Soma alichosema Sumaye. Chanzo ni Mwanahalisi online
Wakati huohuo, Waziri Mkuu mstaafu awamu ya tatu, Frederick Sumaye amesema moja ya sababu kubwa zinazomfanya mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kukosa sifa ya kuchaguliwa, ni kukurupuka katika maamuzi.
Akizungumza katika viwanja vya Tanganyika Packers, jimboni Kawe, Sumaye amesema zipo rekodi nyingi za Magufuli zinazothibitisha kuwa amekuwa mkurupukaji na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa taifa.
Hata mwenyewe amekata tamaa, ameanza kutetea safari za nje za Mheshimiwa Kikwete, hivi rais anawezaje kukaa nje ya nchi kwa zaidi ya nusu ya muda wake aliokaa madarakani? Haiwezekani hizo safari zote zikawa na manufaa kwa Watanzania, kwa kutetea kwake safari hizi, kuna hatari na yeye akafuata mkumbo huohuo, amesema Sumaye.
Nchi hii Lowassa akiingia madarakani zaidi ya Sh. bilioni 900 zinatakiwa zilipwe kama faini kwa kuchelewesha kuwalipa wakandarasi, hasara hii imesababishwa na Wizara ya Magufuli na kuna hasara kuhusu meli aliyoikamata ambayo serikali imeshindwa kesi na kudaiwa fidia ya Sh. Bilioni 3.2, amenunua meli mbovu na chakavu akidhani ni mpya, leo hii kwa aibu ile meli haifanyi kazi tena Dar, amesema.
Ni mtu huyuhuyu ambaye alitaka kubomoa mpaka jengo la TANESCO wakamuwahi na kumshika shati, yeye hajui kama hilo jengo ni mabilioni ya walipa kodi yametumika kujenga, anajua kubomoa tu matokeo yake mpaka wanamshika shati alishabomoa jengo la serikali la TANROAD na katika kuthibitisha kuwa zilikuwa pupa jengo hilo limeanza kujengwa upya palepale lilipovunjwa, amesema kabla ya kuongeza:
Magufuli ni mtu wa maamuzi ya pupa sana. Katika nchi zinazofuata utawala bora alitakiwa kulipa hizo gharama
sasa huyu anataka urais, tumeona akiwa waziri tu anakurupuka na watu wanawahi kumshika shati, hivi akiwa Rais nani atamshika Rais shati?