Dogo aliacha chuo ili afanye biashara ya forex! Mtaani kumekuwa kugumu anaomba tumsaidie arudi kuanza chuo tena

Sikumbuki kama Kuna mahali nimeiponda biashara ya forex. Kuna watu wanafanya na Wana pesa nawafahamu vizuri. Ila Ili kuweza kumaster ukafika level yao si chini ya miaka 3 ya kujifunza kwa vitendo na kwa bidii. Nashauri tu kijana ambaye Yuko chuo na anafanya vizuri asiache chuo Ili akafanye forex. Chuo miaka 3 utakuwa umemaliza. Forex unaweza kufanya ukiwa chuo.
 
Una watu wa kumuongoza mkuu? Muunganishe nao basi. Milioni 2 kumpa mtu akajaribishe kama italiwa au vipi sio poa.
 
huyo nyie mwacheni, kama muna madogo wengine hapo, komaeni na madogo, wasome vizuri,...achaneni na hilo lizee na maisha yake,...
Mkuu hao hawatakiwi kuendekezwa watajitambua kwa muda wao..... nina mtoto wa mjomba angu yeye soma soma yake hakuwa serious ni ubishoo na muziki tu ndo ishu zake... sasa hv amesota pale nyumbani na mambo yake ya miziki zaidi ya miaka mitano mpaka amekoma menyewe... juzi kati nimeambiwa ameokoka ameanza kuimba gospel...
 
Sawa mwambie arudi chuo.
Chezea forex ww aliona atachelewa eeeh.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Kuna vijana wapumbavu sana wakisikia Mark wa Fb aliacha chuo huko Havard wanafikiri nao wakiacha chuo huko msewe wanakuja kuwa kama mark wa Facebook🀣
 
Hatusaidii watu walioacha Chuo kwa uzembe wa kutoelimika 'ujinga', aendelee kutrade forex zake.
 
Tamaa mbaya
 
Heading inasema hivyo "dogo aliacha chuo afanye biashara ya forex! Kwa ataesoma juu juu ataona anguko la dogo ni kutokana na forex wakati hata kulima pia alishindwa au angelima na bado angeangukia pua kwenye mavuno.
 
Moja kati ya ushauri bora kabisa
 
Dirisha la kuomba chuo likishafunguliwa aombe chuo chochote anachotaka atapata tu.

Ila kuhusu Mikopo mwambie HESLB wanamtafta, alipe kwanza Hela ya watu ili wapate kusomeshwa wengine wakati yeye akianza chuo upya.

Kuhusu ndoto ya kupata Mikopo tena asahau. Ila chuo atapata tu
 
Anapenda pesa za dezo dezo
Anapenda pesa za kudownload..
Atainamishwa veri suni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…