Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,778
- 4,859
Mbona hakupiga kura ya hapana 2020 kwenye mkutano Mkuu wa kumpitisha JPM, hansadi yao inaonesha alishinda kwa asilimia mia moja kabisa.Diallo ametema nyongo ya madhila tuliyopata katika awamu ya Magufuli! Amesema kamwe tusije rudia kuchagua mtu ambaye hatuna historia yake!
Diallo ameonyesha wazi hata ndani ya CCM Magufuli hakukubalika bali ni mabavu tu yaliendelea kumweka madarakani
Diallo kupitia kampuni yake ya Sahara Media group bado anaidai CCM fedha nyingi kutokana na matangazo ya kampeni ya mwaka 2015. Pamoja na kuisaidia CCM katika kampeni lakini Magufuli aliamua kuifungia kwa muda na kuinyima matangazo ya biashara kutoka serikalini na hivyo kusababisha kuyumba kiuchumi hadi kushindwa kulipa wafanyakazi mishahara yao.
Aidha Diallo ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza amedai alionja joto la jiwe la Magufuli hivyo amewaasa viongozi kuwa na busara. Amedai kuwa enzi za Magufuli viongozi walilewa madaraka.
Kwa kifupi Diallo amewaasa viongozi kutii sheria na katiba.
Huo ni unafiki wa Diallo,na top up huyo ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. na MNEC.
Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app