DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

Mpumbavu wewe usiyejua mipaka ya IGA ipo vipi, hizi project contracts zilizoandaliwa zimezaliwa baada ya IGA kupitishwa bungeni. Tatizo ni lile lile la kujifanya unajua sana mpaka unatumia na matusi kwenye sentensi zako.
IGA ni Dubai na Tanzania, hizi projects zinazofanyika sasa ni nje ya IGA, hazina uhusiano wowote na IGA.
 
Ni wa mwanzo kabisa, kuna tender zimetangazwa za bandari nyinginezo za hapa hapa Tanzania.
Hiyo yote ni mipango iliyoandaliwa tokea awali, hata kabla ya ufisadi wa IGA haujazaliwa, na itatekelezwa nje ya IGA ya Dubai.
Hilo ndilo unalotakiwa kulifahamu.
 
Habari njema kwa watanzania wanaopenda kuona taifa lao likisonga mbele kimaendeleo karibuni sana DP WORLD tulisukume gurudumu la kuikuza Tanzania kiuchumi.
 
Kosa lililofanyika la mkataba kuvuja na ukageuka kujadiliwa mpaka na wauza maembe njiani halitafanyika tena kwenye mikataba hii ambayo zabuni zake zinatangazwa muda huu.

Serikali imejifunza jambo moja la maana sana.
Jambo la maana sana waTanzania walilojifunza ni kuwa serikali ya Samia ni serikali ya kifisadi, serikali isiyoweka maslahi ya nchi hii mbele ya jambo lingine lolote; serikali iliyo tayari kuwahujumu wananchi wake na kuwafanya kuwa watwana mbele za vitaifa ambavyo sifa pekee vilivyo nayo ni kuwa na ukwasi.

WaTanzania hawataruhusu tena serikali ya namna hiyo itokee tena nchini mwao.
 
Kelele za Watanganyika kulilia dhidi ya mkataba mbovu wa bandari, hazijasikilizwa na DP WORLD wanaingia rasmi ofisini tarehe 01 November.

Watu walikuwa wanadhani watendaji wa DP WORLD ni Waarabu, hapana, kuna Wazungu, Wahindi, Wafilipino na watu weusi.
Sidhani kama DP World ama mawakala wao wa hapa nchini watakuwa na ubavu wa kuweka miguu yao kwenye bandari ya Dar!. Siamini kama hawajitaki!! Mungu wetu ni mkuu sana! Kama hawajitaki ngoja tuone!!
 
Jambo la maana sana waTanzania walilojifunza ni kuwa serikali ya Samia ni serikali ya kifisadi, serikali isiyoweka maslahi ya nchi hii mbele ya jambo lingine lolote; serikali iliyo tayari kuwahujumu wananchi wake na kuwafanya kuwa watwana mbele za vitaifa ambavyo sifa pekee vilivyo nayo ni kuwa na ukwasi.

WaTanzania hawataruhusu tena serikali ya namna hiyo itokee tena nchini mwao.
Ungejua kuw DP World atakapofunga mitambo yake pale bandarini hiyo Serikali itakuwa imeweza kupambana na ufisadi wa sekta ya uchukuzi usingeandika hayo maneno yako.
 
Mambo yakisemwasemwa sana hata kama ni ya kipuuzi hujiumba na kuzaa tukio halisi....
 
Ungejua kuw DP World atakapofunga mitambo yake pale bandarini hiyo Serikali itakuwa imeweza kupambana na ufisadi wa sekta ya uchukuzi usingeandika hayo maneno yako.
Ufisadi wa hapo bandarini unajulikana, na wote unatokana na hao hao wanaotafuta kutuingiza kwenye mikataba ya hovyo kama hiyo IGA.
Ila IGA imekwenda mbali sana, inatafuta hata kutuuza utumwani. Huu siyo ufisadi wa kawaida kama huo wa vifisadi wa hapo bandarini.
 
Back
Top Bottom