beefinjector
JF-Expert Member
- Jul 23, 2009
- 2,458
- 2,496
Hayo yote mi nayajua. Ishu niliyokuwa naijibu ni kwamba huo wimbo haukurekodiwa Aftermath bali Deathrow. Ninajua kwamba nyimbo zote ambazo Dre alirekodi Deathrow ziko chini ya Suge Publishingna Dre alipoamua kuondoka aliacha kila kitu. Lakini kingine cha msingi ni kwamba Dre aliamua mwenyewe tu kuachana na masters za The Chronic. Kusema kwamba Suge alimpiga mkwara Dre mpaka akaogopa kudai rights zake ni just an urban legend. Kama Dre angeamua kukomaa naye angeenda mahakamani na angepata haki yake. Ubabe wa Suge Knight uko exaggerated sana. By the way, Eazy E alim-sue Suge kwa kuvunja mkataba wa Dre na DOC kutoka Ruthless na alilipwa hela nyingi tu. Daz Dillinger naye alimshtaki Suge na akalipwa. Suala la kwamba Suge aliwatisha hao watu wakaogopa kudai haki zao ni stori za vijiweni tu.Kama
“ Nuthin But A G Thang “ ilikua produced at Deathrow Records
Basi nyimbo zote zinamilikiwa na Rights zake na Suge Knights aliyekua Boss wa Deathrow Records
Maana kipindi Dre anataka kutoka Deathrow afanye yake independently Suge Knight alimfanyia u mafia alimuambia aondoke kama alivyo na master zote akamuambia hana rights nazo (Fatilia Utaja Niamini Kwa Hili)
Suge alimuendea na genge la wahuni na dre anakumbuka sana tu jinsi Suge alivyomtoa na kuvunja mkataba na Ruthless Records ya Easy E ki babe na Kimafia vile vile. Suge alikua noma sanaa Snoop Dogg mwenyewe alikiri alikua anamuogopa Suge Balaa back in the days.
Carlifonia Love, Na mangoma yote Under Deathrow Dre hana rights nazo zote hzo...forgot about dre na still dre zile ni chini aftermath wakati huo dre tayari yupo independent.
Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app