DPP na DCI waweka mapingamizi manne kufunguliwa kesi ya Makonda. Wasema Kubenea hana maslahi na maombi hayo

DPP na DCI waweka mapingamizi manne kufunguliwa kesi ya Makonda. Wasema Kubenea hana maslahi na maombi hayo

Kwanza Kubenea ni mwandishi wa habari hivyo ana maslahi na hiyo kesi ila Kwa nini Clouds wenye maslahi na hiyo kesi hawajafungua kesi mpaka sasa?

Hawajitambui kabisa.

Yani mtu mwingine anakutetea wewe unasema Sina shida.
 
Kushambulia media moja au mtangazaji mmoja ni kuitia hofu tasnia nzima ya uandishi wa habari isiweze kufanya kazi zake kwa uhuru na weledi unaotakiwa.

Hujawahi kusikia waandishi wanagoma kutoa habari za viongozi kwa sababu mwenzao mmoja amekamatwa?
Locus standi

Ni ile hali ya kuonesha Wewe umeathirika au una faida gani au hasara gani unapata kutokana na tukio lililetwa au kukusudiwa kuletwa Mahakamani

Mf. Mimi Pohamba sina Maslahi kwny Kesi ya mgogoro wa KKKT kule Mbeya hivyo kwa namna yeyote ile sina maslahi kwny kesi zinazohusu tukio lile
 
Kushambulia media moja au mtangazaji mmoja ni kuitia hofu tasnia nzima ya uandishi wa habari isiweze kufanya kazi zake kwa uhuru na weledi unaotakiwa.

Hujawahi kusikia waandishi wanagoma kutoa habari za viongozi kwa sababu mwenzao mmoja amekamatwa?
Toka mwanzo niliona kubenea atagonga mwamba kwa kuwa serikali haina nia na bashite.

Bashite bado ni untouchable na hapo sasa hivi Kuna kazi kapewa humohumo jikoni.

Bashite ana nyota Kali sana huyo, alilindwa na awamu ya 4, akalindwa na awamu ya 5 na Sasa analindwa na awamu ya 6.
 
Wamwache akajitetee kama wengine, sheria za kipuuzi sana DPP kupinga mtu kufunguliwa mashtaka, gharama zao wenyewe acha wasikilizwe na mahakama huru, DPP mtu wa ovyo sana kaamua kuwa kada wa CCM kutetea wahuni
 
Unamuonea tu DPP, yeye anafata maagizo tu
 
Mapingamizi mepesi sana ! nadhani wameamua kumkaanga lakini wanataka ionekane wamejitahidi kumuokoa .
 
DPP na DCI wameweka mapingamizi manne katika maombi yaliyofunguliwa na Saed Kubenea, kupata kibali cha kumfungulia kesi ya matumizi mabaya ya madaraka, aliyekuwa RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mapingamizi hayo ni, Kubenea kutokuwa na maslahi na maombi hayo.

Pia soma
Mapingamizi hayo ni, Kubenea kutokuwa na maslahi na maombi hayo.[emoji3064][emoji15][emoji3064][emoji2827]
 
Kutokuwa na maslahi maana yake nini?

Kwani Kubenea ndiye DPP?

Kwani yeye ndie mmiliki wa Clouds360 Iliyovamiwa?

Kwani makonda ndie alilifungia mwanahalisi na Mawio magazeti ya Kubenea?

Je!
makonda ndie alimkamata Kubenea kule Namanga mpakani akitokea kenya na kile kiasi cha pesa alichoshindwa kukitolea maagizo?

Lakini pia nauliza!
Hivi enzi za Kikwete wakati Kubenea akimwagiwa Tindikali.
makonda alikuwa amekwishaingia Dar es salaam?

Je makonda ndie alimrekodi Kubenea na Komu wakimteta Mbowe?

Khe!
commonmwananchi
10101.
2022.
 
Kwanza Kubenea ni mwandishi wa habari hivyo ana maslahi na hiyo kesi ila Kwa nini Clouds wenye maslahi na hiyo kesi hawajafungua kesi mpaka sasa?
Clouds hawana USAFI wa kumshtaki Makonda, wanajuana UCHAFU wao.

Rejea kauli ya RC kwamba yeye ndiyo kaipa Clouds 'uhai' kwa kuipa tenders za Serikali.

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
DCI na DPP wanajua wazi kwamba Makonda kwa sehemu kubwa acted on behalf of JIWE, wakiruhusu kesi basi kuna mengi yataibuka na itakuwa fedheha kwa Serikali na baadhi ya 'Big fishes'.

Tazama Sabaya, alipoona hana upenyo wa kuchomoka aliona awataje Rais, Makamu na baadhi ya top officials kwamba they knew his moves na zilipata baraka toka kwao!

Sasa DC tu alitaja yale, vipi kuhusu RC ambaye we all knew alikuwa ndiyo 'mkono wa kiume' wa JIWE! Makonda akiachwa ashtakiwe kuna mengi yatakuwa exposed.

DCI na DPP wamefanya a well calculated decision.

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
DPP na DCI wameweka mapingamizi manne katika maombi yaliyofunguliwa na Saed Kubenea, kupata kibali cha kumfungulia kesi ya matumizi mabaya ya madaraka, aliyekuwa RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mapingamizi hayo ni, Kubenea kutokuwa na maslahi na maombi hayo.

Pia soma
Hilo ni pingamizi mbuzi, litapanguliwa kirahisi sana na upande wa Kubenea.

Katiba ya JMT ndiyo inampa masilahi Kubenea
 
Mkuu kama kweli yeye ni untouchable vipi watu wa USA walimpiga biti asiende kwao?
Anazungumzia hapa Tanzania, wahindi ambao untouchable India yaani hawaruhusiwi kuwasogelea waliobarikiwa na mungu hapa Tanzania ndio magabacholi!
 
Back
Top Bottom