DP World tayari imejenga "Bandari Kavu" Rwanda yenye uwezo wa kontena elfu 50, wakati bandari yetu ni ya kontena elfu 19 tu

DP World tayari imejenga "Bandari Kavu" Rwanda yenye uwezo wa kontena elfu 50, wakati bandari yetu ni ya kontena elfu 19 tu

Katika hili wala hauhitaji kujua aliye nyuma ya hawa DP World ni nani, haijatokea kwa bahati mbaya, hakuna coincidence hapa, ni mipango iliyopangwa ikapangika na sasa tunaenda kupigwa mchana kweupeee.

==========================

TAARIFA KUHUSU UWEKEZAJI UNAOPENDEKEZWA NA DP WORLD TANZANIA

DP World imejenga kituo cha hadhi ya kimataifa cha bandari kavu na kitovu cha usafirishaji katika Rwanda, ambayo ni ndogo kijiografia na isiyo na bahari yenye uwezo wa kuhifadhi makontena 50,000 kwa wakati mmoja. Kinyume chake, bandari ya Dar es Salaam katika Tanzania kubwa kijiografia ina uwezo wa kuhifadhi kontena 19,000 TU kwa wakati mmoja.

Hii ina maana kwamba kama meli kubwa ya kontena yenye uwezo wa kubeba takriban TEU 20,000 au zaidi ingetia nanga Dar es Salaam, kituo kidogo cha kontena cha bandarini hakingeweza kuhifadhi shehena ya meli moja tu.

Wakati mjadala wa kitaifa wenye SIASA NYINGI ukiendelea kuhusu masharti ya uwekezaji ujao wa DP World nchini Tanzania, bandari ya Dar es Salaam bado ina uhitaji mkubwa wa uwekezaji wa miundombinu. Wakati huo huo, Rwanda tayari imejenga bandari kavu ya hadhi ya kimataifa, na nchi jirani ya Kenya inatafuta wawekezaji wa kibinafsi kuendesha sehemu muhimu za bandari zake za Lamu na Mombasa.

Ingawa hoja halali kuhusu masharti ya uwekezaji inapaswa kushughulikiwa, ni wakati sasa kwa Tanzania kujadiliana na DP World kwa kina kwani bandari ya Dar es Salaam itakuwa kama njia tuu ya kupeleka shehena Rwanda. Hii ina maana Rwanda itakuwa inapata faida kubwa kupitia bandari yetu kulinganisha na sisi.
View attachment 2656852

View attachment 2656853

View attachment 2656854

View attachment 2656854

View attachment 2656855
Kwahiyo tumpe bure kwasababu hiyo sio
 
Kukimbilia kusema kua watu wanao kubali kua tuingie ubia wa kuendesha na kuboresha bandariz etu mnawaona kua wasaliti na wamepewa pesa...huu si ukweli bali ni kukosa tu hekima za kuyajua mema na malengo ya Taifa ili. Vipi,wale mnaopinga mkiambiwa mmeongwa na wafanyabiashara wanao tumia hiyo bandari kutupiga pesa na kuuza vitu kwa bei ya juu sijui utasemaje. Ifike sehem watanzania tukubali kua tunabidi kupiga hatua kwa kufanya maamuzi sahihi. Itakuaje vizazi vyetu vya mbeleni wakute tuna bandari lakini bado maisha ya watanzania ni duni? Si watatuona mazezeta kwa kushindwa kutumia bandari kuinua uchumi wa mtu mmoja na nchi kwa ujumla?
Kuna Mengi nyuma ya Pazia. St. Joseph huenda ikabomewa miaka ya mbeleni ili kupisha uwekezaji. Hasa mwekezaji Mwarabu.
 
Ni kweli kabisa DP World wamejenga bandari kavu Rwanda na nimefika pale.
Mbona hilo Ni godauni dogo sana Kama la Costco Na IKEA ... Hilo ndio limemshindwa serikali yetu? Ajabu sana hii...acheni kushabikia haya mambo - iambieni serikali ijenge hiyo dry port kubwa popote Tanzania halafu inunue ma craine ya upakuaji - sio kila kitu tunashindwa- sasa tunaweza nini Kama hata hizi storage facilities zinatusginda?!
 
Katika hili wala hauhitaji kujua aliye nyuma ya hawa DP World ni nani, haijatokea kwa bahati mbaya, hakuna coincidence hapa, ni mipango iliyopangwa ikapangika na sasa tunaenda kupigwa mchana kweupeee.

==========================

TAARIFA KUHUSU UWEKEZAJI UNAOPENDEKEZWA NA DP WORLD TANZANIA

DP World imejenga kituo cha hadhi ya kimataifa cha bandari kavu na kitovu cha usafirishaji katika Rwanda, ambayo ni ndogo kijiografia na isiyo na bahari yenye uwezo wa kuhifadhi makontena 50,000 kwa wakati mmoja. Kinyume chake, bandari ya Dar es Salaam katika Tanzania kubwa kijiografia ina uwezo wa kuhifadhi kontena 19,000 TU kwa wakati mmoja.

Hii ina maana kwamba kama meli kubwa ya kontena yenye uwezo wa kubeba takriban TEU 20,000 au zaidi ingetia nanga Dar es Salaam, kituo kidogo cha kontena cha bandarini hakingeweza kuhifadhi shehena ya meli moja tu.

Wakati mjadala wa kitaifa wenye SIASA NYINGI ukiendelea kuhusu masharti ya uwekezaji ujao wa DP World nchini Tanzania, bandari ya Dar es Salaam bado ina uhitaji mkubwa wa uwekezaji wa miundombinu. Wakati huo huo, Rwanda tayari imejenga bandari kavu ya hadhi ya kimataifa, na nchi jirani ya Kenya inatafuta wawekezaji wa kibinafsi kuendesha sehemu muhimu za bandari zake za Lamu na Mombasa.

Ingawa hoja halali kuhusu masharti ya uwekezaji inapaswa kushughulikiwa, ni wakati sasa kwa Tanzania kujadiliana na DP World kwa kina kwani bandari ya Dar es Salaam itakuwa kama njia tuu ya kupeleka shehena Rwanda. Hii ina maana Rwanda itakuwa inapata faida kubwa kupitia bandari yetu kulinganisha na sisi.
View attachment 2656852

View attachment 2656853

View attachment 2656854

View attachment 2656854

View attachment 2656855
Sijaelewa kitu,DP wamejenga bandsri kavu Rwanda,sasa hv wanawekeza bongo,mzigo uingie,Dar harafu usafilishwe kupelekwa Rwanda wakati ni mzigo wa Msumbiji?kwa vile TU Rwanda kuna storage kubwa?hii Haina mantiki!!
Sie tuna bandari kavu kibao,
Dodoma,Dar,Isaka,Sasa how come mzigo wa kwenda kusini upelekwe kuhifadhiwa Kaskazini Rwanda?
 
Ndio maana Kagame alitia timu ghafra tu juzi kati hapo.
 
Kontena Elfu 19 Hadi Elfu 50 hata wanasiasa Wana Ahadi tamu Sana ukiskia utatamani uchaguzi ufike ili impigie kura ....akisha chaguliwa sasa
Kwahiyo hao nao ni wanasiasa na watawala? Hivi mnakuajue watanzania....ujui kua wakishindwa kutimiza matakwa ya mkataba basi wanakua wameshindwa?
 
Na ndio kile kipengele cha kutovunja mkataba hata kitokee nini kinapopigiwa kelele. Ila naomba kuuliza, kwamba uchukue kontena Dar hadi Rwanda halafu ndio upeleke Zambia? Au kontena litike Dar linende kukaa Reanda halafu ndio ulipakie tena kwa mara ya pili kwenda Kongo?
Rwanda hawana bandari.Kweli mwenye akili timamu container zije hapa Dar alafu ziende kuhifadhiwa Rwanda alafu badae zirudi Dar? Next to impossible.
 
Back
Top Bottom