DP World wawepo Uingereza kwa wanaojitambua halafu Waswahili wa Tanzania tuikatae?

Tanzania ina watu wajinga sijapata kuona hao UK nao wanaanza kwenda kuwakagua Dubai ndio wanawapa kama UK walishamaliza mambo ya kuwa na mikataba sahihi kwa manufaa ya Wananchi wao sio matumbo yao hao DP World ni kampuni kubwa kweli ila zipo sehemu wanashindwa Tender na kampuni zingine bora zaidi hapo kwa Madiba wana dry port Komatiport ambayo wamepewa eneo kwa ajili ya mizigo ya bandari ya Msumbiji ila walishindwa Tender ya Bandari ya Durban na Bandari ya Eastern Cape na kumbuka wana ofisi muda mrefu hapo Durban ila Transnet walitangaza kwa Tender Makampuni zaidi ya 15 yakaomba ilikua 2021 mwishoni mpaka leo 2023 June ni kampuni 4 ndio zimechujwa na hapo inatakiwa kampuni moja ili Bunge leo liidhinishe baada ya Wataalamu wa Transnet na maswala ya Bandari kuelezea...hakuna Msauzi alieenda sijui China,Uholanzi kuangalia ubora wa hizo Kampuni kama tulivyofanya hapa kwetu wasafirishaji wakina Msukuma waende Docks ambako hata hawajui vinafanyikaje vitu na kuachwa Wataalamu kwenye maswala ya Bandari...Nchi hii ina safari ndefu sana kwa kuwa haina Wazalendo wa kweli kwenye Mali zao.
 
Umewasahau wafuasi wa Jiwe
 
Huku kuna ports 51 na zinaingiza mkwanja na 2 za DP pamoja na rail
Ni kampuni inayomilikiwa na Royal family
Acha waingie tu
 
Inaonekana uelewa wako ni kama wa makanjanja wa kule mjengoni waliomezeshwa maneno, unadhani masharti ya mkataba waliosaini UK yanalingana na masharti tuliyopewa sisi? Tunacho pigia kelele hapa ni masharti ya hivyo ya mkataba wenyewe.
 
Mjadala ufungwe😃
 
Weee vipi? Wee ndo uelewi! Shida sio Dp world! Shida ni mkataba kandamizi na kinyonyaji! Uingereza mkataba wao ni kutanguliza maslahi ya Uingereza kwanza na baadaye mwekezaji! Hapa Bongo kwanza walitanguliza rushwa kwa serikali (SSH), wakaja wabunge, wakaha kwa waandishi wa habari! Baada ya hapo wakapitisha mkataba kandamizi! Hawa viongozi tulionao woote wamehongwa na hawajitambui!
 
Acha kunililia hapa. Mimi sio mzazi wako.
 
Mhhh Genta ni ww kweli umeandika huu uzi au mchepuko wako kadandia simu yako?😳😳😳😳
 
DP World wawepo Uingereza ni sawa na mkataba unafanana na uliopelekwa Dodoma kupitishwa na Joseph Musukuma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…