Nimefatilia interview ya Diallo, inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiishutumu serikali ya JPM, serikali iliyopambana kwa ajili ya wananchi. Naenda kujibu hoja zake kwa niaba ya JPM. Rais ambaye ntampigania mpaka kufa.
1. Kwanza, naomba ujue kuwa kudhamini chama kwenye kampeni hukulazimishwa, wewe kama mwanachama ni wajibu wako. Hivyo usitegemee hela ya wananchi walala hoi, ndio wakulipe pesa eti ulipigana kunusuru chama kushindwa uchaguzi 2015.
2. Eti chama kiwe kinaangalia mtu kabla ya kumuweka kuwania urais,.
Chama chenu ni cha vichaa kwa sababu mlimchagua kichaa. Ina maana hamukuona wengine mpaka mkamuona JPM? Ukweli utabakia kuwa ukweli tu, chama chenu kilikuwa kimeoza. Wananchi tuliwachoka, mlikuwa mafisadi, walafi, wezi, mlikuwa mnanuka. Mkaona mmutumie JPM ili awasafishe maana yeye alikuwa ni msafi.
Mlitegemea JPM atapotoka, na mtamuendesha...ila mligonga mwamba!
Mlitegemea atawasamehe kodi mnazodaiwa ..mabilioni ya pesa...mlitegemea atawaachia mianya muibie chama na serikali.
Eti alikuwa na ulinzi uliotisha? Hivi kwa akili zako na usomi wako ulitegemea JPM atapendwa na mafisadi kama wewe na wanaCCM wenzako? Alijijengea maadui wengi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya raslimali za watanzania ambazo nyie kwa miaka mingi mmeshindwa kuzilinda.
Nikukumbushe tu, rais huchaguliwa na Mungu, katika mioyo yenu hamkutegemea JPM awe rais ila Mungu alimleta.
Ntarudi badae kdgo!