Hapa mnachofanya ni kutetea tu. Wewe una hata idea how this crisis works and how does it happen?!
Ngoja nikupe mfano kidogo ili uweze kusoma ramani ya nini kinaendelea.
Fumba macho yako hapo halafu wazia kuwa tunafanya biashara kwa barter trade yaani wewe nyumbani kwako hapo na jamii iliyokuzunguka mnatumia ngano.
Sasa ngano iwe ndio nafaka inayokubalika kuliko nafaka zote. Yaani ukiwa na kisado cha ngano unaweza hata badilishana na mtu mwenye ngombe. Yaani kisado kimoja cha ngano kiwe sawa na gunia 5 za mchele na ni sawa na gunia 10 za mahindi.
Sasa hapo ndani kwenye store muwe na gunia kadhaa za ngano mathalani tuseme gunia 100 tu. Halafu gunia hata 10,000 za mchele na 50,000 za mahindi na zingine za ufuta, zingine za nafaka zinginezo ambazo hazina uhitaji mkubwa sokoni.
Sasa namna nzuri ya kuongeza idadi ya gunia za ngano ni kwa kuwa na mbinu nzuri za matumizi ya hizi nafaka nyingine kuweza kupeleka bidhaa huko nje ambazo majirani watapenda na kukubali kubadilishana kwa ngano.
Mfano mkapika kashata za ufuta, wali, ugali na kuweza kuwapata wateja wa hizi bidhaa na kuweza kuzinunua kwa kisado cha ngano na kuwafanya kuongeza kwa kasi sana stock ya ngano mliyonayo na kuwapa purchasing power kubwa sababu mnayo nafaka inayohitajika katika soko kwa wingi sana kwenye store.
Kinyume chake ni mkae mkitumia ngano ya store kupata mahitaji mbali mbali na kuifanya kupungua kiasi kwamba ifikie minimum stock level ambayo hamtaweza sasa kusustain maisha yenu kwasababu hakuna ngano ya kutosha.
Kama umeelewa huu mfano, then kwenye ngano weka dola, na kwenye nafasi ya nafaka weka pesa yaani tz shilling halafu ongezea na resources zingine ghafi tulizonazo ambazo serikali hutumia kupatia mapato.
Sasa unahusishaje uhaba wa dola kwenye uchumi na vita vya Ukraine sijui COVID-19, yaani hivi vitu vinahusiana nini na sisi kukosa akili na uwezo wa kukusanya dollar wakati huko nje tumezungukwa na mataifa kibao ambayo yanahitaji bidhaa tunazoweza tengeneza hapa ndani na kuziuza kwa misingi ya dola.
Sent from my JKM-LX1 using
JamiiForums mobile app