Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Diallo ametema nyongo ya madhila tuliyopata katika awamu ya Magufuli! Amesema kamwe tusije rudia kuchagua mtu ambaye hatuna historia yake!

Diallo ameonyesha wazi hata ndani ya CCM Magufuli hakukubalika bali ni mabavu tu yaliendelea kumweka madarakani

Diallo kupitia kampuni yake ya Sahara Media group bado anaidai CCM fedha nyingi kutokana na matangazo ya kampeni ya mwaka 2015. Pamoja na kuisaidia CCM katika kampeni lakini Magufuli aliamua kuifungia kwa muda na kuinyima matangazo ya biashara kutoka serikalini na hivyo kusababisha kuyumba kiuchumi hadi kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara yao.

Aidha Diallo ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza amedai alionja joto la jiwe la Magufuli hivyo amewaasa viongozi kuwa na busara. Amedai kuwa enzi za Magufuli viongozi walilewa madaraka.

Kwa kifupi Diallo amewaasa viongozi kutii sheria na katiba.
Mbona hakupiga kura ya hapana 2020 kwenye mkutano Mkuu wa kumpitisha JPM, hansadi yao inaonesha alishinda kwa asilimia mia moja kabisa.

Huo ni unafiki wa Diallo,na top up huyo ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. na MNEC.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Ameongeza kwa kusema nchi imepita kwenye kiza kinene ktk kipindi cha miaka 5. Rais wa awamu hiyo hakuheshimu utu, haki na alivunja katiba wazi wazi.

Anaomba tuwe tunarejea histori za wagombea kabla ya kuwapa urais. Kamwe tusirejee tuliyoyapitia.

View attachment 1847668
Jizi kama hili nani analitaka..mkwepa kodi mpuuzi kabisaa..walifungiwa na TRA kwa kutokulipa kodi wafanyazi wengi wa star tv wakahama pale wengine walikuwa wanajitolea kufanya kazi.

Hebu nyie nyamazeni jpm alipambana na majitu ya ajabu..sanaaa..walikomeshwaa sasa hv yanarudi kwa kasi kama hawa kina sexless..watu waliofukuzwaa kwa kuwa na vyeti feki na wauza ngadaaa.

Note this..it will take more than a century to have someone like jpm...
 
Haya sasa Dialo mbunge wa mwanza vijijini kisha ilemela kama jimbo jipya kaamua kujilipua si mnakumbuka star TV ilivyo zungukwa na na TRA yakidai kodi kwa marungu sili yenu
 
Mkuu unaweza kunisaidia kujua ni kwanini Antony Dialo alipokuwa akilalamika Kutumika na Kudhulumiwa Pesa zake hadi leo akasema amemuachia Mwenyezi Mungu na akawa anacheka?

Halafu mbona tokeo Oktoba 25 mwaka 2015 hadi Machi 17 mwaka 2021 alikuwa 'amekondeana' sana hata Nuru yake Kupotea ila kwa sasa imerudi ghafla halafu anaonekana Mchangamfu na mwenye Furaha?

Nasubiri Majibu yako kwa hamu mno tu.
 
Mara ya mwisho nikiwa bwiru boys alikuja kutuhonga tukampigie kula jamaa

Nakumbuka alinipa elfu 5 na sikupiga kula

Mwizi mkubwa jamaa Ilemela mpaka Leo Igombe na Kayenze hakuna barabara ya lami pamoja na kuwa jiji na uchumi mkubwa wa samaki

Ila tulimkomesha mwaka huo hatokaa asahau!
Wasongolist wa BBTSS mko humu...,mara ya mwisho kumuona anaongea ugolo alikujaga pale kwenye viti akiwa NW sijui wa biashara ama utalii maliasili...kifupi kayumba Diallo hajui hata history ya katiba ya JMT anasema Lancaster, anasema kuwa katiba ya JMT ilifanywa na wananchi sio wanasiasa na sasa wanasiasa wasiingilie mchakato

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mara ya mwisho nikiwa bwiru boys alikuja kutuhonga tukampigie kula jamaa

Nakumbuka alinipa elfu 5 na sikupiga kula
Uchaguzi wa 1995 nikiwa Bwiru Boys alipita kiulaini akipata upinzani hafifu toka NCCR Mageuzi mgombea pia alikuwa ni ex-Bwiru Boys
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dr Anthony Diallo amesema ni makosa makubwa na hatari sana kuwaachia wanasiasa watengeneze katiba ya nchi...
Leo kasema ukweli japo naye ni miongoni mwa hao wanasiasa. Kuthibitisha unafiki wa wanasiasa (Hususani Waafrika-wasowazalendo) tujiulize-wajuzi wa mambo haya tusaidieni, maoni ya wananchi ndiyo yaliyopitishwa na bunge LA katiba au yalipingwa chini na kutuletea katiba inojali na kulinda zaidi maslahi ya wanasiasa?
 
Nimefatilia interview ya Diallo, inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiishutumu serikali ya JPM, serikali iliyopambana kwa ajili ya wananchi. Naenda kujibu hoja zake kwa niaba ya JPM. Rais ambaye ntampigania mpaka kufa.


1. Kwanza, naomba ujue kuwa kudhamini chama kwenye kampeni hukulazimishwa, wewe kama mwanachama ni wajibu wako. Hivyo usitegemee hela ya wananchi walala hoi, ndio wakulipe pesa eti ulipigana kunusuru chama kushindwa uchaguzi 2015.

2. Eti chama kiwe kinaangalia mtu kabla ya kumuweka kuwania urais,.

Chama chenu ni cha vichaa kwa sababu mlimchagua kichaa. Ina maana hamukuona wengine mpaka mkamuona JPM? Ukweli utabakia kuwa ukweli tu, chama chenu kilikuwa kimeoza. Wananchi tuliwachoka, mlikuwa mafisadi, walafi, wezi, mlikuwa mnanuka. Mkaona mmutumie JPM ili awasafishe maana yeye alikuwa ni msafi.

Mlitegemea JPM atapotoka, na mtamuendesha...ila mligonga mwamba!

Mlitegemea atawasamehe kodi mnazodaiwa ..mabilioni ya pesa...mlitegemea atawaachia mianya muibie chama na serikali.


Eti alikuwa na ulinzi uliotisha? Hivi kwa akili zako na usomi wako ulitegemea JPM atapendwa na mafisadi kama wewe na wanaCCM wenzako? Alijijengea maadui wengi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya raslimali za watanzania ambazo nyie kwa miaka mingi mmeshindwa kuzilinda.

Nikukumbushe tu, rais huchaguliwa na Mungu, katika mioyo yenu hamkutegemea JPM awe rais ila Mungu alimleta.


Ntarudi badae kdgo!
 
DIALLO NI MPENZI WA MUNGU KULIKO JIWE!
... at last tumepata mkweli anayeliita koleo koleo!
1625872465528.png
 
Nimefatilia interview ya Diallo, inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiishutumu serikali ya JPM, serikali iliyopambana kwa ajili ya wananchi. Naenda kujibu hoja zake kwa niaba ya JPM. Rais ambaye ntampigania mpaka kufa...
Hiyo namba 2 ni ushauri mzuri sana , unajua mwanzo nilibugi nikidhani wewe ni team jiwe kumbe ni Team Diallo uliyekuja kukongomeka msumali kwenye jeneza , hongera sana mkuu
 
Back
Top Bottom