Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Jiwe bhana! Kwa hiyo baada ya kumfukuza kazi alitaka mama wa watu asiajiriwe tena! Yaan angelialia kama yule jamaa aliyekuwa RC Morogoro kipindi kile! Roho mbaya tu.....
 
Katika hili Magu is right mbona hako kagonjwa alikosema mbombezi wa magonjwa hakakuendelea? Au aliondoka nako? Maana mwele dr alikuwa sahihi tungeendelea kusikia ama kushuhudia watu wakifa. Lakini kimyaaaa
 
Yes, she is well educated lakini kama mkurugenzi wa taasisi kubwa ya tafiti za magonjwa aliteleza kutoa taarifa ya ugonjwa mkubwa kama Zika bila wakubwa wake kuwa na taarifa...(siamini kabisa kama anatumiwa na mabeberu)

Inaonekana watu hawaijui sana Zika, hivi mfano ingekuwa ni ugonjwa kama Ebola hivi, kabla ya mtu wa taasisi ya NIMR kuutangaza unadhani Ikulu isingejulishwa kabla?

Hizi Pandemics huwa zina kautaratibu wake wa namna ya kujulisha umma...
Alisema kuna dalili za ugonjwa wa ZIKA not kuna ugonjwa wa ZIKA
 
Hapa naona watu wameishia kunanga PhD tu..Lakini tumeshindwa kujibu kile alichohoji Mh Rais?je Zika iliishia wapi?Au Dr.Mwella aliondoka nayo kuirudisha UN-WHO?Mimi nataka kujua kama ilikuwepo ilimalizikaje?
Haikuwepo na Dada Mwele Malechela alisa zipo dalali
 
Thesis ya PhD ya Dr Mwele Malecela ipo hata uki google tu unaipata London School of Hygiene and Tropical Diseases.
ya bwana mkubwa ile ya maganda ya korosho inapatikana wapi dada sky?. nataka kuisoma.
 
Hapa naona watu wameishia kunanga PhD tu..Lakini tumeshindwa kujibu kile alichohoji Mh Rais?je Zika iliishia wapi?Au Dr.Mwella aliondoka nayo kuirudisha UN-WHO?Mimi nataka kujua kama ilikuwepo ilimalizikaje?
Ivi yule Mama alisema kuna zika au kuna vimelea vinavyoweza kusababisha zika? Mfano TB, unaweza ukawa na vimelea vya TB Ila huna TB. simtetei, simtetei kwa sababu angewasiliana na mkuu wake kabla ya kutoa ripoti. All in all pamoja na kosa alilofanya, naamini MUNGU wetu bado yu mwema kwake na ameendelea kumbariki.
 
Dr Malachela si alitudanganya adharani, kwanini Raisi asituambue wananchi ukweli, Tataizo la magifur mkweli ukizungua anakupa makavu ujijue.
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
 
Mwafrika ata awe PhD bado njaa zina waendesha, wapo dhaifu sana kwa watu weupe
Thesis ya PhD ya Dr Mwele Malecela ipo hata uki google tu unaipata London School of Hygiene and Tropical Diseases.
 
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
Tatizo mabeberu tukinunua ndege, tukijenga reli, tukijenga barabara kwao sio stori ya maana. Cha maana kwao ni rais kumpongeza rc kwa kuchapa viboko. Unafiki tu.
 
Aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Bi.Mwele malecela ameposti katika akaunti yake ya twitter maneno haya. Nadhani huu ni mrejesho baada ya tamko la Mwenye nyumba kuwa Daktari Mwele malecela alikua anatumika na MABEBERU.

View attachment 1223939
View attachment 1223982
View attachment 1223983

=====

RAIS John Pombe Magufuli, amesema moja ya sababu kumtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya NIMR, Mwele Malecela, ni kiongozi huyo kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusiana na ugonjwa wa Zika.

Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Songwe, wakati alipofika kwenye ziara ya kikazi na kufanikiwa kuzindua kiwanda cha kahawa kilichojengwa na wajasiriamali wa Tanzania, ambapo amesema moja ya mambo ambayo yalipelekea kumtoa kwenye nafasi hiyo Malecelea ni kutangaza ugonjwa.

“Maneno huwa hayaishi, kuna wakati walitangaza kuna ugonjwa wa Zika nchini Tanzania, alipotangaza hivyo wakati mimi najua haupo nilimfukuza saa 7:30 usiku, wala hakuna cha Zika iliyotokea. Baada ya wiki moja wakamteua akawa bosi wao, hii ilionyesha alitumwa kusema aliyoyasema; hizi ni mbinu za kibeberu,” amesema Rais Magufuli.
Na prof Ndullu naye kateuliwa na beberu Ramaphosa?Kuutanģazia u.mma magonjwa ya mlipuko inahitaji umakiini kwan inaweza kuleta athar za ķiuchumi hata hvy Rais Magufuli mpk saiz hajajua uķubwa wa nafas yake yey anaropokà. ق نو
 
TOKA ALIPOFUKUZWA MWALE, NI TAASISI GANI ILIFANYA UCHUNGUZI NA MAJIBU YALIPELEKWA WAPI?.

SHERIA YA TAKWIMU ILITUNGWA KWA AJILI YA NINI?

KUFANYA KILA KITU SIRI.
Kulikuwa hakuna kitu cha kuchunguza in the first place. Ugonjwa wa Zika sio wa kuugua kisirisiri. Ni wa wazi. Niambie wewe mwenye taarifa "sahihi" ni Watanzania wangapi wameishaathirika na huo ugonjwa? Nijibu ukizingatia naishi huku ambako Dr. Mwele alifanya utafiti wa huo ugonjwa.
Haya kuhusu Ebola. Hivi kweli unaweza kuuficha na usikuumbue? Toka Serikali imesema hakuna, wachunguzi huru wameonesha "hatari" gani ya huo ugonjwa hapa nchini?

Ushauri wangu, tujenge tabia ya kuwaamini viongozi wetu. Kufikiri watu wa nje ndio wako sahihi kuliko viongozi wetu ni myopic ya hali ya juu. Wairaq waliaminishwa na watu wa nje kuwa Saddam ni mtu mbaya, leo wanajuta. Walibya waliambiwa hakuna mtu katili na anayewauwa Walibya nchini mwao kama Gaddafi. Wakamuuwa. Leo wanachinjana zaidi ya kuku na Gaddafi hayupo!

Tafakari!
 
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
Heee tuache kuongea mambo yetu kwa Uhuru kisa tutajadiliwa na media za mabeberu? Who cares? Sisi kuongea tuogope ila wao kuingiza majeshi na kuua raia na kupindua serikali za kiafrika kama Libya ruksa?

Waafrika tuna safari ndefu kiukweli ninyi ndio wakina tundu mwishowe mtuletee ushoga kisa beberu kaagiza, mkufilie mbali kabisa na vizazi vyenu visije pata mamlaka
 
Back
Top Bottom