Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Alichokisema Diallo ni kweli ila kuna watu hawataamini. Marehemu hakuwa sawasawa wakati wote. Kuna wakati, mara kadhaa alionekana yupo kwenye shida ya magonjwa ya akili, japo wengine wanaweza kuchukulia ni dhihaka.
Ni sawa na Lissu, nae hayupo sawa sema watu hawalioni hilo ila toka lile shambulizi Lissu hayupo sawa.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dr Anthony Diallo amesema ni makosa makubwa na hatari sana kuwaachia wanasiasa watengeneze katiba ya nchi.

Diallo amesema wanasiasa ni wabinafsi hivyo lazima wajipendelee ndio maana katiba ni lazima itengenezwe na wananchi wakisaidiwa na wataalamu kama ilivyofanyika nchini Kenya.

Diallo yuko mubashara Star tv akihojiwa na Aloyce Nyanda.
Nakubaliana na Dr Diallo huwezi kupata katiba kwa kuwategemea wanasiasa kuongoza mchakato.Viongozi wa dini, NGO, wana academia na makundi mengine inawezekana.wana academia wanaweza kuongoza.
 
Diallo ametema nyongo ya madhila tuliyopata katika awamu ya Magufuli! Amesema kamwe tusije rudia kuchagua mtu ambaye hatuna historia yake!

Diallo ameonyesha wazi hata ndani ya CCM Magufuli hakukubalika bali ni mabavu tu yaliendelea kumweka madarakani

Diallo kupitia kampuni yake ya Sahara Media group bado anaidai CCM fedha nyingi kutokana na matangazo ya kampeni ya mwaka 2015. Pamoja na kuisaidia CCM katika kampeni lakini Magufuli aliamua kuifungia kwa muda na kuinyima matangazo ya biashara kutoka serikalini na hivyo kusababisha kuyumba kiuchumi hadi kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara yao.

Aidha Diallo ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza amedai alionja joto la jiwe la Magufuli hivyo amewaasa viongozi kuwa na busara. Amedai kuwa enzi za Magufuli viongozi walilewa madaraka.

Kwa kifupi Diallo amewaasa viongozi kutii sheria na katiba.
 
Nasubiri kauli ya katibu mwenezi akimponda Diallo.Kijana hapendi ukweli,Nyanda huo mjadala urushe kama ulivyo unaondoa unafiki wa CCM.
KONGWA mawasiliano ni shida,tusaidiane ujumbe ufike.
Utawekwa hapa, ni mjadala muhimu sana!
 
Yale yale. CCM wanachomoa kwa kuwasingizia wanasiasa.
CCM ni chama cha kisiasa, na hivyo hawawezi kujitoa kuwa hawana wanasiasa kama sio wana asa wa mchakato wa Katiba.
Asitulaghai, na wala tusiiache CCM kulaghai. Nani walizunguka nchi nzima? Nani alianzisha kamisheni na mpaka bunge maalum?
Kitaeleweka
 
Diallo ametema nyongo ya madhila tuliyopata katika awamu ya Magufuli! Amesema kamwe tusije rudia kuchagua mtu ambaye hatuna historia yake!

Diallo ameonyesha wazi hata ndani ya CCM Magufuli hakukubalika bali ni mabavu tu yaliendelea kumweka madarakani

Diallo kupitia kampuni yake ya Sahara Media group bado anaidai CCM fedha nyingi kutokana na matangazo ya kampeni ya mwaka 2015. Pamoja na kuisaidia CCM katika kampeni lakini Magufuli aliamua kuifungia kwa muda na kuinyima matangazo ya biashara kutoka serikalini na hivyo kusababisha kuyumba kiuchumi hadi kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara yao.

Aidha Diallo ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza amedai alionja joto la jiwe la Magufuli hivyo amewaasa viongozi kuwa na busara. Amedai kuwa enzi za Magufuli viongozi walilewa madaraka.

Kwa kifupi Diallo amewaasa viongozi kutii sheria na katiba.
Lazima Diallo ataitwa kwenye kamati ya maadili ya chama kama Kinana!
 
Ameongeza kwa kusema nchi imepita kwenye kiza kinene ktk kipindi cha miaka 5. Rais wa awamu hiyo hakuheshimu utu, haki na alivunja katiba wazi wazi.

Anaomba tuwe tunarejea histori za wagombea kabla ya kuwapa urais. Kamwe tusirejee tuliyoyapitia.

View attachment 1847668
Daah mzee kaongea ponti sana hapa! Ujumbe huu aupate mama wa 'chokochoko'! Asithubutu kuturudisha huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima aseme mana pamoja aliibeba ccm kwenye kampeni 2015 ,chuma kilimwambia lazima ulipe kodi

Alale mahali pema yule mwandishi alikufa baada yakukosa ada yachuo kwamtoto kisa sahara media uwezo wakulipa mishahara hakuna magufuli anahtaji kodi
 
Vipi bado inaendelea kuonyeshwa?
 
Ameongeza kwa kusema nchi imepita kwenye kiza kinene ktk kipindi cha miaka 5. Rais wa awamu hiyo hakuheshimu utu, haki na alivunja katiba wazi wazi.

Anaomba tuwe tunarejea histori za wagombea kabla ya kuwapa urais. Kamwe tusirejee tuliyoyapitia.

View attachment 1847668
Mara ya mwisho nikiwa bwiru boys alikuja kutuhonga tukampigie kula jamaa

Nakumbuka alinipa elfu 5 na sikupiga kura
 
Ameongeza kwa kusema nchi imepita kwenye kiza kinene ktk kipindi cha miaka 5. Rais wa awamu hiyo hakuheshimu utu, haki na alivunja katiba wazi wazi.

Anaomba tuwe tunarejea histori za wagombea kabla ya kuwapa urais. Kamwe tusirejee tuliyoyapitia.

View attachment 1847668
Duuh kweli haya mkuu?
 
Kwa hiyo tuendelee kushehelekea?
 
Back
Top Bottom