DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

So suka angekanyaga mafuta kwenda wapi kwa mfano?
Arudi rivas to Bungeni?Akanyage mafuta kwenda home au aanza kuzunguka nao wakora?

May Allah bless Me and You
Umesoma nilichoandika au umekimbilia kujibu tu. Dereva amegundua anafuatiliwa akaamua kwenda nyumbani. Wewe unafuatiliwa nyuma na usiowajua utaenda nyumbani? Ukiingia ndani ndio dead end hio huna cha kujitetea. Kuna sehemu nyingi za kwenda zaidi ya nyumbani tena unaendesha one of the very powerful cars on the market.
 
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_FB_IMG_1498446553489.jpeg
 
Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka chumba cha upasuaji akiwa na fahamu na sasa anapelekwa Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.
======
Taarifa zote za uhakika tutakuwa tunazitoa kila baada ya muda mfupi...
Picha HELKOPITA iliyombeba Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ikiwa angani kuelekea Nairobi
View attachment 583481
Thames Valley ni Reading, Birkshire inakwenda mpaka London, England, huo ni mto.... Hiyo Chopa imefikaje tz in at max 4 hrs... [HASHTAG]#ihatefakenews[/HASHTAG]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhimbili ni rahisi kummaliza maana motive yao asiende marekani kule alikoalikwa. But as far as God is concerned He will protect him because as from now the angels are surrounding him

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo alipopatiwa first aid hospitali ya rufaa Dodoma walishindwa kummalizia hapo na hawakujua kama angejeruhiwa first step angepelekwa hapo?
 
Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

MORE UPDATES

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

View attachment 583477

Kifo hakikimbiwi ila kwa wasiokuwa na imani. Maadam kila kiumbe kiko mbioni kufa na anaekufa sio atakaekufa bali ambae hajafa basi wanaoua wengine wanajiua wenyewe kwa mikono yao.
 
Umesoma nilichoandika au umekimbilia kujibu tu. Dereva amegundua anafuatiliwa akaamua kwenda nyumbani. Wewe unafuatiliwa nyuma na usiowajua utaenda nyumbani? Ukiingia ndani ndio dead end hio huna cha kujitetea. Kuna sehemu nyingi za kwenda zaidi ya nyumbani tena unaendesha one of the very powerful cars on the market.
Lakini mkuu kwa mujibu wa Lisu on Agost 18 alisema anafatiliwa na alisema Sirro na Mkuu wa TISS wawaambie hao watu waachane nae wafanye yenye maana.Nadhan video ipo hapa.
Sasa kwa leo (kwa mtazamo wangu) hawakuwa na shaka maana Lissu alishasema anafatiliwa na alijua ni same to siku za nyuma.


May Allah bless Me and You
 
Wamuondoe kabisa hapa bongo na hata wale watu watakaojaribu kutaka kumuona au kusafiri nae waangaliwe sana....
Awekewe ulinzi wa hali ya juu na makamanda....
Lakini mwenyekiti wake anaweza husika maana jamaa alikua anaunyemelea *UENYEKITI* kwa nguvu zote,unakumbuka yule alifariki kwa ajali ya gari miaka ile naye alikua anautaka *UENYEKITI* na uenyekiti ukachukua maisha yake?

ploudly ngosha [emoji243][emoji243][emoji243]
 
Back
Top Bottom