Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Dondosha mstari wowote wa Biblia unaoupenda leo ni Ijumaa

Warumi 12:14-17
Wabarikini wanaowaudhi;barikini Wala msilaani.Furahini pamoja nao wafurahio;lieni pamoja nao waliao.Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi.Msinie yalio makuu,lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.Msiwe watu wa kuji vunia akili.Msimlipe mtu ovu kwa ovu,angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
 
,
Screenshot_20230303-100543.jpg
 
Luka 18:6-8
Bwana akasema,sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.Na Mungu,je! hatawapatia haki wateule wake wanao mlilia mchana na usiku,naye ni mvumilivu kwao?.Nawaambia atawapatia haki upesi;walakini,atakapo kuja Mwana wa Adamu,je! ataiona imani duniani?.
 
Yesu ni Mungu

Yesu ni Mungu

Yn 1:1...... SUV​

Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
 
Biblia haina tofauti na zile hadithi za akina Abunuwasi. Uongo mtupu, cha ajabu utakuta mtu msomi kabisa anaamini yaliyoandikwa humo.
 
Mimi yesu sio mungu yupo mungu Alie niumba Bali kwa upumbavu wenu mnaniita mungu.ngojeni siku yamwisho nije kuwakana ndio mtajua Kumbe hamjui.
Biblia ipo kimafumbo sana. Ukisoma kama gazeti unapata tafsri yake kama ulivyoandika.
Yesu ni mwana wa Mungu. Soma Yohana 3.16-17 Kwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili tupate kuokolewa.
Yakobo 2:17 Imani bila matendo mema imekufa.
Yesu alikuwa ana maana gani? Kukana? Ufanye uzinzi, uwe mwizi, udhulumu wa watu, ufanye kila aina dhambi. Hautaki kutubu, kwenye nyumba ibada upo, unaimba kwaya na kuhubiri huku matendo yako ni mabaya. Atakukana ndiyo maana yake.
Yohana 14:6 Mimi ndiye njia ya ukweli na uzina

1 Kor 6:9-11​

Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
 
Mimi yesu sio mungu yupo mungu Alie niumba Bali kwa upumbavu wenu mnaniita mungu.ngojeni siku yamwisho nije kuwakana ndio mtajua Kumbe hamjui.
Zaburi 92 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ Ee Bwana, jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
⁶ Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.
 
Back
Top Bottom