Kwa kweli Wairan wanatakiwa kusaidiwa. Wairan wameishi kwa mateso makubwa kwa miaka mingi , sababu ya mtu mmoja. Hii siyo sahihi kabisa. Wanaishi kwenye umaskini mkubwa, umaskini uliotengenezwa na watawala. Iran, kwa rasilimali zake, aina ya watu wake toka historia za kale, lilitakiwa kuwa Taifa lenye utajiri mkubwa na maisha yenye matumaini makubwa kwa watu wake.
Njia za kidiplomasia, njia zisizo za umwagaji damu, kama za vikwazo, zote zimeshindwa kumbadilisha mtawala katili ambaye kila siku anazidi kuwaua Wairan.
Wairan wasaidiwe, lakini je watasaidiwa kuwa huru, bila ya hao hao wanaosaidiwa, kuishia tena kufa kwa maelfu?
Waandae utaratibu utakaolinda maisha ya watu wakati wa hiyo vita ya kumwondoa mtawala katili, Ayatollah. Yule Rais wa sasa wa Iran, haonekani kuwa na matatizo, toka mwanzo alionekana kuwa tayari kufanya mageuzi ya mifumo itakayoifanya Iran kuwa na uhusiano mzuri na jamii ya kimataifa. Tatizo ni Ayatollah.
Ingekuwa ni rahisi, ilikuwa kumbana Ayatollah, kisha Wairan wapige kura ya maoni kuamua wanataka mfumo wa namna gani wa kiutawala. Kisha wawachague watu wanaotaka wawaandalie rasimu ya katika mpya ya nchi. Tatizo, uwezekano wa Ayatollah kukubali kufanyika hilo kwa njia ya amani, ni vigumu sana.