DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Hivi huwa namwona kila wakati anaombewa. Ina maana haya ayatendayo ndio majibu ya kuombewa? Na hao wanaomwombea humwombea kwa Mungu yupi? Siamini kama ni huyu Mungu anayetuhimiza tumpende jirani kama tunavyojipenda wenyewe na pia Mungu nimjuaye anasema mtendee mwenzako vile unavyopenda kutendewa.
Ni mungu huyohuyo anayetutaka tutii mamlaka iliyowekwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa mungu.
 
Baada ya kuona amepewa mwaliko wa kwenda Marekani mkaona akifanikiwa kufika huko atawafunua mchana kweupe na mkaona ni vema zaidi mumnyamazishe kabla ya kufika huko....kwa bahati mbaya sana mission imebuma na ndio mnazidi kumtengenezea njia na nyie kujitengenezea narrow roads......Get yourself prepared coz am sure when he's going to wake up...you will get hard time to block the fire out of him
 
Difficult to magine!!

Mungu wetu mwenye uweza wote tunakuomba yalinde maisha ya mtumishi wako ambaye watumishi wa shetani wanataka kutoa roho yake.

Waangamize wauaji na aliyewatuma kwa mkono wako mkuu na wenye mamlaka yote ili wakajue kuna mkuu kuliko wote, ambaye ni wewe Mungu wetu wa haki na uponyaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inafika kipindi nauchukia huu utawala kuliko kitu chochote kile. kuna siku Mungu mwenyewe atashuka kuiokoa hii nchi. nafikiri mkapa, mwinyi na kikwete wanatakiwa kuingilia kati kuiongoza hii nchi kwasababu sijui hata inakoelekea. kweli maisha ya aina hii ndo mtu afikirie watu tutakuwa wazalendo? watu wanaharibu nchi, wanaharibu umoja wa kitaifa, wajinga kabisa.
Kwani mhusika unamjua?

......
 
Wakuu,

Inadaiwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!


56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

MORE UPDATES

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake



Kwa nini huyo jamaa hakulenga vizuri?
 
Back
Top Bottom