Dr. Dorothy Gwajima na makeke kama Kangi Lugola

Dr. Dorothy Gwajima na makeke kama Kangi Lugola

Dr ngwajima. Mm namuita iron lady, au mwanaume lakini anavaa sketi. Katika utendaji wake hajawahi shindwa. Amekua RMO singida hospitali ya mkoa aliweza kuifanya singida hospital ikawa hospitali ya mfano tanzania kwa kazi za kaizen. Mpaka sasa ukitaka kujifunza KAIZEN sehemu ya mfano ni singida.
Hata sasa naamini wizara zingine zitajifunza kwa wizara ya afya. Namkubali sana huyu mama. Kwa ambao mnamuona hvyo ndio anafanya kazi.
Kaizeni gani wakati dawa hospitalini Singida hakuna! hizo nadharia za wajapani sijuhi watu gani huku kwetu hazifai...siasa zimevuruka utendaji...
 
Nimemsikiliza nikacheka sana ! hivi ni kabila gani huyo mama ?

Namtabiria muda mfupi sana .
Kuna mtu amesema na mnyiramba wa shelui!! Basi wanyiramba watakuwa na bahati wakatu huu!!
1- Kitilla mnyiramba
2- Mwiguru aka madelu mnyiramba
3 - Dorothy aka makelele mnyiramba
Ukiondoa wasukuma kwenye baraza la mawaziri, kabila linalifuata kwa kuwa na mawaziri wengi ni wanyiramba!!
 
Binafsi Siamini kama Wizara ya Afya, ambayo kwa maoni yangu ni Wizara nyeti kabisa inahitaji kuwa na Waziri, ama viongozi wenye makeke, ama makelele yasiyo na tija.

Kwanza uzoefu unatuonesha viongozi wenye makeke/ makelele wala hawadumu katika nafasi zao maana huwa hawana Ufanisi wowote zaidi ya kuzurura huku na huko wakipiga makelele na kutofanikisha lolote... mfano, Paul Makonda, Kigwangallah, Humphrey Polepole, Kangi Lugola na juzi Magu amemtaja Jafo kuwa Anazunguka tu lkn hakuna Ufanisi wowote katika mizunguko yake hiyo na makelele yake.

Sasa ametoka Lugola kaingia Mmama mmoja ana makeke kweli, Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya na Mnyiramba wa Shelui, Singida. Naye anatembea na Ilani ya CCM na scarf ya bendera ya Tanzania kama Lugola na kama Mwigulu...makelele yaleyale, makeke yaleyale, mikogo ileile.

Namwona hafiki Mbali, kama wapo wa Karibu yake wamwambie atulize wenge afanye kazi kwa Utulivu na Maarifa

Asije kusema hatukusema, ana mdomo sana yan chaaa🤧
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Moto wa mabua!
Au ngoma ya kitoto, haikeshi!
 
Huyu mama yupo vizuri ni swala la muda utamkubali labda haujumiwe na watendaji wenzake ila nakuambia ni Moto toka akiwa Tamiseni alikuwa anafanya kazi sana na izo mbwembwe zilikuwepo
Si ajabu watendaji wenyewe ndio hawahawa humu, wachawi wako kazini tena mchana kweupe.Hebu tuachane na neno makeke huyo mama alichoanza kudeliver kina tija, kina ukweli ndani yake?Tuanzie hapo ili tafsir ya mlet a hoja ipate nguvu.
 
atulie aache papara nimemuona ana makeke sana na mdomo. avune busara za Ummy na Dr. Ndungulile
 
Naungana na wote wanaomkubali huyu Dr Dorothy Gwajima kwa kuwa wanayoyaandika kuhusu yeye ni ya kweli. Wale wanaoponda either HAWAMFAHAMU yaani wanaanza kumuona baada ya uteuzi or anamfahamu lakini ni WAHANGA wa uchapa kazi wake.
Nitaongeza machache ninayojuwa. Kwenye kisomo na taaluma hakuna ubishi kwa kuwa ni MD na MPH. Kwenye kazi akiwa DMO Iramba alisimamia uanzishaji wa CHF kwa wilaya nzima na alihakikisha dawa na vifaa tiba vinapatikana muda wote kwenye zahanati na vituo vya afya. Kimsingi alidhibiti wizi wa watumishi wasio waaminifu. Hiyo ilikuwa miaka kabla ya 2012.

Akiwa RMO aliweza kuwakilisha kuwa wilaya zote zinafuata mfumo wa Iramba kwenye kumbukumbu za dawa na vifaa. Hivyo basi Shirika la Afya Duniani (WHO), lilitambua kazi yake kwa kumpa tuzo ya best performing RMO mwaka 2013.

Sasa kama Dr Dorothy Gwajima pekee anatunukiwa tuzo ya performance na WHO kati ya Ma RMOs na DMOs 200 nchi nzima SISI NI NANI tum-doubt leo Magufuli kwa kumpa hiyo kazi.

Najuwa wengi wamemfahamu akiwa Assistant Director pale Wizara ya Afya na akiwa Naibu PS pale TAMISEMI. Ila katika uteuzi bora kabisa ambao Magufuli amefanya ni wa huyu Dr Dorothy.

Wanaosubiri ashindwe watakuwa ni wachawi au wanga tu. Ila naamini katika uchapakazi wake, ni mkweli sana, hapendi wizi, anachukia wavivu, siyo mtu wa majungu. Ana maadili ya kazi, ni mcha Mungu, hapendi wa Tanzania wateseke kupata huduma za afya.

Ukitaka wachukie, kama hutaki yaache ila huo ndiyo ukweli
 
Hii wizara ngumu sana....naomba nitoe mfano mmoja tu kwa leo:
Kuna hii Bima ya Afya ya Jamii CHF, wanachi wameitikia wito wa kuwa na bima hii, ila matumizi yake sasa, familia nzima ya watu watano wanenda wote kutibiwa siku moja(wote "wanaumwa" si wana bima bwana!) wanaonwa na daktari, wanaandikiwa vipimo ila ni mmoja tu mwenye minyoo, na ili kuondoa lawama ya hao ambao hawaumwi kutopewa dawa (wasipopata dawa wanaenda kwa diwani na kusema pale zahanati huduma mbovu) mganga anawapa panadol, nk
Matokeo ya ujinga huu wa watanzania walio wengi ni matumizi makubwa ya raslimali watu na fedha na mfuko huu hautaweza kujiendesha wenyewe...

Ujinga ndio ugonjwa mkubwa miongoni mwetu....
You made my day halafu kingine huu utopolo wa chif hailipwei kwa huduma uliyotoa sipokuwa ni kwa enrollment ya kaya .halafu umeshaaona wapi Bima inaeroll wateja ambao ni wagonjwa wenye maugonjwa sugu ambao kwa mweiz mtu anajitbu kwa 60000 mpaka 70000 .wew unatoa 30000 kwa watu 5 ambao ni wagonjwa kwa mwaka kama sio kituko nini
 
Nitawashangaa Sana madaktari Kama watakubali kupelekeshwa Kama waalimu,wampe tukio moja tu atulize wenge
 
Nitawashangaa Sana madaktari Kama watakubali kupelekeshwa Kama waalimu,wampe tukio moja tu atulize wenge
Huku tamisemi amewaonea sana watu kuna watu hadi wamefsrika na kuacha kazi hebu fikiria unambiwa ununue computer kila mwezi , huku wazee unawatibu bure na wamama bure halafu serikali haikupi hizo hela za kuwatobu bure halafu ule wako usema hamna dawa
 
Yaani kana piga kelele na mikwara miingi. Lakini naona no uginjwa wa media tu. Lugora yuko wapi na suti zake za bendera ya taifana ilani? Hivi bado anatembea nayo?
Binafsi Siamini kama Wizara ya Afya, ambayo kwa maoni yangu ni Wizara nyeti kabisa inahitaji kuwa na Waziri, ama viongozi wenye makeke, ama makelele yasiyo na tija.

Kwanza uzoefu unatuonesha viongozi wenye makeke/ makelele wala hawadumu katika nafasi zao maana huwa hawana Ufanisi wowote zaidi ya kuzurura huku na huko wakipiga makelele na kutofanikisha lolote... mfano, Paul Makonda, Kigwangallah, Humphrey Polepole, Kangi Lugola na juzi Magu amemtaja Jafo kuwa Anazunguka tu lkn hakuna Ufanisi wowote katika mizunguko yake hiyo na makelele yake.

Sasa ametoka Lugola kaingia Mmama mmoja ana makeke kweli, Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya na Mnyiramba wa Shelui, Singida. Naye anatembea na Ilani ya CCM na scarf ya bendera ya Tanzania kama Lugola na kama Mwigulu...makelele yaleyale, makeke yaleyale, mikogo ileile.

Namwona hafiki Mbali, kama wapo wa Karibu yake wamwambie atulize wenge afanye kazi kwa Utulivu na Maarifa

Asije kusema hatukusema, ana mdomo sana yan chaaa[emoji1784]
 
Mumemuacha wapi Jima Aweso waziri wa maji,yeye hana option nyingine tofauti na kutumbua wataalam wake
 
Back
Top Bottom