Donald Trump anatangaza Vita Rasmi dhidi ya LGBTQI+

Donald Trump anatangaza Vita Rasmi dhidi ya LGBTQI+

Oyaa jamani hivi mnafatilia hii speech??.

Jamaa anasema kuanzia Sasa, Marekan itatambua Jinsia mbili tu ambayo ni Ke na Me, na ambazo hutambulika mara tu ya kuzaliwa 🤣🤣🤣🤣

Woyooooooo

Hii naona Elon Musk amemwambia na ku -influence Trump aipiganie kwa nguvu zake zote. Elon ana hasira mtoto wale alizaliwa mwanaume (Xavier) anakapewa hormones blockers zimemsadia kuwa Transwoman (Vivian).

Elon amesema atapigana vita kuondoa hivyo vitu sababu anasema walimdanganya ili akatoa ruhusa mtoto wake apewe hayo madawa.

Museveni alianzishe sasa! Amalizie ile sheria yake iliyoishia njiani baada ya kupata vitisho toka tawala za kishoga. Now has full support from his excellence D. Trump.
Kweli museven atapata nguvu sasa walikuwa wanampiga vita sana naamini kwa nchi kama Amerika ni nchi yenye nguvu duniani naamini tutaungana kote kumsuport trump naamini mungu atatusamehe kutuepusha na majanga na magonjwa
 
ELIMU ELIMU ELIMU... Jamaa ànasisitiza ELIMU juu ya Nuclear Family, Baba ,Mama na Watoto.

Eti siku hizi vitabu vya watoto wetu Hawa, vinawafundisha aina ya familia...

1- Mwanaume na Mwanaume, watoto.

2-Mwanamke na Mwanamke , watoto.

Maajabu Mawaziri husika wapo 🤣🤣🤣
Nafikiri atapigwa vita sana sababu wengi wakubwa wanaafiki hayo mambo. Wengi kwenye establishment wamefanya na wanafanya hayo mambo.

Issue nyingine anataka kumaliza vita ya Ukraine na Russia. Anawaambia Ukraine wasipigane kulomboa Crimea na Donbas bali kuwe na DMZ hapo walipo.
 
Apigwe na nani Amerika ndio supar power duniani hao watakaomponga ni nani? Ingekuwa ni raisi wa nchi za Africa ningekuwa na wasiwas kidogo lakini raisi wa Amerika hio imeshaenda
 
USA, sasa yataka kurudi tena katika namna ya ilivyojengwa na waasisi wake

USA navyoijua mimi, ilijengwa kwenye msingi wa Mungu, na ndiyo maana hata Dollar yao imeandikwa, In God we trust!

Goo goo goo Trump
 
USA, sasa yataka kurudi tena katika namna ya ilivyojengwa na waasisi wake

USA navyoijua mimi, ilijengwa kwenye msingi wa Mungu

Goo goo goo Trump
Ile
Serikali Haina faida zaidi ya kufanikisha malengo ya kishetani.
America in Kauli mbiu nzuri sana "In God we Trust" halafu unakuta kuna huu ushetani mkubwa sana unqanzia huko huko USA
 
Hayo siyo aliyoyasema, shida yenu ni kutojua Kizungu pamoja na kukosa elimu.

Elimu ya Tanganyika inazalisha watu wasiojua hata kusoma wala kuelewa lugha yoyote lakini wana vyeti vyenye MUHURI WA NDALICHAKO.

Donald Trump anachopinga ni kufundisha watoto masuala ya Kingono ikiwemo TRANSGENDERISM, which is good. Watoto waachwe. Hajapinga USHOGAAH.

Na pia uelewe kwamba maswala ya ushoga Marekani ni ya kisheria, sio mambo ya ROPOROPO za majukwaani.

Kule kuna sheria za kuwalinda watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja, lakini pia hata Katiba yao inalinda haki hizo, Na isitoshe hata MAHAKAMA YA UPEO imeshaweka AMRI kwamba Ushoga ni RUKSA MAREKANI.

Kazi ya Rais wa Marekani sio kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda. Akifanya hivyo atang'olewa kama jibwa koko. Lazima akae kwa kujishikilia, ile ni AJIRA kama ajira za AJIRA PORTAL.

Mengine anayoropoka ni maporojo tu ya kuwashika masikio mazuzu na kuwadanganya danganya ili siku zisonge. Hakuna hata Kimoja anachomaanisha hapo.

Cc: Nyani Ngabu FaizaFoxy Stuxnet Lucas Mwashambwa ChoiceVariable chiembe Poor Brain Mbaga Jr Dkt. Gwajima D DR Mambo Jambo min -me raraa reree mshamba_hachekwi mzabzab Mzee wa kupambania Extrovert
 
Sasa ivi ameshakuwa raisi hizo kesi zinazomkabili zitatupwa mbali kama uamininayokwambia ngoja aingie ikulu utaamini na sasa atakuwa na ulinzi mkubwa sana huyo ni raisi wa Amerika mkuu huyo tena sio mwenzangu na mie

Anaweza kujiwekea kinga kwa kesi fulani sababu atamteua Attorney General na kuzifuta kadhaa. Ila kuna ile kesi nyingine zitaahirishwa hadi amalize awamu yake. USA wana utaratibu huo apambane nazo akimaliza muhula wa urais wake.
 
Museveni alianzishe sasa! Amalizie ile sheria yake iliyoishia njiani baada ya kupata vitisho toka tawala za kishoga. Now has full support from his excellence D. Trump.
Usimponze kibabu wa watu muache ajifie taratibu kashajichokea anasubiri kukata ringi tu.

Yule huwa akibabanishwa kisawasawa na waganda anaibua ajenda ya ushoga ili kuzima joto la kisiasa. Pakipoa kidogo unashangaa ANAYEYA halafu sheria anaifuta kimya kimya ili apewe chochote kitu na MABEBERU.

Lile ZEE ni janja mno ila limechoka sana kwa sasa.

Cc: Poor Brain Extrovert Mzee wa kupambania
 
Nafikiri atapigwa vita sana sababu wengi wakubwa wanaafiki hayo mambo. Wengi kwenye establishment wamefanya na wanafanya hayo mambo.

Issue nyingine anataka kumaliza vita ya Ukraine na Russia. Anawaambia Ukraine wasipigane kulomboa Crimea na Donbas bali kuwe na DMZ hapo walipo.
Mkuu, haijarishi itakuweje, ila acha vita vipiganwe, tangu leo naanza kumwombea Trump

Nimekuwa na msongo wa mawazo kwa maisha yangu kufikiri itakuweje siku moja mtoto wangu wa kiume aje kuwa shoga na eti mpumbavu mmojanaye wa kiume aje kuleta posa kwa mwanangu wa kiume??
 
Kwani Trump atafanya nini kuzuia ushoga?
 
Usimponze kibabu wa watu muache ajifie taratibu kashajichokea anasubiri kukata ringi tu.

Yule huwa akibabanishwa kisawasawa na waganda anaibua ajenda ya ushoga ili kuzima joto la kisiasa. Pakipoa kidogo unashangaa ANAYEYA halafu sheria anaifuta kimya kimya ili apewe chochote kitu na MABEBERU.

Lile ZEE ni janja mno ila limechoka sana kwa sasa.

Cc: Poor Brain Extrovert Mzee wa kupambania
Muda sio mrefu litapiga hela. Linakaribia kutiririsha wese for export.
 
Back
Top Bottom