DP World - Rwanda ni kituo kama kama unavyoona ICD zetu hapa Dar... Wanafungua kontena zenye mzigo, wanatoa mzigo wanaweka ndani wanamsubiri mwenyewe aje kuchukua... Wanachowafanyia waagizaji wa Rwanda, mtu akiagiza mzigo , hana haja ya kuja Dar , ataweza kupokea mzigo wako hapo hapo.. Hapa anahudumia end customers ( waagizaji)
Hivyo ni dhana tofauti na uendeshaji wa bandari... Bandari unahudumia kwanza meli zinazotia nanga kwenye bandari husika ( shipping line) na pia halafu unaongeza wigo wa kuhudumia wateja wa nchi nyingine kwa jinsi ambavyo serikali itakubaliana na nchi hizo.. Ambao wanachukua kontena zao , pamoja na meli nyingine kama za nafaka, magari , abiria , mafuta nk.
Kulinganisha bandari ya kavu - DP World Kigali na uendeshaji wa bandari Dar ni vitu tofauti , vyenye operation tofauti kabisa ..
Nilivyosikia waziri , anasema anataka bandari yetu iwe end to end port.. Nilicheka nikaona hata waziri mwenyewe hajui anachosema... Bandari duniani haziwezi kuwa end to end ports - zenyewe ni conduits, ni sehemu ya kupitishia mzigo..
Singapore ambayo ni ya pili duniani kwa shughuli za kontena .... Wao siyo end to end port , wanatumika zaidi kama transhipment port..mizigo au meli zinapitia hapo kwenda Asia , Ulaya, au kuja Africa nk.... Wanapitisha mzigo, hawafungui mzigo..
Sasa Dar port kupitia uwekezaji inaweza kuongeza uwezo wa kuhudumia nchi za jirani, DR Congo, Zambia, Rwanda na Wengine.. Katika hilo hatutakuwa na maajabu sana , kwa vile tutakuwa tunanyang'anyana mizigo na bandari za jirani , katika kuwahudumia nchi ambazo hawana bandari ... Beira, Mombasa, Nacala, Walvis Bay, Durban na wengine na wao watawekeza na kufanya hiki hiki tunachofanya... Hivyo tunaweza kuongeza tija ya bandari ya Dar es Salaam, lakini tusiweke malengo ambayo yatatekelezeki, kwa sababu ya strategic position yetu inatupa wigo mpaka mahali fulani na siyo zaidi.... Bandari za maeneo jirani zitafanana kwa potential market na hata matokeo yake na bandari ya Dar es salaam zinafanya kazi katika soko linalofanana, kwani zinategemea wateja wale wale ..Zitazidiana vitu vidogo vidogo hapa na pale ...