Huyu mtu aliyetenda unyama huu amelifedhehesha taifa letu na kulipaka doa jeusi la milele. Lisu kama Rais wa TLS anaingia katika fikra na mawazo ya wanasheria wote duniani na kuacha kumbukumbu ktk medula oblongata zao ambayo haitafutika. Lisu kama mbunge unyama ule unaingia ktk fikra za wabunge wote wanaompenda na wasiompenda na kuweka kumbukumbu ya kihistoria ktk vichwa vyao hata kama sasa wanajibaraguza. Lisu kama mwanasiasa anaiingiza nchi ktk historia mpya pamoja na kwamba kuna wanasiasa waliokufa vifo vyenye utata, lakini huyu Lisu amemiminiwa risasi nyingi tena katikati ya mchana wa jua kali. Lisu kama mwananchi kumwagika kwa damu yake kutajadiliwa kwa muda mrefu na wananchi iwe positively ama negatively na hili si jambo jema kwa mustakabali wa kizazi cha leo na kijacho. Tuliwahi ambiwa huko nyuma ' za kuambiwa changanya na za kwako' na mimi nasema hivi mbele za Mungu kila mtu atatoa hesabu ya kazi yake mwenyewe. Tanzania kama taifa yatupasa tupendane na kutakiana amani, ahsante!