Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Nakubaliana na Dr Diallo huwezi kupata katiba kwa kuwategemea wanasiasa kuongoza mchakato.Viongozi wa dini, NGO, wana academia na makundi mengine inawezekana.wana academia wanaweza kuongoza.

Uko sahihi, lakini hayo makundi uliyoyataja ni kama hayajui wajibu wao. Wako pembeni wametulia wanasubiri wanasiasa wadai katiba, kisha hao wanasiasa ndio wawape nafasi kuwepo kwenye bunge la kutengeneza katiba.
 
Diallo meongeza kwa kusema nchi imepita kwenye kiza kinene ktk kipindi cha miaka 5. Rais wa awamu hiyo hakuheshimu utu, haki na alivunja katiba wazi wazi.

Anaomba tuwe tunarejea histori za wagombea kabla ya kuwapa urais. Kamwe tusirejee tuliyoyapitia.

Sexless
JamiiForums2052770980.jpg
 
Ki ukweli mh. Diallo ameusema ukweli, JPM alikuwa katili , muuaji na mnyanyasaji. JPM alichukiwa na watu kuliko shetani. Diallo amethubutu kusema kweli , hatukujua kuwa alikuwa na file milembe hospital.
 
Mbona hakupiga kura ya hapana 2020 kwenye mkutano Mkuu wa kumpitisha JPM, hansadi yao inaonesha alishinda kwa asilimia mia moja kabisa.

Huo ni unafiki wa Diallo,na top up huyo ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza. na MNEC.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Magufuli alikuwa hashindi kwenye chaguzi, alikuwa anashinikiza atangazwe mshindi.
 
Yule mtu ni kweli alikuwa na faili Mirembe, mtu timamu hawezi sema nchi ina masaa 48! Au kudeny ugonjwa ambao ni tatizo la dunia nzima
 
Jizi kama hili nani analitaka..mkwepa kodi mpuuzi kabisaa..walifungiwa na TRA kwa kutokulipa kodi wafanyazi wengi wa star tv wakahama pale wengine walikuwa wanajitolea kufanya kazi..ebu nyie nyamazeni jpm alipambana na majitu ya ajabu..sanaaa..walikomeshwaa sasa hv yanarudi kwa kasi kama hawa kina sexless..watu waliofukuzwaa kwa kuwa na vyeti feki na wauza ngadaaa...
Note this..it will take more than a century to have someone like jpm...

Amka ww, zama za siasa chafu na utawala wa kishenzi umepita. Mama juzi si alisema watu walibambikiwa kesi na takukuru zaidi ya 147? Mwigulu si ndio huyo jana kasema kuna watu hela zao zimechukuliwa kimakosa kwenye bank? Katika mazingira hayo unawezaje kupima kwa uhalisia ukwepaji kodi wa huyo Diallo? Ni hivi, Magu alikuwa kiongozi dhalimu na muovu fullstop.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dr Anthony Diallo amesema ni makosa makubwa na hatari sana kuwaachia wanasiasa watengeneze katiba ya nchi.

Diallo amesema wanasiasa ni wabinafsi hivyo lazima wajipendelee ndio maana katiba ni lazima itengenezwe na wananchi wakisaidiwa na wataalamu kama ilivyofanyika nchini Kenya.

Diallo yuko mubashara Star tv akihojiwa na Aloyce Nyanda.
 
[emoji44][emoji44]Eeh alikuwa na file milembe

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliwahi kuambiwa, na mtu mmoja mkubwa sana katika vyombo vya usalama, ambaye kutokana na nafasi yake, ni sharti aongee na Rais kila siku, alisema, 'tuna Rais kichaa, anaweza kuua, anaweza kumfunga mtu yeyote, msidhani ni utani"

Marehemu hakuwa mzima. Kuna wakati alikuwa anakuwa afadhali, kuna wakati ilikuwa dhahiri kabisa ana tatizo la afya ya akili.
 
Nimefatilia interview ya Diallo, inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiishutumu serikali ya JPM, serikali iliyopambana kwa ajili ya wananchi. Naenda kujibu hoja zake kwa niaba ya JPM. Rais ambaye ntampigania mpaka kufa.


1. Kwanza, naomba ujue kuwa kudhamini chama kwenye kampeni hukulazimishwa, wewe kama mwanachama ni wajibu wako. Hivyo usitegemee hela ya wananchi walala hoi, ndio wakulipe pesa eti ulipigana kunusuru chama kushindwa uchaguzi 2015.

2. Eti chama kiwe kinaangalia mtu kabla ya kumuweka kuwania urais,.

Chama chenu ni cha vichaa kwa sababu mlimchagua kichaa. Ina maana hamukuona wengine mpaka mkamuona JPM? Ukweli utabakia kuwa ukweli tu, chama chenu kilikuwa kimeoza. Wananchi tuliwachoka, mlikuwa mafisadi, walafi, wezi, mlikuwa mnanuka. Mkaona mmutumie JPM ili awasafishe maana yeye alikuwa ni msafi.

Mlitegemea JPM atapotoka, na mtamuendesha...ila mligonga mwamba!

Mlitegemea atawasamehe kodi mnazodaiwa ..mabilioni ya pesa...mlitegemea atawaachia mianya muibie chama na serikali.


Eti alikuwa na ulinzi uliotisha? Hivi kwa akili zako na usomi wako ulitegemea JPM atapendwa na mafisadi kama wewe na wanaCCM wenzako? Alijijengea maadui wengi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya raslimali za watanzania ambazo nyie kwa miaka mingi mmeshindwa kuzilinda.

Nikukumbushe tu, rais huchaguliwa na Mungu, katika mioyo yenu hamkutegemea JPM awe rais ila Mungu alimleta.


Ntarudi badae kdgo!

Diallo amesema ukweli akiwa anafahamika, ww unamtetea mtu muovu kwa Id fake, weka jina lako uonekane ukimtetea yule kiongozi dhalimu. Hizi raslimali alizokuwa analinda ni zipi, mbona alipora korosho za wananchi na fedha kwenye Bureau de change, badala ya kutegemea hizo raslimali? Kama kuna raslimali za hivyo, kwanini tunabebeshwa mzigo wa kodi mara mbili mbili kwenye miamala ya simu, mafuta nk? Si muuze hizo raslimali ili zitupunguzie mzigo wa kodi?
 
Back
Top Bottom