DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Wakuu,

Inadaiwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!

9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow
Ni muujiza tu ndio unaweza kumponya Lissu, ila kwa jinsi risasi zilivyomiminwa it is impossible for him to recover
sasa wale walionitukana na kuniambia navuta bangi wanajihisije? we should be polite when we receive any strange news
 
Tumeshindwa sana kama tumefikia hatua hii. Kwa kila anayelitakia mema taifa letu, anajua umhimu wa Lissu. Pamoja na kuikaba serikali, alihakikisha anawataka wawe makini sana
 
Kwa Area D ilivyo huwezi kuniambia watu wasiojulikana, hii hainiingii akilini hata kidogo.. Hili swala sio la kushabikia hata kidogo, kuna shida mahali, kama mtu anaweza kupigwa risasi mchana ktk eneo kama la Area D, basi usalama wetu ni mdogo sana
 
Ni wazi kabisa mkuu, na nafikiri unajua lawama zinaenda kwa nani hadi wakati huu!

Tuweke tofauti zetu za kisiasa pembeni, tumeikuta nchi ikiwa na amani na tuiache nchi ikiwa na amani!

Hakuna tunachoweza kufanya bila amani!
Ila jambo moja tufahamu. Unapokuwa na maadui wengi unaweza kudhuriwa na yeyote ila lawama akatupiwa uliyedhani ndiye adui wako
 
Watz wote ni pamoja na tofauti zetu za kisiasa. Kwanini lakini mnamfanyie mti mbichi, mtetezi wa kweli wa wanyonge na mzaleondo wa kweli. Kama kweli mnaweza kum shot mchana kweupe mtu kama TL basi Tz siyo mahala salama tena kwa binadamu kuishi. Mungu msaidie ndugu huyu apone haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unataka kumuua lissu ili iweje ana ndugu,familia,jamaa,marafiki wanaomtegemea,kwann tusibishane kwa hoja haya mambo ya kuuana yashapitwa na wakati bna tubadilike.
\


Ahhhh!. My country, my country, my mamaland!.

Wewe unalazimisha watu watumie hoja ambazo hawana? Kuna matumizi ya hoja sasa hivi? Hiki ni kipindi cha mabavu tu!
 
Lissu alikua mwanaume pekee aliyeweza ongea Tanzania nzima
Wakaona leo watudanganye na ripoti yao ya uogo wakijua Lissu ataikosoa wakaona wamtoe kabisa

Mungu yupo Lissu hafi
 
".....ni bora mtu uvunje sharia. ...." -Nanihino
 
Back
Top Bottom