DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Watanganyika wamekataa huu mpango ,mpeni hata mzawa itakua safi sana
Walishapewa na ufanisi ukawa ziro na kufuja kwa fujo.
Uzawa hauna maana kiuchumi kama hauleti tija na inakuwa shamba la bibi.Treni hiyo imeshatoka stesheni endeleeni kuota.
 
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kampuni ya DP World ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeanza kushusha vifaa katika Bandari ya Dar es Salaam kuanza uwekezaji.

Aidha, TPA imebainisha kuwa makabidhiano ni tangu Aprili 7, mwaka huu bila kuathiri uendeshaji wa bandari hiyo. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alisema hayo Dodoma akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa katika Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Mrisho alisema DP World ambao wataendesha gati namba moja hadi saba, wameshusha meli nzima yenye vifaa vya kisasa ikiwamo mashine nane za RTG, mashine nyingine 19 za kushusha kontena, jenereta kubwa za kuendesha mashine hizo na mashine nyingine nne ziko njiani.

Haki sawa kwa woteeee!!!
Mimi na timu yangu tumetumwa na Mheshimiwa Raisi wa Tanganyika huku Saudi Arabia kuingia mkataba kati ya bandari ya Zanzibar na kampuni iitwayo kanjanja port limited ya hapa Saudia!!
 
Endelea kuota. Angalizo usijinyee tafadhali.
 
Wananchi wangapi?Una interest na Bandari na mkate umemwagiwa mchanga?Kelele zako binafsi hazisaidii chochote na kama mkataba umekupa tabu sana nenda kwa Mangi nunua kamba cha kufanya unajua. Mimi nitalipia hiyo kamba.
Hiyo treni imeshaondoka stesheni ndio sababu nikakuuliza bandari gani?Endelea kupiga domo.
Umeumia sana. Pole. Jikite kwenye mada. Treni mwisho wake ni kuwa dodo ndio litakuwa na mchanga🤔.

Kamsikilize Tundu Lissu ukalale.
Aisee, hasira za nini bwasheee😂😂😂😂
 
Ukweli ni kwamba Vifaa hivyo vimelipiwa na Serikali yetu-Fedha zetu. Watanzania.
Si wewe ulikuwa unaulizia kama vimelipiwa kodi?Njaa inasababisha usahaulifu.
Serikali yenu ipi?Chadema mna Serikali?Wacha kujitia ukichaa kwa kuingiza ulimi puani.
 
Chadema wamewanywesha kangara hata tafakari hamna tena!, kila jambo ni kulaumu kwa uchungu tu,bila akili.
::Tunataka kuona tija ya maboresho haya, kama taifa.
Bandari yetu ikiweza kushusha mzigo kwa siku Moja hayo ni maendeleo makubwa na labda mizigo ya nchi jirani itaongezeka sana ishu kubwa itabaki sisi tunapata mgao kiasi gani na DP wanapata ngapi na kwa muda gani watakaa nasi
 
Si wewe ulikuwa unaulizia kama vimelipiwa kodi?
Kununua Vifaa na kulipa kodi ni vitu viwili tofauti. Na hata kwenye utaratibu wa Serikali kununua Vifaa, ni lazima mchakato huo uhusishe na Ushuru na forodha-hata kama watajisamehe kodi.

Ndio Nimeuliza kama shehena zilizofika na meli tajwa Vimelipiwa kodi. Kinachokuuma ni nini?
Njaa inasababisha usahaulifu.
Serikali yenu ipi?
Serikali. Ni ya Baba yako?
Chadema mna Serikali?Wacha kujitia ukichaa kwa kuingiza ulimi puani.
Unaongea vitu ambavyo haviwezekani-Mimi ni CCM, I bleed green. 👃🏾👅😂😂😂😂😂🙌🏾
 
Amewagawia mashoga zake wa Dubai in Lissu's voice
😂😂😂😂😂

Mpaka hapa tulipofika, wanasema akemewe, atengwe walakin hakuna anayesema, amesema uwongo!

Pamoja na Yote, kwa suala hili wacha Lissu atumbue jipu tu.
 
Walisema 3 mpaka 7 Leo washaongeza ghafra bila taarifa?
 
Mbona hatujaona hafla ya makabidhiano?

Yaani tupokee ndege kwa hafla na live coverage afu DP wedi wapewe kimya kimya. Hii sio sawa.

Tunaomba irudiwe, ili mafanikio yakiuoneka historia ituoneshe. Kinyume chake pia.
 
😁 Kwenye hili atanisamehe tu. Hii "Transparency" waliotuuzia, waanze kuionyesha kwenye Meli iliyoingia na shehena zake.
Mkuu nipe email yako nikutumie clip niliyoirekodi kwa simu yangu ikionesha meli iliyobeba baadhi ya mashine kazi za pale Bandarini ikiwasili. Ilikuwa ni three weeks ago.
Tatizo wabongo hamtaki kufatilia vitu ila mnajikuta wajuaji. Mpaka sasa watumishi 253 kutoka TPA wamehamia DPW na mshahara wa mwezi wa nne wamelipwa na DPW.
KARIBU.
 
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kampuni ya DP World ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imeanza kushusha vifaa katika Bandari ya Dar es Salaam kuanza uwekezaji.

Aidha, TPA imebainisha kuwa makabidhiano ni tangu Aprili 7, mwaka huu bila kuathiri uendeshaji wa bandari hiyo. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho alisema hayo Dodoma akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa katika Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Mrisho alisema DP World ambao wataendesha gati namba moja hadi saba, wameshusha meli nzima yenye vifaa vya kisasa ikiwamo mashine nane za RTG, mashine nyingine 19 za kushusha kontena, jenereta kubwa za kuendesha mashine hizo na mashine nyingine nne ziko njiani.

Ilikua ni gati mbili tu sasa tunaambiwa ni gati namba 1 hadi 7. sasa hapo wamebakiza nini. Sisi tunasema wanamapinduzi wakirejea kwenye kuongoza nchi tutaitosa DP maana ni mchongo wa vigogo na ni ukoloni mtupu. Tunaju ujio wa DP ni kama ule wa loliondo. Waarabu wanakuja kutubia na kuvuruga nchi yetu kwa kuwahonga viongozi. Ukiangalia loliondo hujui nini nchi inapata wala kitalu hua hakitangazwi tenda muda ukifika. Wanacorrupt jamii yetu tu.
 
Mkuu nipe email yako nikutumie clip niliyoirekodi kwa simu yangu ikionesha meli iliyobeba baadhi ya mashine kazi za pale Bandarini ikiwasili. Ilikuwa ni three weeks ago.
Tatizo wabongo hamtaki kufatilia vitu ila mnajikuta wajuaji. Mpaka sasa watumishi 253 kutoka TPA wamehamia DPW na mshahara wa mwezi wa nne wamelipwa na DPW.
KARIBU.
Mshahara unabadilika au ule ule?
 
Ilikua ni gati mbili tu sasa tunaambiwa ni gati namba 1 hadi 7. sasa hapo wamebakiza nini. Sisi tunasema wanamapinduzi wakirejea kwenye kuongoza nchi tutaitosa DP maana ni mchongo wa vigogo na ni ukoloni mtupu. Tunaju ujio wa DP ni kama ule wa loliondo. Waarabu wanakuja kutubia na kuvuruga nchi yetu kwa kuwahonga viongozi. Ukiangalia loliondo hujui nini nchi inapata wala kitalu hua hakitangazwi tenda muda ukifika. Wanacorrupt jamii yetu tu.
Endelea na ndoto zako na so called wanamapinduzi wa kwenye njonzi.Angalizo chunga usijinyee.
 
Ccm wamekubali kwamba DP World wana akili kuwazidi wao wote pamoja na mwenyekiti wao. Kama DP World wanaweza kuendesha bandari kwa ufanisi kwanini serikali ya ccm isiweze? Hawastahili kuwepo madarakani kabisa.

Imagine, kanchi ka watu 2 million ambacho kanategemea human resources za nchi nyingine kujiendesha leo ndiko anakuja kutuendesha sisi million 64.

Hawa maCCM ni bure kabisa.
 
Back
Top Bottom