Nobunaga
JF-Expert Member
- Mar 22, 2019
- 1,205
- 5,121
Katika hili wala hauhitaji kujua aliye nyuma ya hawa DP World ni nani, haijatokea kwa bahati mbaya, hakuna coincidence hapa, ni mipango iliyopangwa ikapangika na sasa tunaenda kupigwa mchana kweupeee.
==========================
TAARIFA KUHUSU UWEKEZAJI UNAOPENDEKEZWA NA DP WORLD TANZANIA

DP World imejenga kituo cha hadhi ya kimataifa cha bandari kavu na kitovu cha usafirishaji katika Rwanda, ambayo ni ndogo kijiografia na isiyo na bahari yenye uwezo wa kuhifadhi makontena 50,000 kwa wakati mmoja. Kinyume chake, bandari ya Dar es Salaam katika Tanzania kubwa kijiografia ina uwezo wa kuhifadhi kontena 19,000 TU kwa wakati mmoja.
Hii ina maana kwamba kama meli kubwa ya kontena yenye uwezo wa kubeba takriban TEU 20,000 au zaidi ingetia nanga Dar es Salaam, kituo kidogo cha kontena cha bandarini hakingeweza kuhifadhi shehena ya meli moja tu.
Wakati mjadala wa kitaifa wenye SIASA NYINGI ukiendelea kuhusu masharti ya uwekezaji ujao wa DP World nchini Tanzania, bandari ya Dar es Salaam bado ina uhitaji mkubwa wa uwekezaji wa miundombinu. Wakati huo huo, Rwanda tayari imejenga bandari kavu ya hadhi ya kimataifa, na nchi jirani ya Kenya inatafuta wawekezaji wa kibinafsi kuendesha sehemu muhimu za bandari zake za Lamu na Mombasa.
Ingawa hoja halali kuhusu masharti ya uwekezaji inapaswa kushughulikiwa, ni wakati sasa kwa Tanzania kujadiliana na DP World kwa kina kwani bandari ya Dar es Salaam itakuwa kama njia tuu ya kupeleka shehena Rwanda. Hii ina maana Rwanda itakuwa inapata faida kubwa kupitia bandari yetu kulinganisha na sisi.