Doto Magari ana hoja kuhusu Wasomi, asikilizwe!

Bado anatakiwa kupigwa msasa,kama huna akili sasa utaweza vipi kusoma,labda angesema wasomi wana akili ila maarifa hawana hapo kidogo ningemuelewa.
Mkuu,huwezi kuikwepa elimu hata siku moja,
Umuhimu wa elimu utakuwepo mpaka mwisho wa Dunia,

Hiyo simu aliyoitumia kujirekodi ni matokeo ya elimu,Gari alilopanda ni matokeo ya elimu,Nguo alizovaa,Saa aliyovaa,Viatu alivyovaa,pamoja na vingi anavyovitumia katika maisha yake ya kila siku,ni matokeo ya elimu,

Mpaka Nyumba anayoishi,ni matokeo ya elimu,

Asiyekua na elimu kua na hela kuliko mwenye elimu haijustify kua Elimu sio kitu.
 
Anauza magari yakiharibika anatengeneza yeye? Kama shule ilimkataa akomae na biashara, kuna wengine shule iliwakubali akitaka kujenga ghorofa atawafuata wasomi maana hata Raman hajui kutengeneza
 
Kama umesoma inabidi unyang'anywe vyeti kwasababu unayumbishwa na watu wajinga na hujiamini. Mengi alikuwa kilaza? Halafu milioni 50 unaichukuliaje ndugu? Ingekuwa Mwijaku analipwa 50m kwa wiki 2 ingeonekana tu kupitia matendo yake. Hela ni kama ushuzi.. haifichiki kirahisi.
 
Walio karibu yake wamwambie hana akili hata ya kuzaliwa
 
Moral Of The Story: Usipoteze mamilioni yako kusomesha watoto kwenye shule za English Medium kwa sababu hakuna mantiki wala ulazima wowote wa kufanya hivyo.

Toa watoto wako ENGLISH Medium haraka sana wapeleke Kayumba
Ushauri wako ni wa kipumbavu.
 
Doto

Atakuja kufeli vibaya sana huyu

Hii ni Dunia
 
Utajiri ni utajiri haijalishi umeajiriwa au umejiajiri. Ili mfanyabiashara aweze kuingiza Tsh 50m kwa mwezi kama net profit inabidi awe na mauzo yasiyopungua Tsh 350m kwa mwezi. Kwahiyo usichukulie poa mshahara wa mfanyakazi yeyote. Waliojiajiri wanachofaidi ni uhuru ila kwenye pesa usidhani ni rahisi tu.
 
Hujamuelewa.
 
Pesa sio kipimo cha akili hata malaya wanaojiuza na majambazi wauaji wana pesa
 
Cha kukuongezea tu mkuu ni kwamba huyo mburula hauzi magari yake binafsi, ni dalali wa kuuza magari ya wanaume wenzie yeye ni mpiga domo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…