adrenaline
JF-Expert Member
- Jun 17, 2015
- 3,152
- 4,843
Ninachoshangaa Waafrila mtu akiwa na kamgao Yuko tayari kupambana kufa alimradi yeye na familia yake wananufaika. Kama watz wamesema hapana kwanini msisitishe , nguvu kubwa inayotumika ni ya Nini?Mleta mada ahsante sana,mkataba wa DP World na Rwanda hamna tofauti kubwa na huu wa bandari sana labeda katika kuendeleza ndiyo kuna utofauti. Hivi kweli leo hii watanzania tunafikia sehem kukataa uwekezaji ambao unafaida kubwa kwa Taifa letu eti tunakimbia kudanganywa kua bandari inauzwa. Hivi angalia kutoka kontena elfu 19 mpaka kontena elfu 50 mnaona jambo la kawaida. Watu wengi awajui kua mbali na kodi kwa serikali lakini pia bei ya vitu kutoka nje itashuka lakini pia itasaidia ata kusafirisha malighafi na bidhaa nyingine kua rahisi na haraka kwetu.
Bora yako umeona. Kama vile wanaofanya biashara ya Mashuka Tz wanachukulia Uganda landlocked country kwa bei nafuu na wao wanapata faida.Miaka michache tutakuwa tunanunua magari na mizigo mbalimbali na kupitishia Rwanda maana ndiko kutakuwa cheap zaidi..
Punguzeni lawama ndugu ,Tanzania inayo fursa ya kupiga hatua kubwa kwa kuitumia sawasawa Bandari zetu. Serikali yetu imefanya uamuzi sahihi kabisa katika kuweka uwekezaji mkubwa kwenye Bandari yetu.Labda maendeleo ya unguja na pemba
Kwani wanao sema kua serikali iendelee na utaratibu huo wao sio watanzania? Wanaweza wakawa watanzania wengi wanasema hapana kwasababu wamekaririshwa uongo au awajui umuhimu wake. REF. referendum ya 1992 kuhusu vyama vingi,wengi walisema hapana lakini mwisho wa siku wachache wakaibuka washindiNinachoshangaa Waafrila mtu akiwa na kamgao Yuko tayari kupambana kufa alimradi yeye na familia yake wananufaika. Kama watz wamesema hapana kwanini msisitishe , nguvu kubwa inayotumika ni ya Nini?
Unaweza kutusaidia ni wapi imesemekana au imeandikwa kua ni mkataba wa milele? Isije ikawa ni ile nimesikia wanasema...Shida yetu kubwa ni mkataba wa milele, na vipengele vingine lukuki ambavyo havina maslahi Kwa watanganyika
Naona hii itakuwa mahususi kwa ajili ya upande wa DRC Congo na Uganda ambao na wao wanatumia bandari ya Dsm.Na ndio kile kipengele cha kutovunja mkataba hata kitokee nini kinapopigiwa kelele. Ila naomba kuuliza, kwamba uchukue kontena Dar hadi Rwanda halafu ndio upeleke Zambia? Au kontena litike Dar linende kukaa Reanda halafu ndio ulipakie tena kwa mara ya pili kwenda Kongo?
Kagame kafanikiwa kutuingiza box. Kweli huyu jamaa ni akili kubwaKuna mkono wa Kagame kwenye huu mkataba, kumbuka ziara za Samia Rwanda
Yani huyu Kagame ni nyoko aisee!!
Kagame kafanikiwa kutuingiza box na tumejaa. Kweli huyu jamaa ni akili kubwaKuna mkono wa Kagame kwenye huu mkataba, kumbuka ziara za Samia Rwanda
Yani huyu Kagame ni nyoko aisee!!
Umenena !binafsi nafurahi Rwanda ikipiga hatua kimaendeleo kuziona fursa kuzing'amua na kuzichangamkia.
lengo langu labda uwenda majirani wazembe,wala rushwa na wavivu watajifunza kwa huyu jirani yao Rwanda,nchi changa iliyotoka kwenye machafuko lakini kwa muda mchache wanatengeneza nchi yao.
Vitu vinginevyo vinaelezwa humu havina kichwa wala miguu !! 😅Vitu vingine ni uzembe na ujinga tu,hasa bandari kavu hata fundi Maiko anaweza kujenga ukimpa ramani.Pumbaffff eti bandari kavu.
Hushangai hata mashati, viatu na mitumba tunachukua Kampala ambapo hawana bandari ya bahari?....Na ndio kile kipengele cha kutovunja mkataba hata kitokee nini kinapopigiwa kelele. Ila naomba kuuliza, kwamba uchukue kontena Dar hadi Rwanda halafu ndio upeleke Zambia? Au kontena litike Dar linende kukaa Reanda halafu ndio ulipakie tena kwa mara ya pili kwenda Kongo?
Tatizo si ubinafsishaji, DP World, Dubai au ufanisi wa DP World. Tatizo ni jinsi mkataba ulivyo.Katika hili wala hauhitaji kujua aliye nyuma ya hawa DP World ni nani, haijatokea kwa bahati mbaya, hakuna coincidence hapa, ni mipango iliyopangwa ikapangika na sasa tunaenda kupigwa mchana kweupeee.
==========================
TAARIFA KUHUSU UWEKEZAJI UNAOPENDEKEZWA NA DP WORLD TANZANIA
DP World imejenga kituo cha hadhi ya kimataifa cha bandari kavu na kitovu cha usafirishaji katika Rwanda, ambayo ni ndogo kijiografia na isiyo na bahari yenye uwezo wa kuhifadhi makontena 50,000 kwa wakati mmoja. Kinyume chake, bandari ya Dar es Salaam katika Tanzania kubwa kijiografia ina uwezo wa kuhifadhi kontena 19,000 TU kwa wakati mmoja.
Hii ina maana kwamba kama meli kubwa ya kontena yenye uwezo wa kubeba takriban TEU 20,000 au zaidi ingetia nanga Dar es Salaam, kituo kidogo cha kontena cha bandarini hakingeweza kuhifadhi shehena ya meli moja tu.
Wakati mjadala wa kitaifa wenye SIASA NYINGI ukiendelea kuhusu masharti ya uwekezaji ujao wa DP World nchini Tanzania, bandari ya Dar es Salaam bado ina uhitaji mkubwa wa uwekezaji wa miundombinu. Wakati huo huo, Rwanda tayari imejenga bandari kavu ya hadhi ya kimataifa, na nchi jirani ya Kenya inatafuta wawekezaji wa kibinafsi kuendesha sehemu muhimu za bandari zake za Lamu na Mombasa.
Ingawa hoja halali kuhusu masharti ya uwekezaji inapaswa kushughulikiwa, ni wakati sasa kwa Tanzania kujadiliana na DP World kwa kina kwani bandari ya Dar es Salaam itakuwa kama njia tuu ya kupeleka shehena Rwanda. Hii ina maana Rwanda itakuwa inapata faida kubwa kupitia bandari yetu kulinganisha na sisi.
View attachment 2656852
View attachment 2656853
View attachment 2656854
View attachment 2656854
View attachment 2656855