DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Yule Mwijaku hua anajisifu kua ni msomi,ila watu humtukana na kumwambia,usomi wake umeishia kwenye uchawa tu,
Dotto yeye hajasoma na amekua Chawa,na yeye anatukanwa pia!
😀 😀
Doto hajawahi kuwa siriaz anachangamsha tu gengeAnaweza kua na hoja ila uwasiliahaji zero.
Mzoee tu mzaramo huyo hajawahi waza atakwaza watu wengine matani muda woteMbona anatukana tu hatoi hoja. Tatizo la watu wenye elimu ndogo ni moja wana hasira na watu wenye elimu kubwa, na wanataka kuwaona wanafeli kiuchumi ili wawatumie kama mifano kusema elimu ya darasani haina maana kwasababu wao hawana. Anadai wasomi wanatembelea IST, hii sisi wasomi tunaita hasty generalization. Kuna wasomi wengi wanatembelea gari bei kubwa ambazo walizipata kupitia benefits za elimu zao. Pia gari sio kipimo cha mafanikio ya kiuchumi mwambie doto magari kabla ya kuwaita watu wana njaa anastahili japo ka course kuhusu mambo ya development ajue tunapimaje umasikini.
Heheee eti hakuna msomi tajiriMaisha ya katalizumu mwenye degree anamsikiliza mwenye zero ,Super Feo ni darasa la 7 lakini ni Bilionea.
Hakuna msomi tajiri ,ukiona msomi tajiri basi ameiba kupitia peni yake ,lakini hawa type za kina Dotto magari ,mwijaku vipaji vyoa ndiyo vinawapa maokoto tena ya maana ,mwijaku alisema kuna baadhi ya makampuni yanam,lipa hadi milioni 50 kwa kazi ya wiki mbili au mwezi hiyo nje ya matumizi hiyo ni net ,gharama za hotel,nauli,chakula juu ya kampuni.
Pesa hizo nasikia huwa za majini sijui mwijaku kawezaje mwenzie baba levo anachezea tu makamaliMaisha ya katalizumu mwenye degree anamsikiliza mwenye zero ,Super Feo ni darasa la 7 lakini ni Bilionea.
Hakuna msomi tajiri ,ukiona msomi tajiri basi ameiba kupitia peni yake ,lakini hawa type za kina Dotto magari ,mwijaku vipaji vyoa ndiyo vinawapa maokoto tena ya maana ,mwijaku alisema kuna baadhi ya makampuni yanam,lipa hadi milioni 50 kwa kazi ya wiki mbili au mwezi hiyo nje ya matumizi hiyo ni net ,gharama za hotel,nauli,chakula juu ya kampuni.
A). Mfanyabiasha Maarufu wa Magari nchini Ndugu Dotto Magari ameonekana kwenye mitandao akizungumzia namna Wasomi nchini wasivyojitambua Wala kutumia usomi wao kuongeza kipato. Na kutishia kwenye dimbwi la umaskini akifanikiwa Sana ananunua Hari ya IST Tena Kwa mikopo wa benki.
B). Namnukuu "wasomi mmesomea Njaa" jaman lolote.
C). Mheshimiwa Dotto ana hoja ya msingi kuhusu kubweteka Kwa Wasomi wetu. Asikilizwe, ana hoja.
NB: Wasomi msikilizeni Kwa makini, msitumie mihemko kumjibu. Bali jibuni hoja kwa hoja. Msimtukane Wala kumbughudhi hapo ndo kipimo cha usiku wenu kitaonekana.
Heheee eti hakuna msomi tajiri
Vipi ukikutana na alieafaulu ana elimu kubwa na V8 anayo unapanda?Lakini ujikute umesoma halafu unaungaunga maisha, wakati huku wazugaji wanajua kuitega hela, halafu ukikitana na washkaji mliosoma nae primary wakafeli leo hii wanakupa lift na Range Rover.
Mimi huwa nakataa lift zao, lakini pia huwa najiona fwamba kinoma yaani
Huu ndio ukweli
Vipi ambao walipata mitaji ya biashara kupitia mishahara?Rudia kusoma tena ukiona msomi tajiri jua amekwiba ....sizungumzii ma CEO wanaolipwa milioni 50 kwa mwezi hao ni masikini tu ndiyo maana still wameajiriwa....Wasomi mtajari ni design ya late Mengi ,Mafuruki ,walikuwa wanarun bizness zao ila behind ya kuwa matajiri kila mtu anajua.
Acha kuongea kama mwendawazimu , Jamie Daimon CEO WA Jp Morgan unajua analipwa bilioni ngapi kwa mwaka wewe ?Rudia kusoma tena ukiona msomi tajiri jua amekwiba ....sizungumzii ma CEO wanaolipwa milioni 50 kwa mwezi hao ni masikini tu ndiyo maana still wameajiriwa....Wasomi mtajari ni design ya late Mengi ,Mafuruki ,walikuwa wanarun bizness zao ila behind ya kuwa matajiri kila mtu anajua.
kweli Mkuu hii nime experience pia samahani kwa kuongea hv ila asilimia kubwa ya walio na elimu ndogo wakibahatika kushika hela wanajisahau sana ile self awareness haipo kbsa ndio maana jamaa yupo vile kujiona amemaliza... Ukitka kujua ilo muangalie yule mwenzie wa kigoma wanatofauti kubwa sana sidhani jamaa kma ataweza ku mantain Brand yake hata kwa miaka 3 ijayo kwa hizo sifa mbegele alizonazo asijeshangaa anarudi tena kule kule japo ni Mungu ndie ajuae mienendo yetu na mwisho wetu maana hzi hela za upepo usipokua conscious na maisha ya mjini utajiona mtu kumbe watu wanakusubiria tu uporomoke wakucheke na maneno yako!!!!Inasikitisha anaua brand name ya biashara yake mbele ya wateja
Tatizo la kutosoma ndio hilo hajui brand ni nini? Inajengwaje na inakufaje? Yeye kaamua kuua brand na kukimbiza wateja
Shida ya kutosoma hiyo.Wateja wasomi ndio bye bye mjinga sana huyo
wambieni Doto Magari kwamba kunatofauti kubwa sana kati ya kuwa msomi na kuwa tajiriA). Mfanyabiasha Maarufu wa Magari nchini Ndugu Dotto Magari ameonekana kwenye mitandao akizungumzia namna Wasomi nchini wasivyojitambua Wala kutumia usomi wao kuongeza kipato. Na kutishia kwenye dimbwi la umaskini akifanikiwa Sana ananunua Hari ya IST Tena Kwa mikopo wa benki.
B). Namnukuu "wasomi mmesomea Njaa" jaman lolote.
C). Mheshimiwa Dotto ana hoja ya msingi kuhusu kubweteka Kwa Wasomi wetu. Asikilizwe, ana hoja.
NB: Wasomi msikilizeni Kwa makini, msitumie mihemko kumjibu. Bali jibuni hoja kwa hoja. Msimtukane Wala kumbughudhi hapo ndo kipimo cha usiku wenu kitaonekana.
Nitajie tajiri mkubwa duniani ambaye sio msomi katika top 100 ya duniaM
wambieni Doto Magari kwamba kunatofauti kubwa sana kati ya kuwa msomi na kuwa tajiri
Matajiri wengi sana wakubwa sana duniani sio wasomi
Kuna fursa sawa ya kuwa tajiri kati ya msomi na asiye msomi
Dokta anakua msomi ili kuja kuwatibu watu, injinia anakua msomi ili kuja kuinjinia majengo magari nk. Mwalimu anakua msomi ili awafundishe watu, Mwanajeshi anakua msomi ili alitumikie jeshi nk nk
Huu ndio msingi wa usomi
Tatizo la watu wanaojiona sio wasomi wanasumbuliwa na kasumba ya inferior complex
Na kwa bahati mbaya sana wasomi wetu ambao muda wao mwingi unatumika makazini wanalipwa mishahara midogo ambayo inawafanya akina doto magari kuanza kuwatukana ni masikini huku wamesoma
Asichojua Doto magari na wajinga wajinga wengine kama wewe mnao muunga mkono ni kwamba kama hawa wasomi wetu wangekuwa wanalipwa vizuri kama wanavyolipwa wasomi wa USA UK nk Doto asinge waita masikini
Kwa mazingira ya kibongo asiye msomi na anafanya shughuli zake binafsi ana nafasi kubwa ya kuwa tajiri kuliko msomi mwenye master yake lakini kabanwa na kazi siku nzima halafu ukataka afanye maajabu ya kuwa tajiri kisa usomi wake
Na ukiangalia yeye hana wigo mpana kama wengine wale walivyojishikiza kwenye Station za redio mbali mbali... asipoangalia ata baadhi ya endorsement atapoteza kwa upuuzi wake wa kizaramo na mbuli kumlomo zakeInasikitisha anaua brand name ya biashara yake mbele ya wateja
Tatizo la kutosoma ndio hilo hajui brand ni nini? Inajengwaje na inakufaje? Yeye kaamua kuua brand na kukimbiza wateja
Shida ya kutosoma hiyo.Wateja wasomi ndio bye bye mjinga sana huyo
Nikikutajia ndio utakubaliana na hoja yangu?Nitajie tajiri mkubwa duniani ambaye sio msomi katika top 100 ya dunia
Bado anatakiwa kupigwa msasa,kama huna akili sasa utaweza vipi kusoma,labda angesema wasomi wana akili ila maarifa hawana hapo kidogo ningemuelewa.Kuna point moja ameiongelea hapo,
Namnukuu;
"Unaweza ukawa umesoma ila ukawa huna akili,na unaweza ukawa na akili ila ukawa haujasoma"
Bila shaka hapa ndio kwenye point yake hasa.