DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

Sheria ya maliasili inapingana na mkataba wa DPW, ngoja tusubiri!
 
Mi sikutaka poteza muda na mate kuupinga maana ungepitishwa tu
 
Mimi kama mtanzania;
Mimi kama mtanganyika;
Mimi kama mkatoliki;
Mimi kama mtu mwenye utimamu wa akili;
Naisubiri ccm uchaguzi mkuu wa 2025; kama kweli dp world watatia mguu Tanzania kwa mkataba ule.
Njia ya kura ilishapoteza nguvu yake. Kwa sasa wanaweza kutangazwa washindi kwa idadi ya kura wazitakazo, machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatarejesha heshima ya box la kura.
 
Hujui lolote bora ukae kimya tu kama kiburi chako kinakunyima uwezo wa kupata taarifa sahihi kutoka kwa watu mbalimbali.
Wewe ni 'bogus' kabisa.
Uliingia humu JF kwa hilo jina jipya kwa kusudi moja tu la DP World. Hii ina maana huu mradi wa kifisadi ulikuwa unakuhusu kwa karibu sana.

Uwezo wako wa kutetea umeonekana ni mdogo sana, ikiwa na maana shule ya maana huna. Hili halishangazi, kwa sababu utawala huu wa Samia watu wa aina yako ndio mtaji mkubwa sana katika serikali hii.

Sasa mlifikiri waTanzania ni wajinga, kumbe ujinga unawahusu nyinyi wenyewe.
 
Kelele za Watanganyika kulilia dhidi ya mkataba mbovu wa bandari, hazijasikilizwa na DP WORLD wanaingia rasmi ofisini tarehe 01 November.

Watu walikuwa wanadhani watendaji wa DP WORLD ni Waarabu, hapana, kuna Wazungu, Wahindi, Wafilipino na watu weusi.
Mkuu TAJIRI MKUU WA MATAJIRI , asante sana kwa hii!, kiukweli kabisa JF, tuna hazina kubwa sana ya watu, tukiwatumia vizuri, tutafika mbali!, kama hii ililetwa humu September, HGA ikasainiwa October!, kazi inaanza November!, wala sikuulizi umeipata wapi!, ni kukuambia tuu asante!.

P
 
Wewe ni 'bogus' kabisa.
Uliingia humu JF kwa hilo jina jipya kwa kusudi moja tu la DP World. Hii ina maana huu mradi wa kifisadi ulikuwa unakuhusu kwa karibu sana...
IGA ilimaliza kazi yake bungeni, ikatoa njia kwa consession na lease agreement, usidanganye watu kwamba IGA haikuwa na kazi, ilifanya kazi yake na ikamalizika kwa taratibu zote zenye kukubalika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Wewe ulifanya fitina mpaka ukaandaa kipindi cha mahojiano katika chombo cha habari ukafikia hatua ya kumhoji mwanasheria kutoka Kenya ili avunje nguvu mpango wa serikali lakini kila ulichokifanya kimefia njiani.

Watanzania wasio wajinga kumbuka pia ni wafanyabiashara wenye kutumia bandari hii na hawa siku zote walilalamika aina ya utendaji unaojaa urasimu pale TPA, hili ni kundi lililofikiwa katika awamu hii.

Mtapiga sana kelele lakini zitaishia hewani.
 
Kelele za Watanganyika kulilia dhidi ya mkataba mbovu wa bandari, hazijasikilizwa na DP WORLD wanaingia rasmi ofisini tarehe 01 November.

Watu walikuwa wanadhani watendaji wa DP WORLD ni Waarabu, hapana, kuna Wazungu, Wahindi, Wafilipino na watu weusi.

MWONGO.
"DP World Kuanza Kuendesha Bandari ya Dar es Salaam...."

Nani kakwambia DP World ataendesha Bandari ya Dar es Salaam. Tuwekee huo ushahidi hapa sote tuuone.

Na kwa kutokuwa na ufahamu wa kutosha, nani kakwambia kilicho kuwa kikipingwa kuhusu hiyo DP World ni Uarabu wa hiyo kampuni?

Mawazo ya namna hii wewe uliyatoa wapi?
 
Back
Top Bottom