Dr. Umar Johnson aihama Dini ya Kiislamu

Dr. Umar Johnson aihama Dini ya Kiislamu

Hii ni Lugha yetu ya KIAFRIKA.

Lugha ya kiafrika! Unaijua hii lugha imetokana na nini? Hapo zamani enzi za mababu zenu hata kuvaa walikua hawajui kuvaa, wala usafi, wanawake wakiwa hawajistiri, ustaarabu ni ZERO. hebu jiulize ni akina nani walikuja kuwatoa katika ujinga na kuwa wastaarabu mpaka umejua kujisafisha, kuoga, kusoma na kuandika kiswahili n.k!????
 
645d4f17ecbd3d001d512e6c.jpg

Wisdom of ancestors
 
young-african-arab-on-white-260nw-22247143.jpg

Huu sio Utamaduni wa Kiafrika
 
Kiswahili ni Kibantu na kimeazima baadhi ya maneno kutoka kwenye lugha nyingine.
Bado sana wewe, kaa na wazee wanaojitambua na wanaoijua historia watakupa ukweli, hizo hadithi za shule ya msingi msiwe mnatuletea humu, mara sijui babu zetu waliteswa mara sijui nini! Mnachekesha sana
 
Hizi nyingine ni sarakasi lakini ukweli ni kwamba Uislamu unaenda Bega kwa Bega na Arabization.
Nimekuuliza ikiwa uislamu unaenda sambamba na Mila na desturi za kiarabu, ni kwanini waarabu walimpiga vita mtume Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم hadi kufanya mipango ya kumuua.?!
Ukitaka kuukosoa uislamu nunua vitabu vya kiislamu ambavyo vinapatikana kwa lugha zote hasa kiarabu, kiswahili na kiingereza uusome uislamu uuelewe misingi yake pamoja na historia yake.
Hapo hata kama unataka kukosoa utakuwa unakosoa kitu ambacho unakielewa vizuri kuliko kuzungumza maneno ya mihemko bila ushahidi wowote.!
Nenda Kariakoo msikiti wa mtoro ulizia duka la vitabu Kisha ukifika dukani waambieni unataka kitabu kinaitwa
"MAISHA YA NABII MUHAMMAD kilichoandikwa na chief kadhi wa Kenya Sheikh Abdallah Saleh Al farsiy"
Ukisoma kitabu hicho utakuwa na mwanzo mzuri wa kuujua uislamu na historia yake hata ukitaka kukosoa utakosoa kwa ushahidi.
Na kitabu hicho pia kitakusaidia kujua tafauti ya misingi ya kiislamu na kati yake na Mila na tamaduni za kiarabu.
Kupitia kitabu hicho utaelewa kwamba Mila za wazee wa kiarabu wa miaka hiyo hazitafautiani sana na Mila za mababu zako wa kimakonde.
 
Bado sana wewe, kaa na wazee wanaojitambua na wanaoijua historia watakupa ukweli, hizo hadithi za shule ya msingi msiwe mnatuletea humu, mara sijui babu zetu waliteswa mara sijui nini! Mnachekesha sana
Umeishiwa na Hoja
 
Nimekuuliza ikiwa uislamu unaenda sambamba na Mila na desturi za kiarabu,
Kuazini KIARABU Quruani KIARABU kuswali unasoma KIARABU nk.

Kwanini niseme KIARABU wakati MUNGU ni wa WOTE?!
 
Na UISILAMU NI DINI YA WANYWA KAHAWA vipi hapo?!
Sasa wewe kweli unalinganisha kahawa na BANGI?!😆😆😆😆😅😅
Mbona unalinganisha kahawa na vitu vya ajabu?!
ACHA KAHAWA IENDELEE KUITWA KAHAWA AISEE.
Kinywaji murua kabisa hasa asubuhi.
Kule kwetu mkoani Kagera akina Kaijage na Rugemarira wanatafuna kabisa inaitwa "AKAMWANI" na Muhaya akina Dar es salaamu Moja ya zawadi hauwezi kusahau kuwaletea ndugu zake wahaya ambao wapo Dar ni kahawa iliyolaushwa kwa ajili ya kutafuta.
HIYO NDIYO KAHAWA.
 
Kuazini KIARABU Quruani KIARABU kuswali unasoma KIARABU nk.

Kwanini niseme KIARABU wakati MUNGU ni wa WOTE?!
Mbona shuleni tunajifunza kwa kiingereza wakati Kodi tunalipa makabila yote?!
 
Ujuaji wa kijinga,ingekua ndiyo mavazi yao Quran isingeamuru wavae,suruali fupi ni itikadi za sheikh wahabi za kuhuisha sunna, sheikh wahabi alikua mtawala wa saudia ikiitwa hijaz kabla ukoo wa al saudi hawajapewa nchi na mwingereza na kubadili jina la nchi kuwa saudia, pakistan na afghanistan ni wahabi,hijab za kufunika nyuso ni uzushi wa kiwahabi kinyume na maelekezo ya hijabu ndani ya Quran
Bro; unafahamu hayo mavazi yameanza kuvaliwa mashariki ya kati kabla hata Quran haijulikani ndio kitu gani duniani? Hayo ni mavazi ya mashariki ya kati; Waarabu na Wayahudi wamekua wakivaa hivo kabla ya Ukristo na Uislam
 
Kuazini KIARABU Quruani KIARABU kuswali unasoma KIARABU nk.

Kwanini niseme KIARABU wakati MUNGU ni wa WOTE?!
Lugha ya kiarabu ni Lugha ambayo inawaunganisha waislamu Dunia mzima. Mimi 90% ya elimu yangu ya dini nimesomea hapahapa TZ lakini naweza kwenda China , Japani, Australia , India , Naijeria na nchi yoyote duniani na nikaongoza ibada bila shida yoyote.
Sisi waislamu tunaamini kwamba makabila na mataifa yote yameumbwa kutokana na Adamu na Hawa na watu wote ni sawasawa.
Allaah katuchagulia mtume ambaye ni mwarabu na kaifanya lugha ya kiarabu kuwa ndiyo lugha ya kufanyiwa ibada ya swala.
Sisi tumeamini na kuridhia utaratibu tuliowekewa na Mola wetu kupitia mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم.
Tumeridhia Allaah kuwa ni MOLA WETU.
Na Muhammad ni MTUME WETU.
Na uislamu ni DINI YETU.
Na Kaaba ni KIBLA CHETU
Na waislamu wa mataifa na makabila yote wanaume na wanawake ni NDUGU ZETU.
Na Quran ni KITABU CHETU.
Na pepo ya Firdausi ni LENGO LETU.
Wala kelele za makafiri hazitusumbui wala hazitubabaishi hata kidogo.
 
Lugha ya kiarabu ni Lugha ambayo inawaunganisha waislamu Dunia mzima. Mimi 90% ya elimu yangu ya dini nimesomea hapahapa TZ lakini naweza kwenda China , Japani, Australia , India , Naijeria na nchi yoyote duniani na nikaongoza ibada bila
Maadamu malengo ya kusali ni kumuabudu MUNGU NGAI sisi Waafrika tutumie Lugha zetu.

Hata Waturuki wameoindoa Lugha ya Kiarabu kwenye Shule zao ili kuepukana na Arabization.
 
Kuazini KIARABU Quruani KIARABU kuswali unasoma KIARABU nk.

Kwanini niseme KIARABU wakati MUNGU ni wa WOTE?!
Hoja yenu ya kupinga ibada za kiislamu kuendeshwa kwa kiarabu Haina maana hata kidogo.
Kupitia lugha ya kiarabu waislamu Dunia nzima wanakuwa kitu kimoja kwa kuwa mifumo yao ya kiibada inafana.
Lau tungeruhusu angalau kwa hapa TZ ibada ziendeshwe kwa kiswahili kwa madai kwamba kuendesha ibada kwa lugha ya kiarabu ni utumwa! Baada ya muda Kuna makabila yangetaka kuendesha ibada kwa lugha za makabila yao kwa madai kwamba kuadhini na kuswali kwa lugha ya kiswahili vilevile ni utumwa!. Matokeo yake wahaya wangeswali kwa kihaya, wamakonde kwa KIMAKONDE, wanyaturu kwa kinyaturu, wasukuma kwa kisukuma, wakurya kwa kikurya , wachaga kwa kichaga na wao wachaga wamegawanyika Kuna wanaoongea kichaga kimarangu, kimachame, kibosho, kirombo,nk na hapo ukweli ingetokea kuwa dini yenye mfumo wa ibada uliovurugika lakini pia ingekuwa njia rahisi kwa maadui wa uislamu kupotosha mafunzo ya uislamu kupitia lugha zao kwa kuleta tafsiri ambazo zipo kinyume na alivyofunfisha mtume Muhammadi صلى الله عليه وآله وسلم.
 
Back
Top Bottom