Watanzania tukifanikish ku sitisha ili swala la bandari, mwendo ni ule ule kwenye mikataba mingine kama ya Loliondo mpaka Tanzania irudi maana we have nothing to expect from politicians. Wanasiasa wamefornn coalition against citizens, na sisi we stand against them. Tanzania ni ya watanzania na siyo ya Wanasiasa.
View attachment 2676765
Japo tunayasema yasiyo sahihi mitandaoni dhidi ya Watawala na tuliowachagua wakapuuza, wajue kwamba tunaishi nao mitaani. Kwa karne hii ya TAHEMA, wakikosa madaraka yao ya kisiasa, watatukuta mitaani kama Wahenga walivyonena
mpanda ngazi hushuka au
aliye juu mngoje chini. Siyo dua la kuku kwani kuna ushahidi wa waliokuwa na madaraka tunao mitaani tunaona maisha yao, labda wachache wanaolindwa na Katiba.
Hatujasahau wala hatusahau
[emoji830]︎ ubadhirifu wa mali ya umma, ulioripotiwa na CAG;
[emoji830]︎ matumizi ya hovyo ya kodi zetu, misaada na mikopo;
[emoji830]︎ usimamizi dhaifu wa rasimali za Taifa;
[emoji830]︎ urasimu na uzembe katika maofisi ya umma;
[emoji830]︎ na kadhalika
Tunachohitaji ni Wanasiasa tuliowapa dhamana ya madaraka na mamlaka, kikatiba, kutimiza wajibu wao kama ulivyoanianishwa kwenye Katiba, na siyo kuyatumia kwa maslahi yao binafsi.
Wenye madaraka na mamlaka ya kikatiba, wakumbuke kuwa japo wengine, kwa Katiba ya sasa wanaendelea kulindwa, kana kwamba bado wako madaraka, ninaamini Katiba mpya itawaondolea tupambane nao mitaani kunako huduma hafifu za jamii, miundombinu isiyoridhisha, mlolongo wa tozo, na kero lukuki za maendeleo.
KAZI IENDELEE na Kuupiga mwingi