DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

msiwatishe waache wajiunge na mwarabu waachane na upuuzi wa kikokotoo, kama mwarabu anaboresha maslahi kwa asilimia 60 juu ya wanachopata Mungu awape nini tena? wakimbilie kwa mwarabu nchi imeshauzwa hiyo wanaojifanya kukomaa peleka nyasa huko na mwanza.
 
Uyasemayo ni kweli tupu wafanyakazi wa tpa shuhuli hawana tena pale
 
Mbona ujataja Berth Zero - Kwa ajili ya magari. Hii pia imeenda 😀
Halafu unavyosema vifaa vya kisasa...umeona tafauti yake na vifaa vilivyopo?
 
mbona dawa ni ndogo tu kama ameichukua jumla, kuitafuta Tanganyika hadi ipatikane, halafu mwarabu ataitafuta Tanzania aliyoingia nayo mkataba, atembee kwa mguu hadi dubai juu ya maji (kidding), though kama anaongeza maslahi na kama ataongeza kweli ufanisi, ngoja tumwangalie anachofanya, aifanye bora kama zile za dubai hapo labda tutamsamehe.
 
Kuna jamaa yangu yupo bandari, anasema mwarabu yupo serious, malipo mazuri, ila hataki masihara kazini, mixer msosi kazini, utendaji wa kazi upo systematic sio awali walikuwa wanajifanyia fanyia tu.
Kwa manufaa ya vizazi vyetu vijavyo naunga mkono sekta nyingi tu zibinafisishwe ili kizazi kijacho kiadopt utendaji kazi wa wenzetu sio huu ujinga wa kiafrica uliopo sasa
 
Soon or later its inevitable litapita fagio la Chuma..., Automation haiitaji manpower kubwa...; Cha kujiuliza sisi hizo Automation tunashindwa kuzifanya hadi aje aziweke mwingine ? Usiniambie mbona hata UK amefanya nitakuuliza huyo UK ana un-employment kama yetu ?

 
Mzanzibari kutengeneza chawa wa kitanganyika ili kuuza Tanganyika kwa wajomba zake. Tuamke wenye akili zetu timamu tuikomboe tena Tanganyika yetu
 
Ni muda tu utasema Mzee nakuhakikishia kuna watu wamekaa kimya ngoja washike madaraka utakuja kuniambia
 
Hapo kwenye mkataba wa awali ndio kwenye mtego.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…