DP World wawepo Uingereza kwa wanaojitambua halafu Waswahili wa Tanzania tuikatae?

Hata mchina anavyo deal na mzungu ni tofauti na anavyo deal na Mwafrika
Hata bidhaa anatengeneza kwa ajiri ya Ulaya ni tofauti na inayokuja Africa

Wanajua viongozi wetu Africa wanafikiri kwa kutumia cauda equina
 
Mm mdau wa PPP napenda uwekezaji kwenye sekta nyingi za Serikali ili kutoa nafasi ya huduma za ushindani na kuamsha Ari ya utendaji kwenye sekta husika lkn tukisema DP world kuwa Uingereza ni kigezo cha sisi pia kuwakubali hiyo ni hapana, mkataba na makubaliano ya DP world vs Uingereza na DP world vs Tanzania obvious ni tofauti kabisa! Kinacho takiwa kuangaliwa ni makubaliano pekee na nchi husika, tukija upande wa pili kwenye mifano ya nchi DP world wana oparate mfano tukitumia Mfano wa Djibouti na nchi nyingine zenye case mahakamani na DP world tunaweza sema pia DP world haifai, lkn tukienda deep kwenye makubaliano yao utakuta labda mkataba walioingia akina Djibouti ndio unawabana.
 
Hakuna uzi murua kama huu!

Imagine
Watu wanalia TOZO.

Solution ya Tozo ni kuondoa ule ujinga unaifanyika pale Bandarini!

Hapa TRA wajipange tu vizuri kwa kufanya moderation ya kodi kwa baadhi ya Bidhaa kwa Sababu DP wao hawakutani na Mtu.

Ni Mashine tu inascan na kukutolea Assessment kule!

Sasa kuna kitu kimoja watu hawakijua.

Serikali ikiwa na uwezo wa kukusanya Mapato makubwa na kuweza kutoa huduma zote muhimu kwa watu wake ndipo sasa UZALENDO UNAKUWA DHAHIRI kwa Sababu kila mtu atapenda kulinda maslahi ya Nchi isishindwe kuhudumia wananchi wake vizuri kama ambavyo imeweza!

Saa hizi unakuta kuna ujinga mwiiingi kule Bandarini na watu wachache wanaweza kununua vigari viwili vitatu halafu tunasema acha vijana wetu wapate kazi huko Bandarini!

Hakuna!

Tumeambiwa Bandari inapaswa kutuingizia Trillion 2 kwa Mwezi -ikiwa Bandari pekee itatupa iyo 2T maana yake tutafika 4T...sasa Kuna kitu gani tutashindwa kama Nchi?

Huu Mradi na uje hata kesho!!
 
Bado na ww mjnga tu,mashaka yote yapo kwenye mkataba au tuongeze sauti.
 
Elimu elimu elimu.masharti ya mkataba wa uingereza na tz ni tofauti
 
Watoto wako wakiiba vijiko ndani unauza nyumba?
 
Wewe ni mjinga huniambii akili zako zinaishia uko porini


Hujui hawa majangili ya kiarabu yamesitishiwa mikataba nchi nyingi kwa ufisadi na kufanya ujangili

Watanganyika wengi mna low iq ndio maana mnatawaliwa na watu wenye uwezo mdogo
Sawa Juha.
 
Watoto wako wakiiba vijiko ndani unauza nyumba?
hatuuzi, tunabinafshisha uendeshaji. cha muhimu mswahili asikae pale , ukimuona kafunga tai , utadhani utendaji wa maana, hamana kitu, wizi mtupu
 
Thinking Kubwa kama hi yako kamwe usitegemee Lumpen Proletariat kama uwe hodari akawa nayo.

Huwa napenda mno Watu Brainiac kama hivi Wewe ambao mkisikia Jambo hamdemki nalo Bali mnalichakata Kifikra zaidi.
 
Thanks for the Credits Chief na nimeuanzisha huu Uzi ili Masikini wa Akili na Kufikiri wanaoongozwa na uwe hodari nao wawe na Utajiri wa Akili na Maarifa kama tulionao Wengine.
 
watu wengi wanaopinga ubinafsishaji , ni watu ambao hawajui fedha zinavyoibiwa katika mashirika ya umma.
Pesa inaibiwa kila mwaka mawizarani, tubinafsishe wizara zote na Ikulu kuzuia wizi?
 
DP WORLD watu wanashindwa kuelewa kua huyo ni mwingereza kwa mgongo wa hao waraabu wa hapo Dubai.
 
Kumbuka bongolala na check & balance yake😂
 
Ujinga ujinga tu watu hawakatai wawekezaji kisichotakiwa ni aina ya uwekezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…