Mkuu Urani kaua raia wake 12,000+ ,kwako hii ni sawaYaani mie najiuliza tu swali la kawaida : Kinachomfanya Marekani ajiandae hivi kumvamia Iran ni kipi?
Iran amemkosea nini?
Ayatollah amemkosea nini?
Au ndio huo ubabe tuu
Kwamba USA anaweza pia kuangusha utawala wa IRAN?Ayattolah hataweza kukimbia itakuwa kama Sadam Hussein.
Kiongozi pekee alieweza kukimbia au kuokolewa hadi sasa ni Assad wa Syria alieokolewa na Russia.
Na hiyo ni kwasababu hata hivyo alikuwa na "strong connection" na Moscow na London, amewekeza sana kule na mkewe pia alikuwa na "connection" na UK.
Yaani mie najiuliza tu swali la kawaida : Kinachomfanya Marekani ajiandae hivi kumvamia Iran ni kipi?
Iran amemkosea nini?
Ayatollah amemkosea nini?
Au ndio huo ubabe tuu
Kwamba USA anaweza pia kuangusha utawala wa IRAN?
Tusisikie story "Allah Save Iran"Iran huwa anaviziwa Hata mwanzon walimvizia lakini saivi hili vumbi itakua mtihani, muajemi sio Venezuela vita ya upande mmoja hapa wote wanaumia
Iran sio SyriaTusisikie story "Allah Save Iran"
Ukraine haitoisha kamwe, itasimama tu1. Drc
2. Gaza
3. Ukraine
Ha ha ha mnajua nyie mnaona Marekani ni kama Tanzania au Kenya hivi, US ni kitu kingine kile vijana.Yes, ni kweli Iran sio Venezuela na kinofanyika kwa sasa ni Iran asubiria kuwe na "trigger act" kutoka kwa Marekani.
Taarifa za kijasusi zaonyesha kuwa Iran imeingiza mafuta ya kutosha kutoka China ili kutumia kwa makombora yake (ballistic missiles) yapatayo 500 na makombora hayo yamo ndai ya uwezo wake kufikia hiyo meli. na meli ziko tatu hiyo ya Abraham Lincoln na zingine mbili.
Kiukweli Marekani walikuwa wafanye mashambulizi wiki ilopita ila wakasitisha hilo kwa kuhofia kambi zake kugeuzwa vumbi na kwamba Israeli bado haina mifumo imara ya ulinzi, kwani Iran wamesema shambulio lolote kwao litajibiwa na Iran kushambulia maslahi ya Marekani popote pale na mojawapo ni Israeli.
Donald Trump kwa sasa akumbwa na sintofahamu kwani akiiacha Iran bila kuishambulia Marekani itaonekana ni dhaifu na akiingia kichwakichwa kufanya mashambulizi huku akiwa hana ulinzi wa kutosha kwenye kambi zake pamoja na Israeli na Iran ikajibu vilivyo hiyo itakuwa ni aibu kubwa kwake.
Hivyo ndo nikasema sasa hivi ni mchezo wa kiviziana wa paka na panya.
Kwenye haya maandamano ya juzi huenda kuna kitu kiliendelea ndani ya Iran bila wao wenywe kujua na huenda pia shambulio tayari liko mezani.Nia ipo ila kwa sasa ni mchezo wa paka na panya.
Marekani kuipelekea hiyo meli yao kubwa baada ya kazi ya Venezuela, waonyesha ulimwengu dhamira yao, yaani kuwabana China na Russia katika maeneo wanoamini ni yao.
Nyuma yake kuna suala la mafuta na Marekani wataka kuumiliki mazima mfereji wa Harmuz unokutanisha ghuba ya Uajemi, kisiwa cha Musandam pamoja na Oman, hapo asilimia 20 ya mafuta yanokwenda Duniani yapita hapo. Ikitokea Iran ikabinywa vilivyo basi yaweza kuufunga mfereji huo na kusababisha matatizo makubwa ya kiuchumi Duniani kwani bei ya mafuta itafurumuka na pia kusababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa zinginezo.
Hivyo kazi ya kuhakikisha Iran hatakuja kutenda hayo kwenye "worst case scenario" alipewa Israeli na tiyari hadi sasa kavunja uwezo wa Hamas, Hezbollah na kundi la Wahuthi wa Yemen kushambulia meli na miundombinu ingine ya Marekani na nchi za magharibi.
Sasa Marekani ana "options" zipi mezani juu ya kuishambulia Iran?
Moja, njia ya amani yaani matumizi ya diplomasia kwa kuongeza shinikizo kwa Iran kwa vikwazo zaidi.
Pili, kubandika tozo ka bidhaa ambazo Iran waziuza nje khasa mafuta machafu na vifaa zingine nyeti.
Tatu ni kufanya mashambulizi kwenye mitandao na mifumo ya Iran khasa katika jeshi lake la kimapinduzi la IRGC.
Mashambulizi ya kijeshi.
Mashambulizi hayo yamejigawa katika sehemu tatu.
1. Wanaweza kushambulia mitambo ya nyuklia na ili kuua uwezo wa Iran kufanya counter attack.
2. Wanaweza kushambulia mifumo na vituo vya kijeshi vya IRGC kazi ambayo ni ngumu kwani watu wengi watauawa kutokana na kwamba IRGC wamejenga vituo vyao katika maeneo tofauti na yalo katika makazi ya watu.
3. Pia wanaweza kushambulia visima vya gesi na mafuta kwa kutumia ndege za kivita ambazo zitafanya kazi iitwayo "shop sharp" na "surgical strikes" ambazo zinalenga seheu hizo tu bila kuleta madhara makubwa.
Kwa kuwa majasusi wa CIA na Mossad wapo ndani ya Iran kwa sasa, wao ndo wataoelekeza wataotoa au wametoa ramani za mashambulizi.
Ni hayo tu mkuu.
Israel tayari kasema yuko tayari kupigwa mabomu 700 toka Iran endapo kama yatafanikiwa uuondoa uongozi wa IranHivi ni kweli Marekani amedhamiria kushambulia Iran au ni kitisho tu?
True akipigwa ugaidi utapungua duniani.Iran mfadhili mkubwa wa ugaidi duniani apigwe tu hakuna jinsi nyingine
HataMaduro alikuwa na mawazo kama yakoHiyo aircraft carrier yenyewe kila inapopita inapigwa picha na Iran.
Haitasalimika hiyo.
China amepeleka ndege 30 za mizigo ya silaha Iran.
Urusi naye vivyo hivyo.
Alichobugi USA ni kukubali kuondoka Ain Al Asad pale Iraq.
Iraq nayo imempa uwanja Iran kutumia kijeshi. Safari hii wanachokitafuta watakipata.
Irani ni mfadhili kubwa wa ugaidiYaani mie najiuliza tu swali la kawaida : Kinachomfanya Marekani ajiandae hivi kumvamia Iran ni kipi?
Iran amemkosea nini?
Ayatollah amemkosea nini?
Au ndio huo ubabe tuu
Yeye alidai amemaliza vita 6 tokea awe Rais!! Na ndio kilichofanya adai Nobel peace prize na pia kupewa FIFA peace prize!!!hapo hakuna vita iliyoanzishwa na Marekani.
DRC kaikuta,
Gaza kaikuta,
Ukraine ni ya NATO.
Gaidi gani? Mbona Marekani na Israel imemfadhili Al Jolani hadi kuwa Rais wa Syria ilihali ni kiongozi wa Al Qaeda? Hata SDF rebels na PKK wanatambulika kama magaidi ila mbona Israel na USA inawapatia silaha, fedha na mafunzo?Irani ni mfadhili kubwa wa ugaidi