pia: Wananchi wakutana kushangilia kifo cha Ndugai!

DC Saimon amesema baada ya msiba, atazungumza na vijana hao ili kuwarekebisha huku akiwaomba wazazi kukemea tabia hiyo.

Hao vijana wanatakiwa kupewa mtaji wa biashara kwa kusherehekea kifo cha Ndugai. Ndugai alkua spika wa hovyo kuwahi kutokea,, mtu katili kupitiliza. Bora amepumzika
 
Kwenye msiba wa Magufuli kuna watu walikamatwa kwa kushangilia.

Hao watu nafikiri kabla ya kuwakamata watu wajiulize huu utamaduni mpya wa kushangilia vifo umetokana na nini.

Jibu ni jepesi watu wanashangilia watu waliowafanyia ukatili kwa kutumia madaraka yao .

Mimi naungana na walioshangilia maana wametumia haki yao kikatiba kama ilivyo kwa waliosikitika , wasipangiwe cha kufanya .

Viongozi waliopo hai nao wajifunze huu ni msiba wa pili wa mkuu wa mhimili watu wanashangilia.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Saimon Mayeka, amekemea baadhi ya watu kushangilia kifo cha Spika mstaafu Job Ndugai kilichotokea jana Agosti 06, 2025.

DC Saimon amesema baada ya msiba, atazungumza na vijana hao ili kuwarekebisha huku akiwaomba wazazi kukemea tabia hiyo.


========================

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mayeka Saimon, ameeleza kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya vijana kuonekana wakishangilia baada ya taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Yustino Ndugai.

Akizungumza leo Agosti 7, 2025, nje ya nyumba ya marehemu Ndugai katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, DC Mayeka amesema baada ya shughuli za kumpumzisha marehemu kukamilika, watawafuata vijana waliohusika ili kuwaelewesha na kuonesha kuwa tabia hiyo ni kinyume na maadili ya kitanzania.

“Baada ya kumpumzisha ndugu yetu, tutakwenda kuongea na vijana wale kuonesha kwamba ule sio ustaarabu wa Kitanzania na ni utamaduni ambao hatujawahi kuuona Tanzania,” amesema DC Mayeka.

Ameongeza kuwa picha mjongeo zilizosambaa mtandaoni zikionesha baadhi ya vijana wakishangilia kifo hicho zimemshtua, akibainisha kuwa si jambo la kawaida kwa jamii ya Kitanzania.

“Hiki kitendo cha baadhi ya wananchi kushangilia ni kiehemu kidogo sana cha kijiji ambacho baadhi ya vijana ndo wamejitokeza kushangilia. Na kwa kweli ni kitu ambacho kimetushangaza. Kwa hali ya kawaida, mila za Kitanzania, hili jambo linamshangaza kila mmoja kwamba imewezekanaje mtu anashangilia kifo,” alisema.

Amesema ni kweli mtu anaweza kuwa na wapinzani au maadui hasa akiwa mwanasiasa, lakini hakutarajia kuona mtu akishangilia kifo cha mwingine.
Wanavyoteka raia na kuwaua ni utamaduni waliouanzisha.

Kushangilia mtu mwovu anapofariki ni haueni kwa watendwa.

Mungu aendelee kufanya wepesi kwa Watanzania
 
Kila mtu ako na nerve system na ubongo wa tofauti. Sisi wengine raha yetu ni misiba ya wazito maana hapo tunaamin msosi na unyaji upo kama week nzima.
Huu ukiisha afe na mwingine mzito mzito.
 
Rubbish!. Kifo cha Mzee Kibao watu walisikitishwa na kiwango cha ukatili uliofanywa kabla ya kuuawa, matokeo yake yalikuwa nini? Mkuu wa wilaya ya Kongwa hafahamu kuwa "Comforter" wa taifa hili si alishangazwa na kuguswa kwa kifo cha mzee Kibao kwa sababu " Kifo ni kifo tu"? 😳
Hao vijana Mkuu wa wilaya anaenda kuwashauri kitu gani hasa wakati wao wanashangilia tu kifo cha mbunge wao? 🤔
 
Kwenye msiba wa Magufuli kuna watu walikamatwa kwa kushangilia.

Hao watu nafikiri kabla ya kuwakamata watu wajiulize huu utamaduni mpya wa kushangilia vifo umetokana na nini.

Jibu ni jepesi watu wanashangilia watu waliowafanyia ukatili kwa kutumia madaraka yao .

Mimi naungana na walioshangilia maana wametumia haki yao kikatiba kama ilivyo kwa waliosikitika , wasipangiwe cha kufanya .

Viongozi waliopo hai nao wajifunze huu ni msiba wa pili wa mkuu wa mhimili watu wanashangilia.
Mjini Mbeya baada ya Taarifa ya kifo cha Jiwe Mbuzi kadhaa walichinjwa na kupikwa supu pale Mwanjelwa, Polisi wakaja eneo la Tukio wakakuta wananchi wanajichana, wakauliza kwanini mnasherekea? Wananchi wakajibu hatusherehekei ila Tunakula
 
Kwenye msiba wa Magufuli kuna watu walikamatwa kwa kushangilia.

Hao watu nafikiri kabla ya kuwakamata watu wajiulize huu utamaduni mpya wa kushangilia vifo umetokana na nini.

Jibu ni jepesi watu wanashangilia watu waliowafanyia ukatili kwa kutumia madaraka yao .

Mimi naungana na walioshangilia maana wametumia haki yao kikatiba kama ilivyo kwa waliosikitika , wasipangiwe cha kufanya .

Viongozi waliopo hai nao wajifunze huu ni msiba wa pili wa mkuu wa mhimili watu wanashangilia.
Utasikia akina Tulia wanasema "Haunipunguzii chochote" na madam niko ndani ya jeneza.
 
Serikali ya CCM haijafanya lolote juu ya vitendo vya utekaji na uuaji hapa nchini wala viongozi wake kukemea jambo hilo kiasi ambacho imefikia hatua kila kiongozi wa ccm anapofariki watu badla ya kuuzunika wanashangilia
Serikali ya mama samia ijitafakari haikubariki na wananchi na isidanganywe na machawa waliojaa ccm ambao shida yao kubwa ni njaa
 
Kwenye msiba wa Magufuli kuna watu walikamatwa kwa kushangilia.

Hao watu nafikiri kabla ya kuwakamata watu wajiulize huu utamaduni mpya wa kushangilia vifo umetokana na nini.

Jibu ni jepesi watu wanashangilia watu waliowafanyia ukatili kwa kutumia madaraka yao .

Mimi naungana na walioshangilia maana wametumia haki yao kikatiba kama ilivyo kwa waliosikitika , wasipangiwe cha kufanya .

Viongozi waliopo hai nao wajifunze huu ni msiba wa pili wa mkuu wa mhimili watu wanashangilia.
Naam tena haki yao ya msingi kabisa
Haki ya kujieleza
 
Back
Top Bottom